Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Kwa hoja hawezi Jenga hoja, afrika mashariki ni Kenyatta pekee ndie mjenga hoja mzuri na mtamu kumsikiliza ni mtu anae toa fact yaani madini na mwenye confidence ya kujibu hoja kwa hoja na si kutegemea kubebwa.
 
Sasa kama vitu vinaonekana kwa nini ccm wanatumia nguvu nyingi kumpamba? Kila kukicha ndege, sgr or mara sijui nini! Si mkae kimya tu kwani watanzania wanaelewa!
Ni kwa sababu vimeshindwa kuibadilisha Jamii ili Ione faida achilia Propaganda
 
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
Huyo Lisu mbona bado anajificha huko ubelgiji hadi mida hii. Anaogopa sio?
 
Unawajua wote mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya karibu nusu wanatoka kanda moja. Magu ameharibu sana nchi yetu na kwa bahati mbaya watz wengi hawaelewi; siku hizi ukabila umezidi na kufanya mambo bila mpango wala utaratibu ndio kawaida ya siku hizi. Jiwe anapaswa kuelewa kuwa mwisho wa siku atajibu tuhuma peke yake na wote wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa watamkana kabisa atakapomaliza muda wake. Asishangae akisimama mbele ya majaji anaowachagua yeye kujibu mashtaka mbalimbali. Dunia imebadilika sana. Rais wa Malawi aliyepita sasa anakamatwa na polisi wake na pia anakwenda kuhukumiwa na majaji aliowachagua mwenyewe, ndivyo itakavyokuwa kwa jiwe ni suala la muda tu. Msaidieni sio kumdanganya, najua ni vigumu kwasababu sio mtu mnyenyekevu.
Nitajie mawaziri wa3 tu wa kabila lake mkuu wasiwe manaibu waziri maswala ya ukanda sitaki kusikia...
 
hivi membe ni mtoa hoja mahiri kweli?
 
kwanza nikusahihishe jiwe hahutubii bali anafoka.
hawezi kushindana na Lissu. tena ukimkutanisha kwenye mdahalo ndo kabisaaa. ukitaka kujua kiongozi shalo tazama anavyohutubia...anafoka na kutisha tisha ili tusione udhaifu wake
 
Hoja yangu imejikita kwenye ufundi wa kufanya kampeni. Na ukumbuke kampeni ndo mchezo wenyewe wa siasa.

Wewe unadhani Magufuli amefanya mengi kwa mtizamo wako, ila hayo unayoyaona ni mengi kwenye ulingo wa kampeni, story itakuwa tofauti sana.

Magufuli anatakiwa kuwa imara wa hoja kwenye kampeni, kampeni ni vita vya hoja.

Na ujuzi wa wapinzani kwenye kampeni unaweza kukufanya ukajuta hata kwanini ukiongozwa na Magufuli.

Ufundi wa kampeni

Unachosahau watanzania wameshaskia maneno mazuri toka kwa Mwalimu yanatutosha. Au unahitaji LINK Mkuu.
 
Hoja yangu imejikita kwenye ufundi wa kufanya kampeni. Na ukumbuke kampeni ndo mchezo wenyewe wa siasa.

Wewe unadhani Magufuli amefanya mengi kwa mtizamo wako, ila hayo unayoyaona ni mengi kwenye ulingo wa kampeni, story itakuwa tofauti sana.

Magufuli anatakiwa kuwa imara wa hoja kwenye kampeni, kampeni ni vita vya hoja.

Na ujuzi wa wapinzani kwenye kampeni unaweza kukufanya ukajuta hata kwanini ukiongozwa na Magufuli.

Ufundi wa kampeni
Kwani 2015 wewe ndo ulikuwa kampeni meneja wake sasa umejitoa?

Kama alieleweka kabla ya kuonesha umahiri wake wa utekelezaji kwa nn Sasa isiwe ndio kampeni rahisi zaidi kwake kuliko 2015. Kila ataposimama analojambo alilotenda kwa jamii husika ktk kutatua kero so hatahitaji maneno. He will be just pointing to what he have done on a particular area on his first 5yrs term as our Rais. [emoji122][emoji122]
 
Hapa CCM wangeomba mjadala wa wagombea wengine yaani Membe,Lisu na Magufuli..hapa ndy patamu!mjadala uwe live kama Marekani !!
Vipi hutaki wafanyakazi waongezewe mishahara na kupandishw madaraja, wastaafu wapewe stahiki zao mapema, kuwe na uhuru wa vyombo vya habari, hutaki mkuu kuwe na uhuru wa kuishi watu waachwe kutekwa na kupigwa risasi mchana kweupe, hutaki kuona bunge na mahakama kuwa ni mihimili inayojitegemea, hutaki kuona matumizi ya nchi kufuata budget iliopitishwa na bunge??
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
Ameshajieleza na kufanya kampeni kwa miaka mitano sioni ni cha ziada ataongea
 
Yote hayo atatakiwa kujieleza kwenye kampeni ndugu.

Usilazimike wewe kuwalisha watu maneno kwamba kuna vingi vimefanywa.

Ndo mana nikasisitiza, endapo akipambana na mtu mwenye uwezo wa kujenga na kuvunja hoja kama Tundu Lissu, atakuwa na wakati mgumu sana kwenye kampeni.
Mfano watu watakuja na data kuwa uchumi umeshuka na maisha ya watu yameporomoka, hapo huwezi kuwaambia watu nimejenga daraja ukaeleweka.
 
