Kutoka kwenye familia tuliyosomeshwa kwa gharama kubwa kumeniathiri kiuchumi, Kupeleka watoto kayumba ni aibu, Napambana kukwepa aibu

Mtoto wa Kayumba form anapata division one, wewe umetumia miaka minne kulipa school total million 20 halafu mtoto anapata division two.

Wazazi tuanze kutumia akili, wazazi wengi hawana akili hata kama wana degree.
Duh leo Dokta Manyaunyau umeongea pwenti
 
Wewe wazazi wako wanajivunia nn kutoka kwako ?
Maana wanasema utakachowatendea wazazi wako ndicho watoto wako watakutendea
Kwakweli sijui ndgu yangu, hilo wanajua wao mioyoni mwao ila nachoshukuru Mungu ni kua hawakua wanalalamika kama wazazi wa miaka hii, wala kua na stress za ada na malezi.
 
Ofcourse kama nimesoma shule bora siwez peleka wanangu Kayumba. Wazazi walipambana, namimi lazima nipambane
 
Tofauti ya english medium na kayumba ni ndogo sana kiuhalisia ila binafsi huwa naona.
English medium zinaigiza maisha ya kizungu ihali sisi si wazungu na (kifupi hawa watoto ndio wakikua wanaleta stress kwenye falimia zao wanaforce kuishi kizungu) na kayumba zinaishi kiuhalisia kabisa kulingana na mazingira yetu.
 
Watoto kusoma ama kupata elimu nzuri ni wajibu wa mzazi lakini hakuwezi kunifanya nikose usingizi ni wapi wapate hiyo elimu. Kulingana na kipato chร ngu wanangu watasoma mahala popote. Thanks
 
Try to be open minded usitumie nguvu kubwa kubishana kwa mifano na mawazo yawatu yatakayoweza kukupatia idea nzuri nn ufanye

Maana at the end of day ni ww na familia yako mkuu na chaguo ni lako ufanyeje

Kwa kuleta mada kunakitu umeisi hakiendi sawa sasa acha sindano ziingie ,kupona kwake ukae chini na mawazo yaliyotolewa na members afu upate conclusion yaunachoisi hakipo sawa kwa unachofanya now
 
Kweli mkuu pambana ufanikishe hilo kusudio lako, tuliosoma Shule za kata tumeshuhudia uozo mwingi sana wa Elimu na ukijitia kuhoji tuu unashutumiwa ni Usalama wa taifa

Shule za kata walimu wengi ni vigagula( wachawi) hata vile wqnafunzi wanafail kwao ni Furaha kwasababu wao wenyewe watoto wao hawasomi hizo Shule
 
Pambanania broo kikubwa focus asee,make sure vijana hawateseki
 
naomba nikupe mfano mdogo tu mkuu, wewe kwenu mlikuwa mnakula milo mitatu kila siku, hutajihisi uchungu watoto wako wakila milo miwili ?
Swali langu la msingi hujalijibu kwenye huo mfano wako, ingekuwa uko huru hubanwi na historia ya makuzi yako..... wanao ungesomesha Kayumba?
 
Dadeki noma sana.

Hivi watoto huwa wanawasaidia nini maishani?? Zaidi ya wengi kulalamika, sionagi watu wakisifia uwepo wao.
(Tafiti nimeifanyia jf na mtaani)
Duh! Mbona wanitoa kwenye kona? Kwangu furaha kubwa kuliko zooote, ni kuwa na watoto wangu pamoja. Nagamani niwe nao wengi iwezekanavyo.
Mtoa mad hongera kwa mpango wako. Ila ongeza watoto taf walau wafikie 5
 
Duh! Mbona wanitoa kwenye kona? Kwangu furaha kubwa kuliko zooote, ni kuwa na watoto wangu pamoja. Nagamani niwe nao wengi iwezekanavyo.
Mtoa mad hongera kwa mpango wako. Ila ongeza watoto taf walau wafikie 5
Ndo msilalamike sasa, na pia msione ugumu kuwapa wakitakacho.

Na siku nyingine mje na nyuzi kuwasifia watoto wenu, sio za lawama tu.
 
Mwisho wa siku kariakoo ni suluhisho la kila kitu
 
Swali langu la msingi hujalijibu kwenye huo mfano wako, ingekuwa uko huru hubanwi na historia ya makuzi yako..... wanao ungesomesha Kayumba?
offcourse ningeweza kuchagua wasome kayuma ama private.

Kama ningekuwa nimesoma kayumba ningekuwa na uzoefu kwenye mazingira, changamoto, wanafunzi, n.k. hivyo ningeweza kumpa ushauri mtoto jinsi ya kuweza kufit kwenye hizo shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