Kwa aina ya mpira anaocheza Kylian Mbappe, atapotea baada ya kufikisha miaka 30

Kwa aina ya mpira anaocheza Kylian Mbappe, atapotea baada ya kufikisha miaka 30

Iwe jua iwe mvua nitasimama na
Mbappe.

Na wale wasiompenda wajiandae kupata heart attack maana Dogo anaendelea kuushangaza ulimwengu.

Our Mbappe
King of Football
#New Generation👌
Ya kale yamepita sasa ni mapya ya mtaalam Kylian🙌🔥🔥
Kiumbe Kitakachoushangaza ulimwengu ni E Haaland.
 
Nachukia mchezaji asiye na mnyumbuliko na ufundiufundi.
Mtu unakimbia mibio tuuuuu kama Kisinda zimekua riadha zile? Mtu kutoka watu wawili unashindwa. Siwahusudu wachezaji wa namna hiyo kabisa. Chezaji gumu halijui chenga unakuta. Nawachukia.
 
Kwanza naye alikuwa haoni vizuri kama sisi tu

Nimeshuhudia matukio mawili akiyatafsiri ndivyo sivyo kulingana na low quality ya streaming

Hadi kwenye sub napo alikuwa anachemka anataja watu wasio husika kama ndio wanaofanya mabadiliko
Yule sio football commentator ni mtangazaji wa movie kama Lufufu Eder Militao alikua anamuita Milato Nika mute sauti bora niangalie bila sauti kuliko kujazwa taka taka masikioni
 
Kila nikimuangalia huyu mchezaji ninaona anatumia mbio nyingi na ndio mafanikio yake yapo hapo.

Akishavuka miaka 30 hataweza kukimbia kwa kasi ya sasa hivi na hapo atapotea kama alivyopotea Christiano.
Sio mbio tu hata akili ya mpira na skills pia anazo za kutosha, swala la kupotea labda afanye maamuzi mabaya tu kwenye transfer ya club isiyokuwa potential kwake ila dogo anaujua mpira tena sana.
Ni mtu mwenye chuki binafsi tu ndo anayeweza kumbeza Christian Ronaldo
 
Nimesema angalau world cup moja halafu hapo uongeze na vigezo vingine kama copa america, club world, ballon d'or angalau tatu, FIFA player of the year angalau tatu, UCL angalau tatu.

Hapo Messi peke yake anakidhi vigezo.
Acha kuzuga GOAT tunaangalia world cup to full stop kwa sababu world cup ndio inayompima mchezaji ustahimilivu wake kama Pele kacheza hadi ana 38. Hizo UEFA sijui EPL za kila mwaka mbwembwe tu hizo.
 
Watu mliokuwa mnaangalia mpira kupitia TBC huwa hamfichiki

Kwa hiyo nawewe ulikuwa unamsikiliza Nazareth Upete na kumuamini?

Eti chenga ya aina moja' we ulitaka awe nazo pea ngapi?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila nikimuangalia huyu mchezaji ninaona anatumia mbio nyingi na ndio mafanikio yake yapo hapo.

Akishavuka miaka 30 hataweza kukimbia kwa kasi ya sasa hivi na hapo atapotea kama alivyopotea Christiano.
Hakuna ajuaye kesho ya mtu isipokuwa Mungu tu.........acheni uchawi
 
Ronaldo hajapotea akiwa na miaka 30, bado yupo na anafanya vizuri tu kwa umri wake, unless uchambuzi uhusishe mahaba yasiyopimika.

Mbappe anaweza potea hata akiwa na miaka 25 au asipotee mpaka anastaafu na miaka 35 na zaidi au akapotea na 30. Inategemeana na mambo mengi kama majeraha, kujituma, malengo binafsi, ushindani n.k

Kuna watu wana mihemko na messi na Ronaldo mpaka hawawezi kula. Mahaba kupitiliza ni Kilema cha akili, ni hitilafu. Ndo mwisho wa siku mpira hauwi burudani tena unagubikwa na uchambuzi usio na uhalisia na ubishani wa kimahaba.
Screenshot_20221219-153838_Chrome.jpg
 
1. Ronaldo hajapotea akiwa na miaka 30, sasas hivi ana miaka 38 na msimu uliopita tu alikuwa anagombania ufungaji bora, mchezaji akifika miaka 38 ni mkubwa sana, malegend wengi wanastaafu chini ya miaka 35.

2. Mbappe hahitaji hata kufika miaka 30 kuweka legacy yake, jamaa ana stats za kutisha sana, kama Rooney, Owen, Neymar na golden boy wengine huwa wanastaafu mapema sababu wameanza kucheza at top level wakiwa wadogo.

View attachment 2452173
Kiukweli takwimu za mbappe zinatisha kuliko hawa magwiji wawili vikubwa vinavyomgharimu dogo 1. Kwanza hana champions league sio kosa lake wote tunajua timu anayocheza haina kismati na ilo kombe kama barca, real madrid na mau u. 2. Hana ballon dor hii bila shaka ataichukua tu 3. Hana fanbase kubwa kama hao mabroo zake.. uenda messi na ronaldo wakistaafu mbappe ataanza kupewa heshima anayostahili
 
Ndo maana niliwahikushauri ni wakati sasa wa kutazama damu mpya zinachofanya zikiwa changa ili kuzitengenezea kiu ya mafanikio. Unapopigana katika jamii ambayo haikuangalii unachofanya sababu kuna watu wawili tu inawatazama si afya kwa kiu ya mafanikio. Imagine Mbappe anafananishwa na CR7 na Messi, seriously? Ni wakati wa kuruhusu hawa watu wawili.
 
Tatizo kwa sasa soka ni siasa na biashara sio passion kama zamani na system tayari ishawachagua messi na ronaldo. Yaan messi/ronaldo anatakiwa kuwa na moment moja tu nzuri uwanjani kuwafunika wengine wote na story nzima ikawa juu yake hata kama kuna mchezaji mwingine alikua vzr zaidi yake kwa siku iyo ila story ikiandikwa kupitia jina la messi au ronaldo itapata views nyingi, likes nyingi, shares nyingi n.k... yaan hawa jamaa wawili watundike daruga tu angalao kutakua na usawa kwa kiasi fulni
 
Kiukweli takwimu za mbappe zinatisha kuliko hawa magwiji wawili vikubwa vinavyomgharimu dogo 1. Kwanza hana champions league sio kosa lake wote tunajua timu anayocheza haina kismati na ilo kombe kama barca, real madrid na mau u. 2. Hana ballon dor hii bila shaka ataichukua tu 3. Hana fanbase kubwa kama hao mabroo zake.. uenda messi na ronaldo wakistaafu mbappe ataanza kupewa heshima anayostahili
Hata hio Baloon d or usipokua Madrid na Barca inabidi ukomae kisawa sawa.
 
Back
Top Bottom