Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Unakimbia Marekani unarudi Africa, eti kisa ni MuAfrica,ukibahatika kutoka katika bara hili la giza nenda ukakaze huko na hakikisha haurudi nyuma. anyway acha ateseke,hili ni funzo kwa vijana wa kileo.
Floyd Mayweather hataki kabisa mazoea na waafrica.
 
Kuna jamaa zangu wawili mtu na kaka yake nawashangaa sana nao wamerudi bongo hawana hata Mia mbovu
Mmoja kauza kiwanja chake akajirusha hela yote mwingine kaanza kufuga njiwa
Nachoka kabisa
Kumbe hata wanaoendaga mambele huko na taaluma zao huwa wanafeli maisha? Nilijua mimi tu nimeshindwa kujiongeza
 
Mambo ni mengi huku Africa, sometimes unakuwa celebrated ukiwa juu, the day you fail you're done.

attitude yako pia ukiwa juu ina changia hilo, ukiwa mzee wa kusalimia umefunga vioo kazi unayo!
 
Natoa uzoefu kidogo na nilichojifunza kuhusu kuishi ughaibuni, naongelea Marekani ninapopajua zaidi!

Waafrica wengi sana regardless anatoka nchi gani wanapata shida sana ya kuadapt mazingira ya nchi zilizoendelea kwa sababu moja tu kuu "emotional attachment" na nchi tulizotoka. Yani tunashindwa kukubali psychologically kwamba hatupo tena nyumbani na maisha ni popote tufanye maisha kama vile ndio ushanunua kiwanja na kujenga hapo ndio kwako, yani kama unabyohamia Mbeya, Songea, Kigoma, Kibosho mk, panakua ndio kwako hadi mambo yatakapobadilika, tunaamini ipo siku tutarudi nyumbani permanently na tunatakiwa kuwekeza huko ili tusijeaibika, tuwe na sehemu ya kuishi na pia tuwaonyeshe tuliowacha nyumbani kwamba tupo nje na tumeshafanikiwa (kuwakoga) yani wanaotujua waone kwamba tupo tofauti sasa.

Matokeo ya hii emotion tunajikuta tunapiga kazi sana na kutuma sana miamala nyumbani "tufanyiwe" kitu na tunaowaamini, unakuta mtu katuma pesa 10yrs anajenga nyumba ya kuishi na haijakamilika, huku US anateseka ile mbaya, yani hana maisha ng'ambo wala nyumbani. Ni kazi mchana na usiku iwe profession au mpiga box wote hali moja. Hii inafanya tuumize credits zetu na kujikuta tuna madeni makubwa, hatuna assets zaidi ya gari ughaibuni, credits zikiwa mbovu tunapata mikopo ya riba kubwa sana na hatuna motivation ya kulipa kwa wakati kwa kuwa tunaamini muda utafika tutaondoka (who cares). So unakuta mtu kakaa miaka 15 hana nyumba Marekani na nyumbani haijakamilika kwa kuwa anayemsaidia pia anampiga na kuinflate sana costs na hii kama huyo msaidizi ana nia njema, otherwise hata msingi hutaukuta.

Huko US ukiwa na credits nzuri una access ya resources za kutosha kila mahali na kila biashara inakuita ikuwezeshe na kwa riba ndogo sn wakati mwingine hata 0%. Ukiwa na 700+ credits kwa mfano unaweza kuchukua mkopo wa Small business authority (serikali) wa hadi $5m kwa kuwa na business plan na 10% downpayment, ukipata mzigo kama huo ni biashara gani utashindwa kufanya duniani?? Hapo hujagusa opportunities zingine maelfu za serikali ya federal, State, angel funders, ushindani, ubunifu, minority, za makanisa na dini zingine, marafiki, wawezeshaji wasiotaka kujulikana, zote hizi zinazokutafuta kila siku.

Maelezo mengi sana na nitarudi na personal experiences, sijitoi kwenye hali hiyo na nimeshtuka late sana baada ya kutoil sawasawa!
 
Mjinga kabisa. So alitaka kurudi Kenya bila kujua taratibu za Kenya na kujipanga?

15 years kua Marekani ndiyo marafiki wapotee?

Scenario inayomake sense ni jamaa alirudi na mpunga akili za mtoto wa maskini akataka kuwaoshea wenzake na hapo ndipo alipoteza marafiki. Mpunga unaisha anataka arudis taaluma yake ndiyo hayo mengine yakafuata.

Alirudi ili asilisaliti kanisa la Methodist? Ambalo uanzishwaji ni huko Marekani. Why not going to them again? Kenge kabisa
 
Mambo ni mengi huku Africa, sometimes unakuwa celebrated ukiwa juu, the day you fail you're done.

attitude yako pia ukiwa juu ina changia hilo, ukiwa mzee wa kusalimia umefunga vioo kazi unayo!
Hakuna cha attitude, binadamu wengi hasa wanaokufahamu tangu una-hustle huwa wanakuwa na chuki ukitoboa hususan wale waliokuwa wanakuchukulia poa na kuhisi kuwa wao wako more likely kutusua kuliko wewe labda wakilinganisha connections zao au standards mlizokulia. Utakuta madogo wako baa wanakunywa lakini story ni "jamaa yuko mambele lakini sisi kuna-enjoy zaidi yake" wakati huyo mtu wanayemuweka kikao hata kuwawaza hawawazi yuko busy na maisha.
 
Very emotional
 
You couldn't have said better than this
 
A very touching story indeed.They normally say from rags to riches bt in this case it's vice versa,from riches to rags.

Ila nachokipenda kwa huyu jamaa ni kwamba bado ni mpambanaji hajagive up kbsa na kuwa omba omba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…