Kuuliza si ujinga: Hivi Diwani Athumani kashuka au kapanda?

Kuuliza si ujinga: Hivi Diwani Athumani kashuka au kapanda?

Nendeni mkajifunze historia mjue Dr Hassy Kitine na Mzena baada ya kutoka kuwa ma DG wa TISS walipelekwa wapi?

Katibu Mkuu Ikulu sio cheo cha mchezo mchezo Dunia nzima

hadhi ya Balozi ni ndogo kuliko hadhi ya Katibu Mkuu wa Foreign affairs

hadhi ya Katibu Ikulu ni kubwa kuliko Katibu wa Wizara yeyote
Wote hao mzena na kitine ni enzi za zamani kabla usalama haujawa taasisi imara kama miaka hii. Kwa miaka ya karibuni tumeona wakipelekwa nje kwenye balozi.

Hapo ukiangalia vizuri huyu Diwani ataanza kuwa chini ya aliyekuwa msaidizi wake kwenye masuala ya usalama. Sio afya sana kwa taifa.
 
Diwani Athman ameshuka sana. Katibu Mkuu Ikulu ana supervise watumishi wa Ikulu tu. Lakini siyo watumishi wa Ofisi Binafsi ya Ikulu (OBR). Majukumu yake ni madogo kuliko hata Makatibu Wakuu wa Mawizara hususan kasma

Mtu aliyepanda cheo ni Moses Kusiluka ambaye anakuwa Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), huyu ni Mkuu wa Makatibu Wakuu wote.
Ni Mkuu wa Watumishi wa Serikali nchini na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri.
 
Nendeni mkajifunze historia mjue Dr Hassy Kitine na Mzena baada ya kutoka kuwa ma DG wa TISS walipelekwa wapi?

Katibu Mkuu Ikulu sio cheo cha mchezo mchezo Dunia nzima

hadhi ya Balozi ni ndogo kuliko hadhi ya Katibu Mkuu wa Foreign affairs

hadhi ya Katibu Ikulu ni kubwa kuliko Katibu wa Wizara yeyote
Sasa huyu Diwani siyo Katibu Mkuu Kiongozi
 
Chief of staff (katibu wa Ikulu) ni nafasi nyeti sana and very senior kwenye serikali yeyote duniani.

Nchi nyingine hasa zenye unitary constitution kama muundo wa UK (ambao tume-copy) ni mkubwa kushinda katibu mkuu kiongozi ambae ni head of civil services (which includes idara za usalama).

In other words Diwani Athumani hiyo ni promotion.
 
Wala hakuna tatizo lolote jamani , nimeuliza tu maana kutoka kuwa Mkurugenzi wa Tiss hadi kuwa Katibu Mkuu Ikulu , sijajua wapi ni juu .

Je sasa amepandishwa Cheo au Ameshushwa ?

Natanguliza shukrani .
Amepanda maana Diwani Athumani ki hadhi ni sawa tu na mkurugenzi wa idara wizarani...

Now ni katibu mkuu.
 
Hamna diwani sio mtu mbaya na ni mshika dini haswaa na ana rekodi tamu sana kuanzia urpc,ukuu wa mkoa na sehemu nyingine alizopita ila si mara zote unaweza kufaulu sehemu zote,kusema ukweli idara yetu ya usalama wa taifa ilipwaya sana kwenye suala la ujasusi wa kiuchumi hili lipo wazi thus why nkawish siku moja afanyiee replacement tupate bora zaidi yake sio kwamba roho yangu ilijifunga kwa yeye kuwa DG wa TISS....
Hivi kuondoka kwa Diwani ndio TISS itakua Bora ?

Tunataka mabadiliko ya sura ya mtu au mabadiliko ya kitaasisi ?
 
Back
Top Bottom