Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Hoja yangu imejikita kwenye ufundi wa kufanya kampeni. Na ukumbuke kampeni ndo mchezo wenyewe wa siasa.

Wewe unadhani Magufuli amefanya mengi kwa mtizamo wako, ila hayo unayoyaona ni mengi kwenye ulingo wa kampeni, story itakuwa tofauti sana.

Magufuli anatakiwa kuwa imara wa hoja kwenye kampeni, kampeni ni vita vya hoja.

Na ujuzi wa wapinzani kwenye kampeni unaweza kukufanya ukajuta hata kwanini ukiongozwa na Magufuli.

Ufundi wa kampeni
Kampeni si alishafanya 2015 akashinda! Anashindwa vipi kufanya alichokifanya 2020?
 
Wapinzani wanakwenda na hoja nyingi kwenye kampeni lakini kubwa itakuwa hii ya ukandamizwaji wa haki za kiraia, uhuru wa vyombo vya habari, pamoja, usalama wa raia na ubaguzi wa kisiasa na hali ngumu ya maisha kwa sasa.

Kwa CCM hoja yao kuu ni ya ujenzi wa miundombinu Reli, barabara, Bwawa la umeme, Elimu bure, Afya nk

Hoja ambazo zitavutia wananchi wengi ni zile za wapinzani...maana zinawagusa directly......suala la maisha magumu linawagusa karibia 80% ya watanzania...ubaguzi wa kisiasa wameuona kwa macho!!
 
Magufuli ni mzuri kwenye ubabe,hofu ni vitisho. Muniombee nimejenga flyover 😂 😂😂
 
Naomba uwaze kama mtu mwenye akili timamu.Usijichetua ubongo kama CCM
Mtu mjinga mjinga utamshauri nini mpaka akuelewe?Nitatumia njia gani kuwashauri hao mamilioni ya watu?Kwa platform gani na nitatoa wapi resources?Na watanisikiliza kwa vile nina mamlaka gani??
Punguza ujuaji Mkuu Unajifanya unajua kumbe HUJUI!!!
 
Nafikiri udikteta yaani hakuna hata haja ya kusema kitu; inajulikana magu hasikilizi waandamizi wake na hufanya mambo bila hata kushirikisha bunge mifano ipo mingi mno. Unaona hata hakuruhusu demokrasia ndani ya ccm kuhusu wagombea wengine, ukitaka magu akuchukie hata akutumie watu wakuue wewe mpe changamoto, akina Lissu, Mbowe ni matokea machache tu ya maelfu walioteswa.

Ukabila: angalia baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya achilia mbali vyeo vingine fanya hesabu utashangaa
Ubabe; hata hili unataka maelezo?

Udini; tulizoea ulinganifu wa dini ila siku hizi hiyo busara haipo tena.
Kwà mbowe hapo Hakuna Ukweli wowote zaidi ya kutafuta huruma za wananchi tu, Pia naomba nitajie Baraza la mawaziri wakabila lake wizara 3 tu Mkuu yaani wawe Full ministers na sio Deputy Ministers!!! Bado hoja ya dini hujajibu mkui
 
Punguza ujuaji Mkuu Unajifanya unajua kumbe HUJUI!!!
Povu ruksa!

Una majibu ya kitoto eti nikawashauri.Nakuuliza kwa means ipi unassma nipunguze ujuaji.Wewe na hao wasio jielewa ni wa kushauriwa pia.
 
Sioni kama kuna namna yoyote ya kumuangusha Magufuli
 
Tulisumbuka kumjua Magufuli 2015, lakini leo hii tunajua tutapata nini kama akichaguliwa. Watanzania wanataka matokeo na sio maneno au ulevi. Muda wa kumtafakari umepita.
Kosa sio lako ni la mzazi

Andika ulichotaka kuandika,Hili jukwaa sio la mipasho na majigambo

Jenga hoja kupinga au kukataa

Mfano:Sikubaliani na mleta uzi kwa kuwa Magufuli ni jasiri wa maamuzi kwenye baadhi ya mambo mfano ugonjwa wa corona

Mfano 2:Nakubaliana na uzi kwa kuwa halimudu jukwaa vizuri kwani mheshimiwa anachomekea maneno yanayokera mfano udhalilishaji kwa Das ukerewe

Sasa wewe mpumbavu unaleta mipasho na vioja hapa JF

Hayo mambo peleka chamani kwako
 
Povu ruksa!

Una majibu ya kitoto eti nikawashauri.Nakuuliza kwa means ipi unassma nipunguze ujuaji.Wewe na hao wasio jielewa ni wa kushauriwa pia.
Punguza ujuaji Mkuu!! WaTZ sio wajinga Kama unavyofikiri et Bongo Movies ndio inajaza Watu hivi uko sawasawa kweli kichwani au ulienda Shule kusomea UJINGA!??

CCM inawazidi Vyama kwa COVARAGE mipango na mikakati katika kampeni wanajipanga haswa eti 97% wajinga Yaan kwa Percentage hiyo inaleta logic wewe na familia yako yote mpo ndani ya hiyo Percentage!!!
 
Punguza ujuaji Mkuu!! WaTZ sio wajinga Kama unavyofikiri et Bongo Movies ndio inajaza Watu hivi uko sawasawa kweli kichwani au ulienda Shule kusomea UJINGA!??

