Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Magufuli ana washabiki wengi?

Ila hivyo vigezo vyako hata haters wa Magufuli wanavyo!
Katika nchi kiujumla kuna watu wengi wa aina hiyo, wengine wana nyadhifa kubwa tu.

Ndiyo maana unaona hata kwa wanaompinga Magufuli kuna watu wanamshambulia kishamba kwa makosa ambayo hajayafanya ila wanategemea atayafanya 2025!

Na polisi wa Magufuli wakizuia maandamano ya wapinzani, kwa makosa ambayo wapinzani hawajayafanya ila wanatarajiwa kuyafanya, wapinzani hao watalalamika kwamba polisi wanawazuia kinyume na haki.

Double standard.

Ujinga juu ya ushamba pande zote.
 
Kosa kubwa unalolifanya ni kuanza kuwaza kuwa Rais Maguli atajiongezea Muda! Waza nini atakifanyia nchi na aliahidi nini kipindi hiki!
Alishasema kuwa hataongeza muda na hapendi harakati za akina Juma nkamia! Acheni ramli chonganishi.
Mimi hata mwizi anayejulikana kwamba ni mwizi, watu wakitaka kumfunga kwa wizi ambao hajaufanya bado ila watu wanasema atakuja kuufanya miaka mitano baadaye, nitamtetea kwamba kumhukumu kwa wizi ambao hajaufanya ila watu wanatarajia aufanye si haki.

Hususan kwa sababu, huyu ni mwizi, kashaiba, anaweza kushitakiwa kwa wizi aliokwishaufanya tayari.

Sasa, kwa nini unataka kumhukumu mwizi kwa wizi unaosema atakuja kuufanya miaka mitano baadaye, wakati mwizi huyu kashaiba mwaka huu, na anaweza kuhukumiwa kwa wizi huo ambao ushatokea tayari?

Tumhukumu Magufuli kwa makosa aliyoyafanya.Yapo mengi tu.Hatuna uhaba wa makosa ya Magufuli aliyokwisha yafanya.

Tusimhukumu kwa ubashiri wa makosa tunayofikiri anaweza kuyafanya mwaka 2025.

Tukianza kuhukumiana kwa makosa tunayofikiri yatafanyika baadaye, hakuna atakayebaki salama.

Atatokea Polisi umemshinda swaga kitaani kwenye kuwania mwanamke, atasema wewe sura yako imekaa kama mwizi wa miaka ijayo, tukuwahi kukufunga jela kabla hujaiba ili kuepusha wizi utakaokuja kuufanya badaye.

Kumbe ni gubu lake tu la hila kwa sababu umemshinda kutongoza.

Ni kanuni ile ile tu ya kumhukumu Magufuli leo, kwa makosa ya kufikirika ambayo watu wanabashiri atayafanya mwaka 2025.
 
Katika nchi kiujumla kuna watu wengi wa aina hiyo, wengine wana nyadhifa kubwa tu.

Ndiyo maana unaona hata kwa wanaompinga Magufuli kuna watu wanamshambulia kishamba kwa makosa ambayo hajayafanya ila wanategemea atayafanya 2025!

Na polisi wa Magufuli wakizuia maandamano ya wapinzani, kwa makosa ambayo wapinzani hawajayafanya ila wanatarajiwa kuyafanya, wapinzani hao watalalamika kwamba polisi wanawazuia kinyume na haki.

Double standard.

Ujinga juu ya ushamba pande zote.
Kuna mtu humu kanituhumu ukabila, kisa tu nimesema Magufuli hataongeza muda.

Je, huo nao ni ushamba?

Mimi sikusukumwa na ukabila nilivyosema kuwa hataongeza muda wa kukaa ikulu.

Lakini mtu anaibuka na kudai kuwa namtetea Magufuli [I don’t know how] kwa sababu ya ukabila.

Kwa vigezo vyako huo lazima uwe ushamba aisee.

Siyo?
 
Naona kabisa akiongeza muda, kwa nini awamu hii ndo kuna hisia za kuongeza muda? " Atake ama asitake tutamuongezea" ndugai. Kwa hizi sifa na mapambio ataongeza labda mtu afe kabla ya 2025
 
Hii mitano yenyewe kajiongezea.
Unataka ajiongezee mara.
Huu UCHAFUZI hajashinda.
 
