Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Wewe unatakaje kwa mfano? Unatamani kuwa mwanaume?
 
Una mawazo ya hovyo sana ya uharibifu, mke wako, watoto wako wa kike na wakwe zako wana hasara sana.
 
Kwa nini wanawake wakafe katika vita vilivyoanzishwa kwa ujinga wa wanaume wenye kushindanisha ego zao na kutunishiana misuli?? Hata wanaume wenye akili huwa wanajitahidi sana kuepusha, kuepuka au kuepukwa na vita.
 
Kweli aisee. Hii nimeshuhudia Babu alikuwa na wake wanne na mke wa tatu alimkuta na watoto wawili akaja nao kukaa Kwa babu na wale watoto walimheshimu Babu kama baba yao mpaka Leo japo ni marehemu
Marehemu ni nani sasa, hao watoto, au babu au baba yao?
 
Hakuna kitu wanaume wanaogopa kama kushindwa na mwanamke katika maisha,kazi,pesa,elimu na kila kitu

No wonder kuna wanaume wanaamuq kuoa golikipa bora maisha yampige lakini awe na mnyonge wake nyumbani

Inferiority complex yasumbua wanaum
Wanaogopa 'ulevi' unaotokana na hayo uliyoyataja.
 
Wewe ukiwa mwanaume utakubali kwenda kupigana katika vita vilivyoanzishwa na wanawake?
Hata kama haukubali, huo ndio ukweli
Vita vikubwa vyote vya dunia vimeanzishwa na wanaume, genocides zote zimeanzishwa na kutekelezwa na wanaume, ni ujinga kudai wanawake wafe kwa sababu ya ujinga usiowahusu. Kama mnataka na wawo washiriki kikamilifu vitani na katika mauaji ya kimbari wapewe fursa kikamilifu za kuanzisha vita, mizozo ya kisiasa na mauaji ya kimbari.
 
Kwa jinsi ulivyo shusha mada yako kwa manung'uniko mkuu, naona unajilaumu kuwa Mwanamke!
Hapana, fikiria nje ya box na uwe na fikira pana, kuelewa hali ya kundi fulani la watu sio lazima uwe mmojawapo wa kundi hilo.
 
Huenda hapa ndipo tatizo kubwa zaidi lilipo. Inabidi wanawake kwenye ndoa wajitihadi sana ku-offer zaidi ya sex na kutunza watoto.
Vipi lakini ukiolewa ukiwa kama sio kilema unachangia mchango mzuri kuboresha hali ya familia??
Kabisa mkuu.
Kuacha mtu mmoja apambane peke yake(maisha yote😭) binafsi naona sio sawa.

ILA hata kama sio kilema na unasaidia ukishakubali tu kuolewa maana yake ni kuwa chini ya huyo aliyekuoa na ndio hapo vitu kama kuomba ruhusa ndio utoke vinakua sehemu ya maisha yako.Ukiona hiyo ni shida usiolewe sbb kwenye ndoa lazima mwanaume awe juu mwanamke chini.Ikiwa tofauti hamfiki!
 
Hajaja, mmekutana, na wakati mwingine hata ni wewe umemfuata yeye.
Akakubaliana na masharti yangu siyo? Kuepuka kuwa chini ya usimamizi wa mtu mwingine ni kutoingia kwenye mahusiano ama ndoa hapo utapuyanga hata ukeshe klabu hakuna wa kukuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…