Kuvaa Hijab ni dini au udhaifu wa wanaume?

Mbele ya wanaume ambao ni halali kukuoa kwahiyo unapo ufunika vizuri unaepusha matamanio kwao hapo ndipo inapelekea Kubakwa au kusumbuliwa
Huwezi kuondoa tamaa kwa kufumika mwili. Huo ni ushenzi tu
 
Lazima tukubaliane kuwa dini zetu na vitabu vyake vyooooote ni kazi ya wanaume pekee
Mwanaume ndio mwenye Dunia yake na mwanamke alitoka ubavuni mwa mwanaume kwa hiyo lazima apangiwe masharti jinsi ya kuishi katika utawala wa mwanaume asiishi jinsi anavyotaka yeye
 
Huna hata akili yaani we akili zako binadamu na ng'ombe watembee uchi sawa ,sasa wewe mbona unavaa nguo?
Navaa nguo ndio lakini sisemi kuwa ni amri kutoka kwa Mungu kuwa nivae nguo. Navaa nguo kwakuwa nimewakuta watu wanavaa ngua, wamegundua wenyewe kutengeneza nguo, ni makubaliano yao. shida iko pale mtu atakapouliwa kwakuwa hakuvaa nicab.
 
Navaa nguo ndio lakini sisemi kuwa ni amri kutoka kwa Mungu kuwa nivae nguo. Navaa nguo kwakuwa nimewakuta watu wanavaa ngua, wamegundua wenyewe kutengeneza nguo, ni makubaliano yao. shida iko pale mtu atakapouliwa kwakuwa hakuvaa nicab.
😂😂😂Izo ni Sheria fulani usiwe obsessed na Iman za watu wala tamaduni hata wamasani wanashinda na mashika town kimpango wao hata wakae materko wazi hamna tatizo
 
Uzi pumba
 
Dini ya Uislaam inataka mwanamke afiche nywele zake hiyo ni Amri na sababu zilizotolewa ni kwamba mwili wa mwanamke ni karubia wote ni Uchi kwamba anatamanisha kwa hiyo anatakiwa auhifadhi.

Ahahah kwahy mwili wa mwanaume hautamamishi
 
Hapana hapana hapana, vitu vyote muhimu vya MwenyeziMungu hajaviacha huru ili wewe ujichagulie ufanye au uache, vitu vyote kutoka kwa Mungu ni lazima ufanye la sivyo utakufa hapohapo au utasambaratika. Kwakuwa Mungu amekuumba yeye anajuwa ni lipi unaweza na lipi unashindwa kama vile wewe usivyoweza kupakia container kwenye bajaj. Mungu anataka wewe upumue hivyo ni lazima upumue la sivyo utakufa, anataka ule chakula, utoe haja kubwa na ndogo, ulale usingizi, uzae, uchukie, ucheke, ukohoe, nk huwezi kujichagulia neno la Mungu. Kama hijab ingekuwa ni kwaajili ya mungu mtu angekufa hapohapo akiivua au akiikosa. Hijab isisababishe watu kuuana, ndoa kuvunjika, watu kudharauliana nk kwakuwa hijab sio dini, it is something nice to have, sio lazima wala muhimu/.
 
Kutambua kuwa tupo uchi kulianzia Eden baada ya Adam na Eva kwenda agaist na katazo la Mungu kuwa wasile mti wa kutambua mema na mabaya but b4 hapo Adam na Hawa wote walikuwa uchi tu na hakukua na shida yyte....
 
Umeandika ujinga tena usio kuwa na shaka ndani yake

Kwamba binadamu azaliwe na hijab?🤣
 
Sikiliza wewe na usiwe kama umekumbwa na uhayawani, kila mahali kuna taratibu zake kwa mujibu wa imani zilizopo huko. Hawajawahi kuingilia huo wako unaoishi nao, basi heshimu ya wengine.

Iran nzima inajulikana inaongozwa kwa sheria za kiislamu kali tena chini ya dhehebu la shia, mavazi na taratibu zingine zinafuatwa maana ni sheria ya nchi. Hii hata ukienda mgeni unatakiwa uitimize sawasawa, kwani wao wakija huku ulipo wewe wanakutana na sheria zake na wanazifuata.