Mimi hata mwizi anayejulikana kwamba ni mwizi, watu wakitaka kumfunga kwa wizi ambao hajaufanya bado ila watu wanasema atakuja kuufanya miaka mitano baadaye, nitamtetea kwamba kumhukumu kwa wizi ambao hajaufanya ila watu wanatarajia aufanye si haki.

Hususan kwa sababu, huyu ni mwizi, kashaiba, anaweza kushitakiwa kwa wizi aliokwishaufanya tayari.

Sasa, kwa nini unataka kumhukumu mwizi kwa wizi unaosema atakuja kuufanya miaka mitano baadaye, wakati mwizi huyu kashaiba mwaka huu, na anaweza kuhukumiwa kwa wizi huo ambao ushatokea tayari?

Tumhukumu Magufuli kwa makosa aliyoyafanya.Yapo mengi tu.Hatuna uhaba wa makosa ya Magufuli aliyokwisha yafanya.

Tusimhukumu kwa ubashiri wa makosa tunayofikiri anaweza kuyafanya mwaka 2025.

Tukianza kuhukumiana kwa makosa tunayofikiri yatafanyika baadaye, hakuna atakayebaki salama.

Atatokea Polisi umemshinda swaga kitaani kwenye kuwania mwanamke, atasema wewe sura yako imekaa kama mwizi wa miaka ijayo, tukuwahi kukufunga jela kabla hujaiba ili kuepusha wizi utakaokuja kuufanya badaye.

Kumbe ni gubu lake tu la hila kwa sababu umemshinda kutongoza.

Ni kanuni ile ile tu ya kumhukumu Magufuli leo, kwa makosa ya kufikirika ambayo watu wanabashiri atayafanya mwaka 2025.
Hili jambo ni rahisi sana.

But for some reason, kuna naona hawalielewi kabisa. Ni kama somo flani hivi lililo gumu.

Sijui kwa nini tu inaonekana kama vile ni somo gumu kulielewa.

Au labda wamejawa na chuki/ hisia hasi [negative feelings] kiasi kwamba chuki zao zimeghubika kabisa akili zao?

Mtu bado hajalifanya kosa. Lakini anazungumziwa kana kwamba keshalifanya.

SMH!!!
 
Kuna mtu humu kanituhumu ukabila, kisa tu nimesema Magufuli hataongeza muda.

Je, huo nao ni ushamba?

Mimi sikusukumwa na ukabila nilivyosema kuwa hataongeza muda wa kukaa ikulu.

Lakini mtu anaibuka na kudai kuwa namtetea Magufuli [I don’t know how] kwa sababu ya ukabila.

Kwa vigezo vyako huo lazima uwe ushamba aisee.

Siyo?
Tabia moja ya ushamba ni kufanya assumptions kirahisi.Kama nilivyosema, tabia hii inaendana na lack of sophistication.

Watu washamba wanaendana na kukosa elimu na kukosa uwezo wa kuchambua mambo kwa kina.

Kama hivi.

Msukuma anayemtetea Magufuli ni lazima awe mkabila.Hili si kweli, mimi natetea haki ya kumhukumu mtu kwa makosa aliyoyafanya na kutomhukumu kwa makosa yanayofikiriwa kwamba atayafanya, na hivyo, namtetea Magufuli dhidi ya tuhuma za makosa aanayodaiwa atayafanya mwaka 2025. Namtetea si kwa sababu ya ukabila, bali kwa sababu sipendi mtu ahukumiwe kwa makosa ya kufikirika na kudhaniwa atayafanya baadaye.

Mtu anayempinga Magufuli ni CHADEMA. Si kweli, mimi napinga hoja mbovu za serikali/Magufuli na za CHADEMA.

Mtu anayesema unamtetea Magufuli kwa sababu ya ukabila, ana wajibu wa kuonesha kwa nini unamtetea Magufuli kwa ukabila, na si kwa sababu nyingine kama mrengo wako wa kisiasa, fikra zako kifalsafa, unazi wako katika chama, daraja lako katika jamiii, dini yako, na kadhalika.
 
Hivi mtu ambaye wala huishi naye 24/7 unajuaje kuwa hali bata au anakula bata?

Kama humuoni mchana kweupe akila bata ina maana usiku wa manane hali bata?
 
