Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi ni kazi sana

Tafuteni hotel yenye garden hapo mtapata garden bure na watawafanyia arrangement ya viti na meza mtalipia chakula na vinywaji hela inayobaki mtamlipa mpiga picha watapata kumbukumbu ya picha. Wale wakalale kama haelewi alete hela.

Au nendeni Cozy Cafe wenyewe unalipia chakula na vinywaji, mapambo na eneo bure. Hiyo hela inatosha
 
Alikeni watu wachache, fanyeni kaparty kadogo kimtindo sio mpaka umati wa watu.
Wasisahau kubeba JBL speakers na bundle ya kutosha kwenye simu wapige muziki direct toka Youtube
 
Attachments

  • images (93).jpeg
    images (93).jpeg
    19.6 KB · Views: 4
[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana yaani mwenye harusi katoa laki 5 tu kati ya 5M ...aisee bwana harusi katisha[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tafuteni hotel yenye garden hapo mtapata garden bure na watawafanyia arrangement ya viti na meza mtalipia chakula na vinywaji hela inayobaki mtamlipa mpiga picha watapata kumbukumbu ya picha. Wale wakalale kama haelewi alete hela.

Au nendeni Cozy Cafe wenyewe unalipia chakula na vinywaji, mapambo na eneo bure. Hiyo hela inatosha

Yes hata Cozy cafe patawafaa sana, kama wapo Daslam, pako vizuri.
Adjustments.jpg
 
Hii nimeipenda sana
harusi ni jambo la kifamilia mimi sitaki kabisa mambo yakuwekana mbele kama padri anaongoza ibada. Kuna rafiki yangu alifunga ndoa mwezi uliopita, aliweka milioni 5 hakuna mchango wa mtu. Tulitoa order hotel moja matata waandae chakula chenye thamani ya sh 20,000 kwa kila mtu, vinywaji tulipiga bajeti ya bia 10 kwa kila mtu yani 25,000 (kumbuka wengine hawanywi pombe gharama inashuka) jumla max 45,000 kwa kila mtu. Waalikwa 30 upande wa bibi na 30 baba.. 45,000*60=2,700,000 iliyobaki ilitumika kwenye mavazi na vitu vingine vidogo vidogo. Sehemu ya shughuli hotel waliandaa kwa gharama zao cause ni order kubwa.. watu walikula wakasaza, wakatambaa tulikesha mpaka majogoo..
 
Pledges za michango yote ni milioni 18, harusi ni mwezi huu wa tatu mwishoni, hadi muda huu watu wachache wametoa, cash iliyopo ni milioni moja kasoro. Bwana Harusi kachanganyikiwa kaniachia mipango yote nipange mimi, nafanyaje?

Bwana Harusi aliahidi kutoa milioni tano lakini katoa laki tano tu, nyingine hajatoa, anamtaka MC Garab wakati uwezo hana, yaani ni kama ndugu wamemsusia, simu hawapokei, nimemshauri asifanye sherehe ni kama haelewi, sijui itakuwaje.
Kama uenyekiti wa harusi ni Kazi wa Chama cha siasa utakuwaje?
 
Pledges za michango yote ni milioni 18, harusi ni mwezi huu wa tatu mwishoni, hadi muda huu watu wachache wametoa, cash iliyopo ni milioni moja kasoro. Bwana Harusi kachanganyikiwa kaniachia mipango yote nipange mimi, nafanyaje?

Bwana Harusi aliahidi kutoa milioni tano lakini katoa laki tano tu, nyingine hajatoa, anamtaka MC Garab wakati uwezo hana, yaani ni kama ndugu wamemsusia, simu hawapokei, nimemshauri asifanye sherehe ni kama haelewi, sijui itakuwaje.
Uenyekiti wa harusi ni kazi ngumu na ya kijinga. Fanya kazi zako... Hiyo wala sio kazi..

Mwambie kama anataka hayo makubwa unamtakia kila la kheri na umkabidhi mafungu na daftari la pledge...

Tunaacha kukaa chini kuchakata mawazo ya kibiashara na kuhangaikia financing ..tumekalia sare na ukumbi.. so sad.

Inabidi siku moja mchana tukiwa barabarani ishuke mvua kubwa ya vitu vizito ipige vichwa vyetu hivi mpaka akili ijiseti vizuri.
 
Wewe umezaliwa bongo ama? Mbona unajifanya hutujui sisi wabongo? Kwa nini michango tuchange mapema kiasi hicho? Nmataka hela yetu kuizungusha kwenye biashara zenu?Tutachanga siku 3 kabla.
Wabongo tuko tiyari changia harusi ila sio mgonjwa aliyepo hospital.😂😂
 
Tafuta mkeka, unga wa ngano kilo 15, mchele kilo 50 na nyama kilo 25 alafu vunga anza kutembea na chupa ya maji kubwa akikuuliza kila kitu kipo sawa? Kohoa kdogo fungua maji kunywa funda moja alaf muonyeshe ishara ya kutulia kwa mkono
Jibu bora zaidi kwa mwaka 2021. Litumike pia kwenye kamati zingine za harusi pale mambo yanapokwenda mrama. Nimecheka mno mkuu.
 
Pledges za michango yote ni milioni 18, harusi ni mwezi huu wa tatu mwishoni, hadi muda huu watu wachache wametoa, cash iliyopo ni milioni moja kasoro. Bwana Harusi kachanganyikiwa kaniachia mipango yote nipange mimi, nafanyaje?

Bwana Harusi aliahidi kutoa milioni tano lakini katoa laki tano tu, nyingine hajatoa, anamtaka MC Garab wakati uwezo hana, yaani ni kama ndugu wamemsusia, simu hawapokei, nimemshauri asifanye sherehe ni kama haelewi, sijui itakuwaje.
Mkabidhi kilichopo basi apange yeye wewe uwe mgeni mwalikwa
 
Mwambie amalize yeye kwanza ndiyo upate nguvu ya kutafuta wengine,maana swali litakuka bwana harusi latoa ngapi?
Halafu wanataka wapate zawadi ya 1/8 yaapato,bado walazwe,wakodiwe gari nk
 
Hivi kwani huwezi kufanya harusi pekee yenu bila michango?

Nauliza tu
Eti,mnaipiga pale church mkimaliza buku 50 za pastor then hao group mtu sita tu mnapiga bonge la dinner kituo chochote mnarudi home mbonji hiyo kilo 5 chenchi inabaki.
Harusi yangu nilipika mwenyewe chakula watu 100,watu walikula,kunywa mpk kusaza na kudance usiku wote.
Sikumchangisha mtu senti 10,walileta vizawadi tu.
 
harusi ni jambo la kifamilia mimi sitaki kabisa mambo yakuwekana mbele kama padri anaongoza ibada. Kuna rafiki yangu alifunga ndoa mwezi uliopita, aliweka milioni 5 hakuna mchango wa mtu. Tulitoa order hotel moja matata waandae chakula chenye thamani ya sh 20,000 kwa kila mtu, vinywaji tulipiga bajeti ya bia 10 kwa kila mtu yani 25,000 (kumbuka wengine hawanywi pombe gharama inashuka) jumla max 45,000 kwa kila mtu. Waalikwa 30 upande wa bibi na 30 baba.. 45,000*60=2,700,000 iliyobaki ilitumika kwenye mavazi na vitu vingine vidogo vidogo. Sehemu ya shughuli hotel waliandaa kwa gharama zao cause ni order kubwa.. watu walikula wakasaza, wakatambaa tulikesha mpaka majogoo..
Hii nimeipenda lazima niige
 
Back
Top Bottom