Chuki ya dini kubwa mnaileta nyinyi, waislamu hawana habari na nyinyi na wala hawagusii kuhusu sheria za kwenu. Ndiyo kama hao Iran wanafanya yao, cha ajabu wewe upo mbali nao unaanza kusambaza maneno ys chuki.

Waislamu wanafundishwa kuheshimu imani za wengine na hata enzi za Mtume mwenyewe alishaishi na wakristo na wayahudi na hakuwahi kuingilia imani zao. Huku kuwachokonoa na kuleta chuki zako, wakija kujibu au kufanya jambo kwa kuchukizwa useme ni wabaya.

Wewe shika dini yako achana na za watu, kama kuna makosa yanatokea kwao hata kwako yanatokea pia. Kabla ya kumnyooshea mtu kidole, hakikisha mkono wako ni msafi.
 
Umeandika ujinga tena usio kuwa na shaka ndani yake

Kwamba binadamu azaliwe na hijab?🤣
Kama haiwezekani kuzaliwa nayo basi ni dhahiri kuwa kuvaa hijab sio mpango wa Mungu na sio maagizo Mungu kwa binadamu, maana Mungu hana asichokiweza. Inawezekana kabisa Mungu wako na Mungu wangu wana sifa tofauti kabisa. Maagizo ya Mungu ni kila kila mtu kuamini kuwa Mungu yupo na kila kitu kinatoka kwake, na pili kila mtu amshukuru Mungu kwa kila jambo. Shukuru hivyo ulivyo na unachokipata bure (hewa, chakula, kutoa uchafu, nk
 
Nadhani mimi nawewe tunaongea kitu kimoja. Anayetaka kuvaa hijab avae, asiyetaka asivae.
Kumlazimisha mtu asiyetaka kuvaa hijab, aivae. Hilo ni kosa ambalo tunalifanya sisi binadamu.

Kuhusu mifano yako, sijui ni wapi tunabishana au kupingana ndugu yangu.

Kwa uchache Mungu ameumba binadamu na kumpangia utaratibu wa kula, kupumua, n.k lakini amemuachia chaguo yeye (binadamu) aamue nini afanye, nini asifanye with an associated consequence.

Binadamu akiamua kula na kupumua, consequence yake anaishi.

Binadamu akiamua kukataa kupumua (akajiziba pumzi) na akaamua kukataa kula, consequence yake atakufa.

Chaguo ni la binadamu, Mungu hakulazimishi ule au usile, hilo ni chaguo lako kulingana na utashi wako.
Yeye ameweka tu utaratibu ila suala la kuufuata au kutokuufuata ni juu yako.

Katika hatua nyingine, Mungu ameweka utaratibu wa kumuabudu.
Ukichagua kumuabudu, kuna consequences za kufanya hivyo. Ukichagua kutokumuabudu kuna consequences zake pia. Unachagua wewe mwenyewe "uzike au usafirishe".

Mambo ya hijab ni dini au sio dini, mambo hijab zimeumbwa na nani, hayo tuyaache maana sio sehemu ya wasilisho langu na wala sioni umuhimu wa kuyajadili hapa.
 
Hijab inatengenezwa na wanadamu kwa mikono yao na sababu zao, lakini uhai wa yule binti aliyeuliwa unatoka kwa Mungu, wangemwacha Mungu amuadhibu mwenyewe kama kweli hijab ni kwaajili yake Mungu. Yaani mtoto avae hijab ili wewe utupu wako usimdisie, la sivyo utamuua asipoivaa. Yaani mtoto akusaidie wewe kwenda peponi kwa yeye kuficha nywele zake vinginevyo itatenda dhambi. Umekuwa beberu?
 
ewaaa! hapo tuko pamoja, sema tu mambo yote yanayotoka kwa Mungu yamefungiwa alarm (kengele) na Mungu mwenyewe kukumbusha ulifanye. kama ukiona jambo halina alarm ujue hilo halitoki kwa Mungu, ni lako mwenyewe na mkeo. Mfano, chakula kikiisha mwilini utajisikia njaa, maji yakipungua mwilini utajisikia kiu, ukichoka utajisikia usingizi, uchafu ukitaka kutoka mwilini alarm italia uende msalani. Pia kama muda na siku ya kuabudu ukifika wewe utajisikia hamu na deni la kwenda kuabudu na hata usingizi utakatika, ukiwa mgonjwa kuna kengele itapigwa kukujulisha. Hijab ni jambo lako mwenyewe tu halina kengele wa kiu, kwanini mtoto afe kwa hilo? Na mambo yaMungu ni rahisi sana kuyatambua kwa kutumia hizo alarms lakini pia huwa linawahusu viumbe vyooote vilivyoumbwa na Mungu, kama hujui Mungu anataka nini angalia basi viumbe wengine wanafanya nini na hawafanyi nini.
 
Kwa kweli mambo ya imani yana changamoto siyo mchezo.
1.Kwa hiyo mtu asipofunga mlango na mwizi akaiba hatahesabiwa kama mwizi kwa sababu aliona mali ndani akatamani na hivyo kosa ni la mwenye nyumba/chumba ambaye hakufunga mlango na siyo la mwizi?
2. Kwa nini wanaume wawalazimishe wanawake kusitiri tamaa zao? Yaani mwanamke hastiri kwa sababu yake mwenyewe bali ili mwanaume asitamani. Kwa mfano huo kwenye namba 1 hapo mwenye nyumba ahakikishe anafunga milango ili mwizi asishawishike kuiba na hata akiiba hatakuwa na hatia?
3. Hivi kati ya ambaye anatamani(mkosaji) na ambaye hakufunga mlango nani mkosaji?
4. Kama unaona ukipita jirani na baa utalazimika kunywa pombe basi pita mtaa mwingine na siyo kukazimisha mwenye baa abomoe baa yake ili usitamani pombe.
 
Ukiona mtu anacho kitu kinachoibiwa na wengine ujue mtu huyo ni mkosaji mbele ya Mungu. Mungu hataki mtu mwenye mali, hapendi mtu anaelaza ziada wakati kuna watu wasiokuwa na chakutumia leo. Hiyo pesa ya kununulia baiskeli kuna mtu aliihitaji kwaajili ya kununulia chakula leo. Kwa kawaida Mungu anataka watu wote wafanane ki mali na kila kitu ili kesho watu wote watoke wakatafute. Tajiri (mwenye kitu cha kuibiwa) ni chukizo kwa mungu, hatauona ufalme wa mbiguni, kifupi tajiri haendi peponi kwakuwa amekufuru. Hata Yesu ilikuwa vigumu adui kumfahamu kwakuwa alikuwa amefanana kimavazi na watu wengine, ndio maana yule jamaa alimtambulisha kwa adui kwa njia ya kumbusu. Leo hii weeee, watumishi wanaonekana hata kwa mbali kabisa kwa afya, mavazi na utajiri wao.

Kama wewe hapo mtaani kwako hufanani na wanamtaa wenzio, unaibiwa, una mageti makubwa, una walinzi, una mambwa ujue wewe huna msaada kwenye hiyo jamii, una hofu ya kuibiwa usijihangaishe kabisa na mambo ya Mungu, ni chukizo
 
Nadhani jambo la kumtamani mwanamke kisa kuona nywele napinga,maana wazee wetu wa zamani walikuwa hawavai na kujificha ficha na mambo yalikuwa mazuri tu.

Minadhani jambo la kuvaa ni la kijamii zaidi ukikua unaona hata matiti kama kwenye nchi ya eswatin uwezi ona cha ajabu.
ukikua kwenye jamii watu wana vaa ijabu muda wote ukiona hata unywele lazima ushituke maana iyo hali mnakuwa mmejitengenezea wenyewe na jamii yenu.

Kwa mfano ukiona ziwa la mwanamke anae nyonyesha wala ushituki ila mwanamke asie nyonyesha linakupa msisimko.


Kwangu naona haya mambo ni jamii tu na jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…