Hili jambo ni rahisi sana.

But for some reason, kuna naona hawalielewi kabisa. Ni kama somo flani hivi lililo gumu.

Sijui kwa nini tu inaonekana kama vile ni somo gumu kulielewa.

Au labda wamejawa na chuki/ hisia hasi [negative feelings] kiasi kwamba chuki zao zimeghubika kabisa akili zao?

Mtu bado hajalifanya kosa. Lakini anazungumziwa kana kwamba keshalifanya.

SMH!!!
Ukikaa karibu na choo kinachotoa harufu chafu, kwa muda mrefu, pua zako zikazoea ile harufu chafu ya choo, utaona ile harufu chafu ya choo ni ya kawaida tu.

Sasa, hapo panaponuka harufu chafu ya choo, akija mtu kutoka mbali kwenye hewa safi, ambaye hajazoea harufu hiyo chafu, akasema "hapa pananuka harufu chafu ya choo", watu waliozoea harufu hiyo, wanaweza wasimuelewe, wakaona huyu anajidai.

Hii ilinitokea mwaka 1996 katika mizunguko yangu, nilifika sehemu inaitwa Muhoro, ukivuka kidogo tu mto Rufiji kuelekea kusini na Kilwa Road (is it still called Kilwa Road down there?).

Nilifika kibiashara, nilikuwa naelekea kusini zaidi. Nikakamata machalii wa Muhoro wakawa wananionesha kimji. Kimji kinanuka mavi sehemu yote, especially jioni baada ya jua kuzama for some reason. Nafikiri kuna mvuke mvuke fulani wa biomass huwa unapanda wakati ardhi inapoa baada ya kijua kupiga kwa siku nzima na kiubaridi cha usiku kuanza.

Nikamwambia mshikaji tumetoka naye Dar. Hapa pananuka mavi. Akasema usiseme hivyo out loud, wenyewe washazoea, wataona unawaletea mashauzi mtoto wa Upanga na Oysterbay.

Sasa hapa wewe ni rahisi sana kunielewa, lakini kuna watu washazoea harufu ya choo, nikiwaambia hii ni harufu chafu ya choo, hawatanielewa.

Sanasana wataona nawatukana tu.
 
Hivi mtu ambaye wala huishi naye 24/7 unajuaje kuwa hali bata au anakula bata?

Kama humuoni mchana kweupe akila bata ina maana usiku wa manane hali bata?
Ukabila! Mtu anayefahamu “absolute power corrupts absolutely”(hiyo siyo starehe) akiongea hivyo, utajiuliza maswali kama hayo endapo haufahamu.

Eti “starehe”😀🤦🏾‍♂️Mtu anayebeba maburungutu ya pesa kila anapotembea. Hiyo siyo starehe!

Ya usiku wa manane atajidai pia kuyafahamu kama yule dada mkuu kule Kisarawe(siyo starehe).
 
Hivi mtu ambaye wala huishi naye 24/7 unajuaje kuwa hali bata au anakula bata?

Kama humuoni mchana kweupe akila bata ina maana usiku wa manane hali bata?
Magufuli ni public figure.

Ni ngumu kwa yeye kwenda sehemu yoyote ile bila ku attract attention.

Unless huwa ana sneak out of Ikulu kimya kimya bila security entourage, anapanda KLM anaenda zake Amsterdam. Anapiga shopping la nguvu De Bijenkorf, anarudi tena kimya kimya.

Ni lini huyu Rais katoka hata nje ya Tanzania?

Akitoka nje ya Tanzania anaendaga Burundi na Uganda.

Ni lini kaenda Atlanta, Miami, New York na kufikia Waldorf Astoria na kukaa wiki nzima kwenye presidential suite?

Lini kaenda Davos na entourage ya watu 200 na kufikia Hotel Seehof?

Siyo lazima kuishi na mtu, tena ambaye ni public figure, ambaye ndo raia namba moja wa nchi, kujua kama he lives a lavish lifestyle.

Watu walijuaje Mobutu ni mla bata?

Teodoro Nguema Obiang mbona anajulikana ni mla bata.

Babake naye hivyo hivyo.

Hizi siyo zama za ujima.

Huwezi kuwa public figure halafu unaishi a lavish lifestyle na watu wasijue.
 
Back
Top Bottom