Chekechea na Primary nimesoma english medium private.
Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.
Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.
Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ? Kwa jinsi wazazi walivyonipambania maisha ya shule yawe mepesi kweli watoto wangu waanze kwenda kayumba ?
Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba, wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?
Hivi hata wazazi watanichukuliaje ? wamepambana nisome kwa raha kisha wajukuu wao niwasomeshe kayumba ??
Kwa mfano mwepesi, hata kama ulisoma kayumba, kwenu ulikuwa unakula milo mitatu, ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane kuhakikisha watoto wanakula milo mitatu, vinginevyo utajihisi vibaya, nafsi haitakuwa na amani, utajisikiaje wazazi wako au ndugu zako wa karibu wakijua ?
Nina watoto watatu napambana mno watoto wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
Hadi sasa napambana sana japo kipato si kikubwa.
- First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
- wa pili yupo Primary day ada laki 9.
- Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
- Sina mpango wa kuongeza mtoto wa tatu labda uchumi ukae sawa
Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni, Suala la kufaulu wapo mpaka wanafunzi wanaokaa kwenye sakafui darasani wanapasua vibaya mno.
- Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
- Chakula kizuri shuleni
- Mazingira tulivu
- Usafiri shuleni hadi nyumbani
- kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
- Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
- Hakuna kujazana darasani
- kujifunza computer utotoni
- Library
- masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
- Marafiki wengi hutokea familia zinazojali malezi
- n.k.
Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.
Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za mafuta, wife ana passo, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga