Kuuliza si ujinga: Hivi Diwani Athumani kashuka au kapanda?

Kuuliza si ujinga: Hivi Diwani Athumani kashuka au kapanda?

Ukicheki wavuti ya KMK , jukumu lake namba tatu ni "Address Operational issues of TISS and PCCB"

Bila shaka masuala yasiyo operational yatakua chini ya mamlaka ya uteuzi

Nadhani utaratibu huo unaatumika pia kwa IGP na KM wao wa Mambo ya Ndani

..kwa mfano, katibu mkuu wizara ya ulinzi ana mamlaka gani kwa Mkuu wa Majeshi, au Mnadhimu Mkuu?
 
Katibu Myeka ndio nasikia leo hilo neno Myeka ila sidhani ndio chief staff. Katibu wa Ikulu ndio mkuu wa shughuli za Ikulu that equates to ‘chief of staff’.

Katibu wa wizara ya mambo ya ndani on paper ni mkubwa kuliko mkuu wa idara ya usalama na katibu mkuu kiongozi ndio boss wao ambae yupo Ikulu.

Chief Staff ndio head ndani ya Ikulu wa watumishi wote kila anachoambiwa raisi na yeye anatakiwa kukijua na ndio mshsuri wake mkuu kwenye maamuzi na nchi nyingi anaingia vikao vya baraza la mawaziri kwa sababu kila anachoshauriwa raisi na yeye lazima akijue.
Kwa maana hiyo KM Ikulu ndio mshauri wa karibu zaidi wa Rais kuliko KMK na DG wa Usalama. Hivyo ana nguvu kwa maana ya mshauri wa karibu zaidi wa Rais.
 
Diwani Athman ameshuka sana. Katibu Mkuu Ikulu ana supervise watumishi wa Ikulu tu. Lakini siyo watumishi wa Ofisi Binafsi ya Ikulu (OBR). Majukumu yake ni madogo kuliko hata Makatibu Wakuu wa Mawizara hususan kasma

Mtu aliyepanda cheo ni Moses Kusiluka ambaye anakuwa Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), huyu ni Mkuu wa Makatibu Wakuu wote.
Elimu yako ulipata wapi aisee, Katibu Mkuu kiongozi ni Mkuu wa utumishi wa umma.
Katibu wa Baraza la Mawaziri.
 
Kwa maana hiyo KM Ikulu ndio mshauri wa karibu zaidi wa Rais kuliko KMK na DG wa Usalama. Hivyo ana nguvu kwa maana ya mshauri wa karibu zaidi wa Rais.
Of course hiyo ndio role yake, kila anachoambiwa raisi na yeye anatakiwa akijue pia, kutoka kwa mshauri wake yeyote.
 
Chief of staff (katibu wa Ikulu) ni nafasi nyeti sana and very senior kwenye serikali yeyote duniani.

Nchi nyingine hasa zenye unitary constitution kama muundo wa UK (ambao tume-copy) ni mkubwa kushinda katibu mkuu kiongozi ambae ni head of civil services (which includes idara za usalama).

In other words Diwani Athumani hiyo ni promotion.
Watakaokuelewa ni wachache sana.

Lakini cha kujiuliza ni kwamba, kama hatufuati katiba tuliyojiwekea wenyewe, tunawezaje kufuata katiba ya wakoloni!!???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maana hiyo KM Ikulu ndio mshauri wa karibu zaidi wa Rais kuliko KMK na DG wa Usalama. Hivyo ana nguvu kwa maana ya mshauri wa karibu zaidi wa Rais.

..Cdf, Igp, Dg Tiss, ndio wasaidizi na washauri Raisi anapotekeleza majukumu ya Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Nendeni mkajifunze historia mjue Dr Hassy Kitine na Mzena baada ya kutoka kuwa ma DG wa TISS walipelekwa wapi?