CCM inawazidi Vyama kwa COVARAGE mipango na mikakati katika kampeni wanajipanga haswa eti 97% wajinga Yaan kwa Percentage hiyo inaleta logic wewe na familia yako yote mpo ndani ya hiyo Percentage!!!
Nilienda kusomea ujinga.
Ila mimi sio mjinga kuliko wewe.
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
Hao ulio wataja (Lissu na Membe) wakipambanishwa na Magufuli ni sawa kupampanisha Magufuli na giza na kuwaambia binadamu wachague! Lissu na Membe ni giza, chocbote watakacho kiongea iwe ni hoja au ni kupinga hoja za Magufuli - itakuwa ni giza ni nadharia tu. Vitendo vya Magufuli tumeisha viona hata akisimama jukwaani kama bubu, kila mtu anajua uwezo wake. Hata watoto wadogo ambao hawapigi kura.
Hawa wengine itakuwa ni kujitembeza tu! Ndiyo maana wanaotaka katiba ibadilishwe Magufuli aongoze milele wanazidi kuongezeka exponentially
 
Yote hayo atatakiwa kujieleza kwenye kampeni ndugu.

Usilazimike wewe kuwalisha watu maneno kwamba kuna vingi vimefanywa.

Ndo mana nikasisitiza, endapo akipambana na mtu mwenye uwezo wa kujenga na kuvunja hoja kama Tundu Lissu, atakuwa na wakati mgumu sana kwenye kampeni.
Ila Tundu Lissu hatakuwepo, toa mifano inayokubalika! Tundu Lissu by all means hatakuwepo
 
Wapiga kura wa nchi hii wengi huwa wana maamuzi yao tayari kabla hata ya kampeni.

Wanachagua vyama zaidi kuliko watu au hoja!

Ndo maana Lowasa aliyekuwa anaongea kama anaelekea kukata moto alipata kura nyingi kuliko Anna Mgwira aliyekuwa akiwasilisha vyema na mambo yenye mashiko.
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!

Atatolea maelezo lile kundi lake la watu wasiojulikana? Udhaifu wa Magufuli kujieleza uko wazi, ndio maana wanaccm hawako tayari Magufuli aingie kwenye kampeni na mshindani, hasa ya aina ya Lissu. Wanajua kilichomkuta JK vs Slaa uchaguzi wa 2010, hawako tayari kimkute Magufuli 2020.
 
We nawe kama hufikiri. Membe kazaliwa leo? Hatuangalii hoja tunaangalia matendo. Magufjli ana vitu vikubwa kafanya vinamsemea hata kama angegeuka bubu tutamchagua tena. Propaganda hazina kazi tena kwa sasa mkuu. Hoja wasubiri 2025 ambapo huyu atakuwa anaondoka na wanaokuja hawana cha kuonekana. Sijui kama unanielewa. Hata hawa kina Lissu wanatafuta aibu tuu. Maembe ndiyo kabisaaaaaa maana hata 2015 alikuwepo pia. Magu hana mbadala mpaka 2025.
 
Wapinzani wasibweteke,wahakikishe wanaunganisha nguvu pamoja(Wapinzani wa Kweli) na wakiweza kuhamasisha wapiga kura na kuhakikisha wanazilinda ipasavyo,CCM mpya ni wepesi mno.Wamefanya kampeni peke yao kwa miaka mitano lakini bado wanawazuia wapinzani kufanya siasa hata mikutano ya ndani.
Wanafahamu kuwa wanaenda kushindwa,hivyo tujihadhari(They are dangerously despedesperate),we need to act with caution.
 
Kwà mbowe hapo Hakuna Ukweli wowote zaidi ya kutafuta huruma za wananchi tu, Pia naomba nitajie Baraza la mawaziri wakabila lake wizara 3 tu Mkuu yaani wawe Full ministers na sio Deputy Ministers!!! Bado hoja ya dini hujajibu mkui
Unawajua wote mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya karibu nusu wanatoka kanda moja. Magu ameharibu sana nchi yetu na kwa bahati mbaya watz wengi hawaelewi; siku hizi ukabila umezidi na kufanya mambo bila mpango wala utaratibu ndio kawaida ya siku hizi. Jiwe anapaswa kuelewa kuwa mwisho wa siku atajibu tuhuma peke yake na wote wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa watamkana kabisa atakapomaliza muda wake. Asishangae akisimama mbele ya majaji anaowachagua yeye kujibu mashtaka mbalimbali. Dunia imebadilika sana. Rais wa Malawi aliyepita sasa anakamatwa na polisi wake na pia anakwenda kuhukumiwa na majaji aliowachagua mwenyewe, ndivyo itakavyokuwa kwa jiwe ni suala la muda tu. Msaidieni sio kumdanganya, najua ni vigumu kwasababu sio mtu mnyenyekevu.
 
Enzi za porojo na mapambio kwenye majukwa ya kampeni zimeshapita. Watu watakupima kwa matendo yako ya nyuma na unayokusudia kuyafanya.

Kwa bahati nzuri Matendo ya kimaendeleo ya Rais Magufuli yamedhihirika kwa kila mwananchi mwenye macho ...Matendo yake ni tiketi ya moja kwa moja ya kuingia kwa kishindo katika awamu ya pili
Swali ni kuwa ni nani atakayesimama kwenye jukwaa la kampeni kuwaeleza watu wa Kigoma kuwa DSM kumejenwa madaraja ya kupitisha magari kwa juu na nini faida yake kwa watu wa Kigoma. Hapo ndo panahitajika ufundi mkuu. Kusifu kupita kiasi kunaharibu uelewa wa watu wengi kumbe
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
Sasa kama vitu vinaonekana kwa nini ccm wanatumia nguvu nyingi kumpamba? Kila kukicha ndege, sgr or mara sijui nini! Si mkae kimya tu kwani watanzania wanaelewa!
 
Seek not for words, seek only for facts and thought and crowding in will come the words unsought.

By Horace

By the way

Jina lako limekaa Kama la Porn [emoji93]
 
Back
Top Bottom