Kutoka kwenye familia tuliyosomeshwa kwa gharama kubwa kumeniathiri kiuchumi, Kupeleka watoto kayumba ni aibu, Napambana kukwepa aibu

Kwahiyo unasomesha English Schools kwa presha/hofu tu ila sio matakwa yako, kwa maana ungekuwa uko huru wanao wangesoma Kayumba?
naomba nikupe mfano mdogo tu mkuu, wewe kwenu mlikuwa mnakula milo mitatu kila siku, hutajihisi uchungu watoto wako wakila milo miwili ?
 
Mkuu shule sio muhimu sana kumpeleka private kitu muhimu ni ku spend muda na mwanao. Hakikisha bia yake ya kwanza anakunywa na wewe. Kaa nae karibu mfundishe jinsi ya kuwa mwanaume. Shule ni muhimu lakini watoto wa wasiojiweza wanatoboa kwa sababu wazazi wanakaa karibu na watoto.
 
Mtoto wa Kayumba form anapata division one, wewe umetumia miaka minne kulipa school total million 20 halafu mtoto anapata division two.

Wazazi tuanze kutumia akili, wazazi wengi hawana akili hata kama wana degree.
Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni kuzidi ufaulu.

Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno
 
Tafadhali kaka usipambane kwenye maisha kukwepa aibu, Bali pamban kutimiza malengo.
Aibu haziishi kiongozi ila malengo unaweza kuyatimiza.
 
Tafadhali kaka usipambane kwenye maisha kukwepa aibu, Bali pamban kutimiza malengo.
Aibu haziishi kiongozi ila malengo unaweza kuyatimiza.
Kwa mfano mwepesi hata kama umesoma kayumba lakini ulipambaniwa ule milo mitatu (breakfast, lunch na dinner), ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane kuhakikisha watoto wanakula milo mitatu, vinginevyo ni aibu yako binafsi hata kama utaifanya iwe siri.

Mtu aliekuzwa kwa milo miwili kwake kawaida kuja kulisha watoto milo miwili, akikwambia na wewe uwalishe watoto milo miwili ni ngumu kumuelewa.
 
Hongera sana kwa kuwa na mawazo mema kwa familia yako, hongera sana kwa kuweza kupata mke anaeweza kusikilizana na mkakubaliana kwa yaliyo mema kwa maisha yenu na vizazi vyenu, naomba sana mumtumainie sana Mungu ktk mawazo yenu ili myatimize na kuwaombea sana watoto wenu waweze kuwa watiifu na wakamilifu ktk yale mnayo waongoza na kuwafunza, mbarikiwe sana.
 
unachokizungumza ni sawa, ila kwako inakuwa kama mateso, yaani mzigo umekuelemea, kiuhalisia hatutakiwi kuwafanya watoto waishi maisha tuliyoishi sisi, yaani kama sisi tulisoma kayumba basi walau watoto wetu wasome hizo za medium, na kama sisi tulisoma medium watoto wetu wasome zile za kulipa kwa dola yaani international, na hiyo inatakiwa iwe within yourself sio kwa sababu baba alinisomesha medium basi na mimi nalazimika nimlipie mwanangu medium kwa presha ya wanaonizunguka lakini si kwa sababu nina nia hiyo
 
Za dollar ni International schools zenye mitaala ya cambridge hawafati mtaala wa necta,

ni bei sana mwaka moja pekee ada ni milioni 20

Kina P Funk na Master J walisoma huko nao wanawapambania watoto wasije kugusa mitaala ya necta, Master J aliwahi kusema alikuwa na uwezo wa kununua V8 lakini aliamua kusomesha
 
Hard times creates strong people.

Strong people create easy times.

Easy times creates lazy people.

Hivi ndivyo cycle ya poverty ilivyo.

Unavyompa mwanao good times sana ndivyo unavyomfanya kuwa maskini.
 
Kupanga ni kuchagua. Hayo uliyoyaorodhesha, ukiachilia usafiri niliyapata sekondari ya Usagara- Tanga, ya Serikali.
Kusema shule binafsi, hakukuzuii kufanya uchunguzi wa shule ipi ya Serikali unaweza kutoa huduma nzuri.
 
kujenga au kujijenga?
 
Mtoa Mada Sijakuelewa kumbe unajibana ili ujenge Sasa kwann unalalamika? Mi nikajua umepauka hta mia huna , kazi huna na kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…