Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Ahahaha
 
Kuna jamaa alidai tutakimbilia kwa wazalendo wenzetu WaChina tuliowanyima bandari ya Bagamoyo kwani wao wana mapesa mengi mpaka ya kuwakopesha waMarekani. Sijui alikuwa nani yule utopolo?
 
Yeah....hata jina lenyewe mie naona linatutukanisha tu........kama 'wao' ni mabeberu (mbuzi dume), ina maana 'sisi' ni "mbuzi jike"? Haaaaa......
 
Baada ya kichapo cha mbwa mtu kwenye box la kura naona unaibuka na nyuzi za kitoto. Unajua nini maana ya Beberu? Unadhani kila mfadhili ni Beberu. Unafahamu dhana nzima ya Imperialism? Tumia akili zako unapofanya ukosoaji wa kiuchambuzi.
Ule nao unauita uchaguzi?
 
Tatizo ccm mumejusahau na kulifanya Taifa la Tanzania kama kichwa cha mwendawazimu. Kila mwenyekiti wenu mpya anakuja kujifunzia kunyoa hapo toka uhuru. Sijui kama hata wewe mwenyewe unaelewa ulichokiandika.

Wapi nimesema maendeleo yatakuja kwa ufadhili? Toka uhuru hadi kufikia 2015 ndiyo mumefahamu?
 
Well said.
 
Umetaja mataifa ambayo yalikuwa masikini kama sisi wakati wa uhuru, lakini sasa wako juu. Halafu tatizo ni beberu
 
Kama kungekuwa na "going back to future" ya ukweli, sidhani kama ungeiwaita mabeberu, nadhani ungewaita mashetani, wabakaji, wauaji, wezi, waporaji, na kama sikosei matusi makubwa zaidi kuliko hayo...
Hao jamaa unaodai wameendelea siyo watu wazuri kabisa, ni binadamu wenzetu sawa ila wana tabia za kikatili mno, sana sana..
Jaribu kusoma history kidogo ujuwe siri za utajiri na maendelea yao labda ukirudi tuweze kuongea kivingine...
 
BEBERU sio matusi mzee ......kwa kiingrerza tunawaita imperialist....


Kumuita mtu Beberu inafanana (an analogy) na kumuita mtu mwizi, kama ni mwizi na ushahidi unao basi kumwita mwizi sio tusi lakini kama huna ushahidi basi kumwita hivyo ni tusi. Mtu anakuwa beberu pale ambapo anafanya ubeberu vinginevyo beberu, kwa tafsiri ya nchi zinazofuata misingi ya kijamaa, ni tusi.
 
China imeendelea sana
Ilipewa misaada?
Badilisha mtazamo
Umatonya ni fikra mgando

yan unaongelea nchi ya pili kwa utajiri duniani unafananisha na nchi iloyopo kwenye nchi kumi za mwisho kwa umaskin duniani mkuu upo sawa upstairs ??

Nan alokwambia china haijawah kupewa msaada ??
 
Usengelema mkubwa kuliko wote kila likitajwa hilo neno "BEBERU" ndugu zetu wa CCM wanahusisha na jambo baya, ila hao hao kina kabudi wakiwa wanapikea misaada wanawaita WAHISANI , sasa swali langu kwanini wakati wanapokea misaada wasiseme "MABEBERU" wameleta hela hizi na hizi, SOMETHING SOMEWHERE IS NOT OKAY, ila kuna mbwa kutoka ccm itakuja kutetea huo upuuz.
 
Ninyi watu mnakaririshwa haya mambo au mnafuatilia historia sahihi?
Kuna raisi wa Tanzania ambaye amemzidi Nyerere kwa kupata misaada toka magharibi na mashariki mwa dunia?

Hakuna hata aliyefikia nusu yake...
Nyerere alikuwa mtu wa diplomasia hasa, juu ya yote alikuwa na kiburi na jeuri ya kukataa misaada yenye mashariti ya kijinga.
 
Nilidhani kila mtu hapa anajua kilichopo nyuma ya kuitana majina mabaya!

Ad hominem fallacy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…