Kuwasili kwa treni ya abiria jijini Arusha kwa mara ya pili baada ya miaka 30

Leo Jumatatu Shirika la reli linafanya majaribio ya safari za treni ya abiria toka Moshi kwenda Arusha. Mgeni mualikwa ni katibu mwenezi wa ccm Humphrey Polepole.

Nimejiuliza tu kumbe TRC ambalo ni shirika la umma, ni wakala wa CCM siku hizi?...
Kwani CCM siyo mali ya watanzania ?
 
Kwahiyo kutoka Dar mpaka Arusha ni treni? Price Tsh ngapi?
 
Mtapanda tu. Usilete kejeli wewe
Moshi kwenda Arusha wananchi wanatumia coaster bus TSH 3,000 kwa kutumia masaa 1.30 kuingia arusha.sasa train kutoka Moshi kwenda Arusha itatumika masaa 4 Nani wa kuisubiri? Itapalia abiria kwa TSH 330 au?
 
Hizo ni ndoto za mchana. Na ukiona unaota mchana ujue karibu utakuwa chizi
Apande huyo slow slow na mke wake!

Na mwisho wao wa kukaa uraiani ni pale Lissu akiapishwa kuwa rais, haya makando kando yote waliyoyafanya ccm yatawacost
 
Hata mimi naamini iko siku wapinzani watachukua nchi lakini si kizazi hiki cha sasa. Labda mwaka 2045
 
Kwani Kilimanjaro wanaishi Wachagga tu?
 
Wameamka kwa lipi mbona ni washamba tu
 
Udukumani kuna kila kitu. Kama train ipo, meli zipo, ndege zipo, magari yapo, dhahabu ipo, almasi ipo, Jiji lipo, wanawake wazuri wenye miguu kama chupa ya bia wapo, wasomi wapo, ng'ombe zipo na Rais yupo. Je, una lingine?
na heri huo ujinga angefanya ukanda wa wasukuma huko kaskazini anapoteza muda wake tu
 
Nalisikia ndio linaingia Arusha town saa hii na honi kama zote.
 
Hongera sana Magufuli kwa kweli,unastahili sifa zote.Mmm,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete waliturudisha nyuma sana kwa kweli.Hii ni hukumu kwao wote, popote walipo, hata kama sio ya mahakamani.
 
Ndio maana nimepita maeneo ya ushirika na kwa mr price kinyaa watu hakuna. Jamaa a yangu yupo Uchira anasema wamekodi Coaster kwenda kuishangilia treni. Ccm hoyeeee
Duh! mr price imefungwa zamani!!!!! huko Moshi wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…