Uchaguzi 2020 Kwa aina ya utoaji hoja wa Magufuli, atapata shida sana kwenye kampeni akipambana na mtu dizaini ya Tundu Lissu au Bernard Membe

kwani ndo mara ya kwanza yeye kupiga kampeni? we nawe uelewa wako ni mdogo sana
 
Huyo Lisu unayemsifia amejaa hasira, jazba na majigambo mwanasheria msomi hana lolote
msi
 
Hakuna tume huru hivyo atapita
Pammoja na kutowepo tume huru,Magufuli atashinda kwa jinsi alivyojitwisha miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa.
Mtu wa kuhakikisha inakamilika kwa wakati ni yeye tu.
Hakuna jinsi hasa hii miaka 5 ijayo.
 
Pammoja na kutowepo tume huru,Magufuli atashinda kwa jinsi alivyojitwisha miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa.
Mtu wa kuhakikisha inakamilika kwa wakati ni yeye tu.
Hakuna jinsi hasa hii miaka 5 ijayo.
Kwa hiyo anakamilisha kwa pesa yake?
 
Atasema alinunua wabunge wa upinzani akawaingiza sisiemu
 
Anamaanisha kuwashauri vyama vya upinzani, siyo mamilioni ya watu
 
Kwa hiyo anakamilisha kwa pesa yake?
Pesa yetu,hakuna jinsi,ila akitaka new projects apart from these,apate hisani au approval ya Bunge kwanza,vinginevyo taifa litaingia matatani.
 
Hatuna shida na porojo sie tunataka actions; sasa bank yenu tayari ina i-rank Tanzania kuwa ya uchumi wa kati.
 
This is bullshit thread
 
Umeibua swala muhimu sana kwenye kampeni, na ukweli una kawaida ya ubishi wa kufichika. Lakini hii point yako imekuwa ngumu sana kuwaingia Watanzania. Kote hata jana nilipita Uswaa/ Machame nikienda Upareni na swali hili lili ibuka , lakini watu wote wanakwambia waongeaji wazuri hawawataki kwao ni wanini ? wao wanataka matokeo. Na ambayo Magufulu anawapa.
 
Yaah kabisa ingepaswa mdahalo kufanyika 2015.

Nna imani kabisa midahalo ni njia nzuri sana ya kumsoma kiongozi, sijui kwanini Tanzania huwa haifanyiki hii kitu
Mwaka 1995 mgombea wa CCM, Mkapa alikuwa hoi dhidi ya Mrema lakini elimu yake na uwezo wake wa kujenga hoja ulimsaidia kushinda uchaguzi ule. Mkapa hakuwa anajulikana sana na wananchi kwasababu alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje lakini mpinzani wake aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu kwa hiyo alijulikana na kupendwa sana hasa na vijana lakini alishindwa uchaguzi. Nyota ya Mkapa iliyomsaidia kushinda ilijitokeza kwenye MIDAHALO ya wazi na wapinzani wake ambayo ikampaisha mpaka ushindi kwa sababu aliwafunika wote na kuinuka kidedea. Bahati mbaya sana pamoja na ushindi huo, CCM kikaogopa kabisa MIDAHALO kwenye kampeini za uchaguzi. Mkapa alikuwa wa kwanza na wa mwisho kushiriki! Kikwete pamoja na umahili wake wa lughà hakushiriki kwa sababu Chama chake hakikuafiki ingawa wapinzani wachache walishiriki. Magufuli pia hakushiriki kwa sababu hizohizo lakini yeye aliishia kufanya push-up jukwaani na kushinda so kwa kishindo.
 
Suala la Magufuli kuleta matokeo bado ni subjective sana. Huwez kuwaaminisha watu wa huko vijijini kwamba Magufuli anapiga kazi kwa kununua ndege ambazo wengine wataishi watakufa hawatazipanda.
 
Suala la Magufuli kuleta matokeo bado ni subjective sana. Huwez kuwaaminisha watu wa huko vijijini kwamba Magufuli anapiga kazi kwa kununua ndege ambazo wengine wataishi watakufa hawatazipanda.
Kuna ukweli ambao tutaupinga kwa sababu siasa inatuamrisha tufanye hivyo, upinzani unataka uzungumze yale ambayo hayajafanywa.

Lakini hakuna sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania ambayo haijaona mkono wa Magufuli kwa hiki ama kile na maeneo mengi yameona karibu vitu vyote kwa pamoja.

Kila binadamu anafikiri kivyake na ana haki ya kusema kile ambacho anafikiri ni muhimu kuliko vingine. Ila kwa maendeleo ya pamoja yanayo wagusa wengi na kwa muda mfupi kwa Mkoa wa Kilimanjaro ni hii mara ya kwanza.

Siwezi kusemea mchango wa Rais Magufuli mikoa mikoa mingine ambayo sikupa bahati kuitembelea kwa hii miaka mitano.
 
Nawaangalia Halafu Nasema Hii Bhaghoshaa.
😁😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…