Hili jambo ni rahisi sana.
But for some reason, kuna naona hawalielewi kabisa. Ni kama somo flani hivi lililo gumu.
Sijui kwa nini tu inaonekana kama vile ni somo gumu kulielewa.
Au labda wamejawa na chuki/ hisia hasi [negative feelings] kiasi kwamba chuki zao zimeghubika kabisa akili zao?
Mtu bado hajalifanya kosa. Lakini anazungumziwa kana kwamba keshalifanya.
SMH!!!
Ukikaa karibu na choo kinachotoa harufu chafu, kwa muda mrefu, pua zako zikazoea ile harufu chafu ya choo, utaona ile harufu chafu ya choo ni ya kawaida tu.
Sasa, hapo panaponuka harufu chafu ya choo, akija mtu kutoka mbali kwenye hewa safi, ambaye hajazoea harufu hiyo chafu, akasema "hapa pananuka harufu chafu ya choo", watu waliozoea harufu hiyo, wanaweza wasimuelewe, wakaona huyu anajidai.
Hii ilinitokea mwaka 1996 katika mizunguko yangu, nilifika sehemu inaitwa Muhoro, ukivuka kidogo tu mto Rufiji kuelekea kusini na Kilwa Road (is it still called Kilwa Road down there?).
Nilifika kibiashara, nilikuwa naelekea kusini zaidi. Nikakamata machalii wa Muhoro wakawa wananionesha kimji. Kimji kinanuka mavi sehemu yote, especially jioni baada ya jua kuzama for some reason. Nafikiri kuna mvuke mvuke fulani wa biomass huwa unapanda wakati ardhi inapoa baada ya kijua kupiga kwa siku nzima na kiubaridi cha usiku kuanza.
Nikamwambia mshikaji tumetoka naye Dar. Hapa pananuka mavi. Akasema usiseme hivyo out loud, wenyewe washazoea, wataona unawaletea mashauzi mtoto wa Upanga na Oysterbay.
Sasa hapa wewe ni rahisi sana kunielewa, lakini kuna watu washazoea harufu ya choo, nikiwaambia hii ni harufu chafu ya choo, hawatanielewa.
Sanasana wataona nawatukana tu.