Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Kuwa mwanamke wa kisasa Tanzania ni changamoto sana katika mahusiano/ndoa

Hao watoto wao single mother wengine sasa hivi ndio wanatukana single mothers!
Mtu kuzaliwa na single mother hakumfanyi aukubali single mother au kuusapoti.
Matokeo ya usingo mother ni kutokana na neuritis za wanawake wa kutosikiliza.
 
Sijaelewa point yako, sioni mantiki ya hii hoja yako, yani kwa sababu ulimualika mtu akachangia na akaja kwenye harusi yako lazima pia ukimualika katika mgogoro wako wa kudaiwa kuvamia kiwanja cha mtu aje pia??
Uko too irrelevant na umeonesha kutoelewa nilichoandika.

Kwa ufupi tu

Umesema "wanawake wanapaswa kugomea kwenda vitani kwasababu walioanzisha vita ni wanaume"

Hii ni hoja unayoonesha udhaifu wa wanawake katika ngazi za juu za maamuzi ya mwisho.

Umeonesha kwamba hawapaswi kupewa dhamana ya kuwa top leaders kwasababu ya uoga wao na jinsi walivyo incompetence kwenye battle field.

Hiyo ni hoja ambayo unaonesha kuwa wanayopaswa wanawake kufanya ni yale tu ambayo yamesababishwa na wanawake wenzao.

So basically unakuwa umekubali kuwa fursa zote ambazo zimeletwa na hao viongozi wanaume hazipaswi kushobokewa na wanawake.

Uhalali anaoweza kuupata mwanamke kwa kunufaika na uongozi wa wanaume basi ndio uhalali huo huo unaomtaka naye ajitokeze mstari wa mbele kupigania nchi yake.
 
Ukiwa Feminists ni shida,

Single mother ni shida,

Ukiomba pesa malalamiko

Ukimzidi mwanaume wako kipato kama yeye sio marioo tatizo.

Ukimzidi mwanaume elimu ni tatizo

Ukivaa nguo za kubana sio wife material

Ukitoka nyumbani unatakiwa kuomba ruhusa.

Ukichelewa kurudi nyumbani tatizo.
Natafuta Ajira njoo huku
 
Mtu uliyezaliwa na mwanamke unapata ujasiri wapi wa kuwaita "creatures"? Na kwa nini unataka kumcontrol binadamu mwenzako?

Wanawake ni watu wa kuwaheshimu na kuwaenzi kutokana na nafasi yao ya kipekee ya kutuzaa na kutulea wakati hatuna uwezo wowote wa kujifanyia lolote.

Na mara nyingi tukipita huu umri wa kujimwambafy, hao hao wanawake ndio wanatulea mpaka tunapoondoka katika hii dunia. Kuwatukana ni upumbavu wa hali ya juu.

Amandla...
Hoja yako haina mantiki ni kama useme yule mwanamke ni sister wa kanisa la Roman hivyo hana dhambi,basi usimhoji kama anazo
 
Maadili ya karne ya saba sio maadili ya leo, pia maadili yanaendena na level ya sayansi na teknolojia. Mkiwa katika level ndogo ya sayansi na teknolojia maadili yenu yanakuwa ya kijima zaidi na kandamizi kwa wanawake.
Utakuwa hujui maana ya maadili. Wizi ni mzuri au mbaya ? Uzinzi ni uzuri au mbaya ? Kutembea uchi ni kizuri au kubaya ? Sasa haya yote hayapitwi na wakati mzee, hata teknolojia iwe itakavyo kuwa yatabaki kuwa mabaya.

Yaani Kuna vitu haviathiriwi na wakati.
 
Wewe ukiwa mwanaume utakubali kwenda kupigana katika vita vilivyoanzishwa na wanawake?
Hata kama haukubali, huo ndio ukweli
Vita vikubwa vyote vya dunia vimeanzishwa na wanaume, genocides zote zimeanzishwa na kutekelezwa na wanaume, ni ujinga kudai wanawake wafe kwa sababu ya ujinga usiowahusu. Kama mnataka na wawo washiriki kikamilifu vitani na katika mauaji ya kimbari wapewe fursa kikamilifu za kuanzisha vita, mizozo ya kisiasa na mauaji ya kimbari.
Kwahiyo sasa hivi rais Samia akiingia kwenye mgogoro binafisi na kagame na akaamuru jeshi la Tz liivamie Rwanda wanajeshi wa kiume watagoma kwenda vitani badala yake watakusanywa wanawake ndo waende vitani kisa mgogoro umeanzishwa na wanawake wenzie?

Hapa duniani mamilion ya wanaume wamekufa wakipigania uhuru wa mataifa yao je huo uhuru wanawake hawafaidiki nao?

Uingereza chini ya malikia Elizabeth imeanzisha mgogoro mingapi hapa duniani ?
Kama nafasi ya kuzua mgogoro wamesha pewa na kuzua hiyo migogoro.
Hao wanawake wa kisasa unao wasema wamekuwa tatizo kubwa ndani ya jamii.
 
