Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

Kwa hoja hawezi Jenga hoja, afrika mashariki ni Kenyatta pekee ndie mjenga hoja mzuri na mtamu kumsikiliza ni mtu anae toa fact yaani madini na mwenye confidence ya kujibu hoja kwa hoja na si kutegemea kubebwa.
 
Sasa kama vitu vinaonekana kwa nini ccm wanatumia nguvu nyingi kumpamba? Kila kukicha ndege, sgr or mara sijui nini! Si mkae kimya tu kwani watanzania wanaelewa!
Ni kwa sababu vimeshindwa kuibadilisha Jamii ili Ione faida achilia Propaganda
 
Huyo Lisu mbona bado anajificha huko ubelgiji hadi mida hii. Anaogopa sio?
 
Nitajie mawaziri wa3 tu wa kabila lake mkuu wasiwe manaibu waziri maswala ya ukanda sitaki kusikia...
 
hivi membe ni mtoa hoja mahiri kweli?
 
kwanza nikusahihishe jiwe hahutubii bali anafoka.
hawezi kushindana na Lissu. tena ukimkutanisha kwenye mdahalo ndo kabisaaa. ukitaka kujua kiongozi shalo tazama anavyohutubia...anafoka na kutisha tisha ili tusione udhaifu wake
 

Unachosahau watanzania wameshaskia maneno mazuri toka kwa Mwalimu yanatutosha. Au unahitaji LINK Mkuu.
 
Kwani 2015 wewe ndo ulikuwa kampeni meneja wake sasa umejitoa?

Kama alieleweka kabla ya kuonesha umahiri wake wa utekelezaji kwa nn Sasa isiwe ndio kampeni rahisi zaidi kwake kuliko 2015. Kila ataposimama analojambo alilotenda kwa jamii husika ktk kutatua kero so hatahitaji maneno. He will be just pointing to what he have done on a particular area on his first 5yrs term as our Rais. [emoji122][emoji122]
 
Hapa CCM wangeomba mjadala wa wagombea wengine yaani Membe,Lisu na Magufuli..hapa ndy patamu!mjadala uwe live kama Marekani !!
Vipi hutaki wafanyakazi waongezewe mishahara na kupandishw madaraja, wastaafu wapewe stahiki zao mapema, kuwe na uhuru wa vyombo vya habari, hutaki mkuu kuwe na uhuru wa kuishi watu waachwe kutekwa na kupigwa risasi mchana kweupe, hutaki kuona bunge na mahakama kuwa ni mihimili inayojitegemea, hutaki kuona matumizi ya nchi kufuata budget iliopitishwa na bunge??
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!
Ameshajieleza na kufanya kampeni kwa miaka mitano sioni ni cha ziada ataongea
 
Mfano watu watakuja na data kuwa uchumi umeshuka na maisha ya watu yameporomoka, hapo huwezi kuwaambia watu nimejenga daraja ukaeleweka.
 
Tatizo mnatoa maoni humu,lakini kwenye field jamaa anakubalika.
 
Enzi tulizonazo ni za hoja, kama kujenga madaraja hata mtoto wangu ukimkabidhi pesa za kujenga daraja atajenga.

Kiongozi ni strategic thinker sio mbeba matofali.
 
Kama umeelewa utagundua nin mana ya nilichoandika!!mjadala wa wazi kuna mtu ataondoka kwenye line!!
 
Miaka
Miaka mitano ya mwanzo ya Magufuli kaitumia kufanya kampeni kwa vitendo, ingawaje ni kweli hotuba zake sio za kisiasa, Tundu Lissu anaongea upuuzi na uchonganishi wa kuvuruga nchi, kuirudisha nyuma nchi, hana lolote la kumshinda Magufuli, kugombea kwake ndiyo kifo cha CHADEMA.
 
Nitashangaa sana iwapo unachagua mtu kwa kupima idadi ya alivyojenga badala ya kuangalia na mambo mengine ya msingi kama democracy,na hata Hali za maisha za Watanzania kwa ujumla wao,Hatuwezi kuwa na viongozi ambao vipaumbele vyao ni ujenzi badala ya wananchi.Ujenzi ni sehemu ya maendeleo lakini ustawi na mustakabali wa wanajamii ni jambo lingine jema.Watu wanataka Katrina maya, watu wanataka elimu bora,watu wanataka kujikwamua kiuchumi,watu watumishi wanataka nyongeza ya mishahara yao na mengineyo.CCM mlipata kura yangu ya urais 2015 sasa hivi nayaangalia chama mbadala
 
Kwani kuna kitu Magufuli anahitaji kuwaleza watanzania wasio kijua au kukielewa? Magufuli ahitaji kujieleza chochote kwa mtanzania ...matendo na mambo yake yanaonekana wazi!

Upo sahihi
Je ni kwanini anazuia mikutano na kukamata wengine wakifanya siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…