Kutovunjwa bunge Leo Hadi hapo August, ni ishara ya kufanyika reforms kupata katiba mpya?

CCM itapata pigo kubwa sana mwaka huu, pigo moja tu,pigo lililonyooka,pigo takatifu
 
Salaam!

Bunge halijavunjwa, limeahirishwa tu,

Sasa Nini kimelengwa hapo?

Ni kudhibiti wahamaji au ni mpango wa reforms kupata tume huru ya uchaguzi?

Karibuni 🙏
Hizo reform zitafanyikaje wakati shughuli za bunge la 12 zimesitishwa? Linavunjwa mwezi wa nane ili kuendeleza shughuli za mawaziri.
 
Vipi kuhusu baraza la mawaziri na kuvunja bunge?..miaka yote ya uchaguzi bunge lilivunjwa julai?
Baraza La mawaziri bado Hubaki Kufanya Kazi mpaka Litakapoapishwa Baraza Jipya...

mKuu Tambua Haya..

1. Serikali haivunjwi Rais anaendelea kuwa madarakani

Rais wa Jamhuri ya Muungano anaendelea na madaraka yake hadi rais mpya atakapoapishwa (Ibara ya 37(5)).

bunge sio Moja ya Serkali kwahyo hakutakuwa na ombwe la uongozi wa juu serikalini.

2. Mawaziri wanaendelea kushika nafasi zao

Mawaziri, pamoja na Waziri Mkuu, wanaendelea kufanya kazi kwa kipindi kifupi hadi serikali mpya itakapoundwa, japokuwa wanakuwa kama "caretakers" yaani wanatekeleza majukumu ya msingi tu bila kufanya maamuzi makubwa ya sera.

Ibara ya 51(2) inaruhusu Waziri Mkuu kuendelea kushika wadhifa hadi rais mpya atakapoteua mwingine.


3.Kama Hakuna Bunge Mambo ya Sheria Mpya na Bajeti hayafanywi

Kwa kuwa hakuna Bunge, hakuna sheria mpya zinazopitishwa, wala mijadala ya kibunge kufanyika hadi uchaguzi mkuu ukamilike na Bunge jipya lifunguliwe rasmi.


4. Madaraka ya Serikali yanadhibitiwa

Serikali inaendelea kutekeleza majukumu ya kawaida (routine functions), lakini haipaswi kufanya maamuzi makubwa (major policy decisions) hadi serikali mpya iundwe baada ya uchaguzi.
 
Ahsante Wakili kutusanua.
 
Bunge la zanzibar nalo wameahirisha,nako kuna reforms?
 
Ipo kikatiba kwamba ukivunja bunge then ndani ya siku 90 lazima uwe na bunge jipya..So election ni Oct..do the math..hana jilya huyo mama ndugu zangu hapa ni kukoleza No refirms no Election!
Ibara ya 90(2)(b) ya Katiba:

"Rais atavunja Bunge ikiwa uchaguzi wa Rais au wa wabunge utafanywa ndani ya siku tisini baada ya kuvunjwa kwa Bunge..."
 
Wabunge wamepiga makelele na kulalamikia Nini?

Uamuzi huu hawakuupenda,

Nadhani kuna mipango yao immeharibiwa.
 
Mimi sio mwanasiasa ila hili la kuhairishwa ni mwiba mkali kwa wabunge maana huenda pia stahiki zao zitachelewa wakati huo mchakato wa kura za maoni unaendelea ambapo wengine walikuwa wanasubiri hizo pesa ili wapitishe takrima kwa wajumbe.
Mchakato wa uchaguzi unasimama,yaani raisi akivunja bunge ndo vacant zinakuwa wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…