Katibu Mkuu Ikulu sio cheo cha mchezo mchezo Dunia nzima

hadhi ya Balozi ni ndogo kuliko hadhi ya Katibu Mkuu wa Foreign affairs

hadhi ya Katibu Ikulu ni kubwa kuliko Katibu wa Wizara yeyote
Hawa watu ni wa kuwapuuza tu mhenga mwenzangu. Sasa mtu anashindwa vipi kujua nani mkubwa kati ya MKURUGENZI na KATIBU MKUU, tena Katibu Mkuu Ikulu (Chief of Staff).
 
Watakaokuelewa ni wachache sana.

Lakini cha kujiuliza ni kwamba, kama hatufuati katiba tuliyojiwekea wenyewe, tunawezaje kufuata katiba ya wakoloni!!???

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida inaanza kwenye succession planning ya vyama vya siasa watu wana ascend kwa kusoma tena kidogo mlengo wa chama cha siasa na uelewa wa nafasi za serikali (civil services) bila ya kufahamu sifa zinazotakiwa kupewa hizo nafasi.

Sasa kuna katiba inayompa raisi madaraka ya kuteua kila sehemu hapo ndio vurugu machi ilipo akazimishwi kufuata utashi.

Ila serikalini kwenyewe bado wanamfumo mzuri sana tena sana, kwenye succession planning sema unaishia kwenye nafasi ya ukurugenzi wa wizara. Ukiwasikiliza wakurugenzi karibu wote ni very technical kwenye field zao na wanajua ufanyaji kazi wa wizara zao kinaga ubaga.
 
Chief of staff (katibu wa Ikulu) ni nafasi nyeti sana and very senior kwenye serikali yeyote duniani.

Nchi nyingine hasa zenye unitary constitution kama muundo wa UK (ambao tume-copy) ni mkubwa kushinda katibu mkuu kiongozi ambae ni head of civil services (which includes idara za usalama).

In other words Diwani Athumani hiyo ni promotion.
Tafsiri yako siyo sahihi,katibu wa ikulu cyo chief of staff.labda katibu mkuu kiongozi unaweza mlinganisha na chief of staff wa mataifa makubwa.
 
Kumbe huyu ndie suphian juma Chawa maarufu wa mh.rais kwa Sasa twitter? Coz kule Twitter nako kauliza swali Kama Hilo hilo
Mimi siyo chawa Sufiani , labda kama kakppi swali langu
 
Tafsiri yako siyo sahihi,katibu wa ikulu cyo chief of staff.labda katibu mkuu kiongozi unaweza mlinganisha na chief of staff wa mataifa makubwa.
Katibu mkuu kiongozi anaitwa ‘cabinet secretary’.
 
Sawa wewe mwenye akili, mwenye kudharau wengine kisa mrengo wao wa siasa.
Upumbavu ni haiba ya mtu sio dharau wala tusi. Kama kuna mtu mnene, mfupu, mrefu sas mwingine ni mpumbavu. Au anaweza kuwa mpumbavu mnene au mpumbavu mfupi😃 zinaweza kuwa combined
 
..Cdf, Igp, Dg Tiss, ndio wasaidizi na washauri Raisi anapotekeleza majukumu ya Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Nadhani kuna majukumu wanaripoti moja kwa moja kwa Rais na mengine kwa KM wa Wizara yao husika.

Ndio maana ya hivyo vyombo kuwa chini ya Wizara ambayo mtendaji mkuu ni KM. Masuala ya bajeti, sheria na sera yanaratibiwa na KM. Mengineyo ya kiusalama ndio yanakwenda kwa Waziri na Mhe Rais
 
Demotion kubwa.... umetoka kusimamia idara nyeti yenye influence kubwa ndani na nje ya nchi, na kwenye mustakabli wa nchi, kwenda kusimamia ikulu tu! Tena naona kawekwa karibu ili asifurukute
Tiss ina influence nje ya nchi kumbe?
 
Back
Top Bottom