Tatizo mnatoa maoni humu,lakini kwenye field jamaa anakubalika.
 
Enzi za porojo na mapambio kwenye majukwa ya kampeni zimeshapita. Watu watakupima kwa matendo yako ya nyuma na unayokusudia kuyafanya.

Kwa bahati nzuri Matendo ya kimaendeleo ya Rais Magufuli yamedhihirika kwa kila mwananchi mwenye macho ...Matendo yake ni tiketi ya moja kwa moja ya kuingia kwa kishindo katika awamu ya pili
Enzi tulizonazo ni za hoja, kama kujenga madaraja hata mtoto wangu ukimkabidhi pesa za kujenga daraja atajenga.

Kiongozi ni strategic thinker sio mbeba matofali.
 
Vipi hutaki wafanyakazi waongezewe mishahara na kupandishw madaraja, wastaafu wapewe stahiki zao mapema, kuwe na uhuru wa vyombo vya habari, hutaki mkuu kuwe na uhuru wa kuishi watu waachwe kutekwa na kupigwa risasi mchana kweupe, hutaki kuona bunge na mahakama kuwa ni mihimili inayojitegemea, hutaki kuona matumizi ya nchi kufuata budget iliopitishwa na bunge??
Kama umeelewa utagundua nin mana ya nilichoandika!!mjadala wa wazi kuna mtu ataondoka kwenye line!!
 
Miaka
Nimemuangalia Rais Magufuli kwenye mikutano mingi sana akihutubia. Niseme tu kuna uhodari fulani anaukosa kwenye kuhutubia ambao ni 'Precision' - usahihi na umakini wa maneno.

Usahihi na umakini ni silaha muhimu sana unapoongea kwenye umati wa watu ambao wanatofautiana utamaduni, imani, na uwezo wa kimaisha.

Ukifuatilia hotuba za Magufuli vizur, utagundua imekuwa ni kawaida kupata utata mwingi sana, ambao mara nyingi unagawa hisia za watu.

Kwa darubini hiyo, endapo Magufuli akipambana na mtu ambaye ni makini kwenye utoaji wa hoja kwenye jukwaa kama Tundu Lissu au Bernard Membe, ni wazi kabisa Magufuli atateseka sana kwenye uwanja wa kampeni.

Maana watatumia hiyo weakness yake kumkaanga kwa kutumia reference ya alichokiongea kwenye jukwaa.

Mfano tu, kwa haiba ya Magufuli, sitashangaa akihutubia kwa Kisukuma akipiga kampeni kanda ya ziwa, kitu ambacho najua kitakuwa kinampunguzia credibility kwa watanzania, kwamba kuna harufu ya ukabila na ukanda ambacho pia hakitasaidia sana CCM maeneo mengine ya nchi.

Mambo kama hayo na mengi mengine, ndio yanaenda kufanya huu uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kipekee sana.

CCM wana dola, lakini wajue tu kwamba Dola haitapanda jukwaani kupiga kampeni.

Ikiwa CCM wakijisahau sana, kampeni zitaenda kuchochea hisia za wananchi kuelekea upande wa upinzani kama ilivotokea mwaka 2010 na 2015 ambapo nguvu ya umma ilisaidia sana upinzani kwenye kupata viti vya ubunge na udiwani.

Hii ina maanisha, itakuwa ni kazi ngumu sana kwa dola kuhakikisha aliyeshindwa kwenye kampeni lazima atawale, maana watakuwa wanashindana na nguvu ya umma ya wananchi, kitu ambacho kitaweka shakani amani ya nchi.

Kwa hili, ndo maana nna imani kabisa, kama upinzani wakifanikiwa vizur kwenye kampeni kuanzia urais hadi udiwani, kitu ambacho kitapelekea kupata kura nyingi za wananchi, mambo yatakuwa ni tofauti sana.

Mshindi lazima tu atatangazwa na ni yule ataeshinda. CCM wakishindwa kwenye kampeni na wakishindwa kushawishi wananchi, wasahau kabisa ushindi wa mezani. Hata Dola itashindwa kuwahakikishia ushindi.

Ndo maana ya ule usemi, mwenye nacho huongezewa. Kama CCM haitakuwa nacho kwenye kampeni, isitegemee kuongezewa au favour. Haitakuwepo
Miaka mitano ya mwanzo ya Magufuli kaitumia kufanya kampeni kwa vitendo, ingawaje ni kweli hotuba zake sio za kisiasa, Tundu Lissu anaongea upuuzi na uchonganishi wa kuvuruga nchi, kuirudisha nyuma nchi, hana lolote la kumshinda Magufuli, kugombea kwake ndiyo kifo cha CHADEMA.
 
Nitashangaa sana iwapo unachagua mtu kwa kupima idadi ya alivyojenga badala ya kuangalia na mambo mengine ya msingi kama democracy,na hata Hali za maisha za Watanzania kwa ujumla wao,Hatuwezi kuwa na viongozi ambao vipaumbele vyao ni ujenzi badala ya wananchi.Ujenzi ni sehemu ya maendeleo lakini ustawi na mustakabali wa wanajamii ni jambo lingine jema.Watu wanataka Katrina maya, watu wanataka elimu bora,watu wanataka kujikwamua kiuchumi,watu watumishi wanataka nyongeza ya mishahara yao na mengineyo.CCM mlipata kura yangu ya urais 2015 sasa hivi nayaangalia chama mbadala
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!

Upo sahihi
Je ni kwanini anazuia mikutano na kukamata wengine wakifanya siasa?
 
Back
Top Bottom