Hata wanaotoa kauli hizo, wanajua wanazitoa kisiasa.
Njia rahisi ya kumtawala Muafrika ni kumtengenezea adui wa pamoja, yani hawa wakoloni weusi wa leo kina Magufuli wanaotutawala kwa kuiba kura wakishindwa kutatua matatizo ya wananchi, kimbilio lao ni kuzusha vita dhidi ya "mabeberu".
Hapo wanawachota wananchi.
Na utakuta watu masikini kabisa wanaokandamizwa na hii serikali, na wao wanaitetea, kwa sababu tu wamelishwa ujinga wa "kupigana dhidi ya mabeberu".
Kusema ukweli ubeberu kwa kiasi fulani upo. Dunia ina geopolitics, ina espionage, ina national interests. Kwa hiyo, dhana ya "mabeberu" si kweli kwamba ni ya uongo kabisa.
Ila, wanasiasa wanajua kuitumia kwa manufaa yao, si kwa manufaa ya taifa.
Wanajua kuutumia ukweli fulani mdogo (a kernel of truth) na kuukuza vibaya kwa manufaa yao ya kisiasa.
Maanay yake nini?
Chukulia Wamarekani kwa mfano. Nchi yenyewe imegawanyika. Kuna Democrats na Republicans.Kuna Conservatives na Liberals. Kuna watu wa mijini na wa vijijini. Hawa si wamoja, wenyewe wanapingana.
Kwa kuangalia "popular vote", mshindi, Joe Biden, mpaka sasa, hajafikisha hata 51% ya kura zote. Yuko kwenye 50.8%. Wakati Trump yuko 47.3%.
Katika serikali ya Trump, kuna watu wamejiuzulu kazi serikalini kwa kupingana na muelekeo wa serikali ya Trump.
Rais George W. Bush, a conservative and Republican, ndiye rais aliyeisaidia Africa kuliko marais wote, kuliko hata Obama. Hususan kwenye mambo ya kupigana na magonjwa kama Malaria na AIDS.
Sasa watu hawa very complex. Tuukiwashutumu, basi na shutuma zetu ziwe complex.
Siyo mtu unaiba kura, Wamarekani wakikusema umeiba kura, unajitetea kwa kuwaita mabeberu.
Wakati hata wananchi wako wengi tu wanalalamika umeiba kura na umezima mitandao ya kijamii.
Sasa hao wananchi wako nao ni mabeberu?
Kuiba kura na kuzima mitandao ya kijamii nako si ubeberu?
Beberu ni lazima awe mzungu au Mmarekani?