Maadili ya karne ya saba sio maadili ya leo, pia maadili yanaendena na level ya sayansi na teknolojia. Mkiwa katika level ndogo ya sayansi na teknolojia maadili yenu yanakuwa ya kijima zaidi na kandamizi kwa wanawake.
Kwahiyo hiyo teknolojia ndo imekuja kuwarazimisha kuwa wazinzi,walevi,matapeli wa mapenzi sio?
 
Labda kama mnaongelea wanawake wa Dar au maisha ya mahusiano ya Dar - tena Dar Kinondoni, Ilala sehemu ndogo na Ubungo sehemu ndogo.
Nje ya hapo, watu wanaoa masingle mothers, wanawake walioachika - wanaolewa wanazaa tena kama kawaida - huo unyanyapaliwaji upo tu humu kwenye keyboards kiuhalisia watu wanaona hatari na kuzalishana.

Pia hao wanawake wenye sifa ulizitaja hapo juu wako wachache sana labda kama mnaongelea hawa superstars fake wa mitandaoni na wanamuziki.
Mtaani huku bado mfume dume UMETAMALAKI...mwanaume ndo mtafutaji namba moja,haijalishi kama mama anafanyakazi ama la.
Hao FEMINISTS mnaosema labda hawa wanaotumia majina fake onlibe but kwenye real life feminists ni wachache sana.
 
Hakuna kitu wanaume wanaogopa kama kushindwa na mwanamke katika maisha,kazi,pesa,elimu na kila kitu

No wonder kuna wanaume wanaamuq kuoa golikipa bora maisha yampige lakini awe na mnyonge wake nyumbani

Inferiority complex yasumbua wanaume
Wa hivi wengi hawana mbele wala nyuma 🤣🤣 wanatafuta watu wanyonge ili wapate ahueni kihisia.
 
Labda kama mnaongelea wanawake wa Dar au maisha ya mahusiano ya Dar - tena Dar Kinondoni, Ilala sehemu ndogo na Ubungo sehemu ndogo.
Nje ya hapo, watu wanaoa masingle mothers, wanawake walioachika - wanaolewa wanazaa tena kama kawaida - huo unyanyapaliwaji upo tu humu kwenye keyboards kiuhalisia watu wanaona hatari na kuzalishana.

Pia hao wanawake wenye sifa ulizitaja hapo juu wako wachache sana labda kama mnaongelea hawa superstars fake wa mitandaoni na wanamuziki.
Mtaani huku bado mfume dume UMETAMALAKI...mwanaume ndo mtafutaji namba moja,haijalishi kama mama anafanyakazi ama la.
Hao FEMINISTS mnaosema labda hawa wanaotumia majina fake onlibe but kwenye real life feminists ni wachache sana.
Mambo mengi yanayoandikwa na wengi humu huwa ni ya kusadikika na toxic. Single mom wanaolewa na wanajenga ndoa na familia zinanawiri.
 
Utakuwa hujui maana ya maadili. Wizi ni mzuri au mbaya ? Uzinzi ni uzuri au mbaya ? Kutembea uchi ni kizuri au kubaya ? Sasa haya yote hayapitwi na wakati mzee, hata teknolojia iwe itakavyo kuwa yatabaki kuwa mabaya.

Yaani Kuna vitu haviathiriwi na wakati.
Wizi ni kosa la jinai wala sio suala la maadili ya jamii fulani.

Uzinzi ni nini?

Sijawahi kuona mtu mwenye akili timamu anatembea uchi duniani labda wakati fulani wanawake walikuwa wanaandamana vifua wazi kupeleka ujumbe.
 
Tatizo unakuta mtu maisha yake ya kuungaunga halafu anaoa mke
Ni kama amejitafutia mtumwa
Hapo atataka maji moto ya kuoga apelekewe
Ataacha hela mbuzi bado anataka akirudi akute wali nyama
Hana hela hta ya dobi, anataka kumrundia mke wake minguo ya grisi afue
Ni ushenzi mtupu maisha ya kimasikini
Kuna ukweli mkubwa katika hili.
Umasikini pia unachangia sana katika haya mambo.
 
Tabu ndio hii sasa inayotokana na kufata hayo mabadiliko. Lazima akili itumike sio kila mabadiliko yanafatwa, kuna vitu vimeshatangulia muda, yaani havipitwi na wakati hasa maadili . Ndio maana ukienda kinyume na maadili lazima uharibikiwe.

Mwanamke wa kisasa amefanywa mjinga na kutumia kama chombo cha starehe, imefikia hata yale yanayo mdhuru anaona ndio sawa ila yale yenye kumpa hadhi na heshima anayapiga vita, unajiuliza akili zao wanazitumia kwenye nini ?

Siku zote mwanamke anahitaji uangalizi wa mwanaume na usimamizi awe atakavyo kuwa.
Kaeo kweli. Ndio hivyo mkubaliane na hali. Maadili yanabadilika kulingana na mazingira na utandawazi.
 
Back
Top Bottom