Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Kwa Watanzania hii kitu kueleweka ni ngumu sana watu wanataka mpka sherehe ndiyo kuanza kusumbuana na kadi za michango
 
Huku kwetu hata kwa baiskeli au kwa mguu watu wanatembea na sio big issue. Ndoa ni sakrament, sio show off
Nakubali lakini husindikizwa na ndugu wakishafunga ndoa na sherehe hufanyika nyumbani wakila vyakula vilivyoko hapohapo kijijini.Wakishatoka Kanisani huenda kwa miguu au baiskeli umati wa wanakijiji ndugu majirani nk wakiwasindikiza hawawi wapweke kama hao wa Kakobe
 
Uislam dini nzuri sana kwenye upande wa kuoa 😂😂😂,,, pisi 4 za kwenda ruksa kuzimiliki kwa gharama ya chupa za chai na mandazi tu.
Hatari mpka nafikilia ning'oe pisi ya hijabu hizi za vitenge vya santini ni cost sana mara ununue vitu upeleke kwa mashangazi zake wote ndiyo ubebe mke kwa hili hawataniona ,😆😆🤸🤸
 
Mbona hamkuwasindikiza kupanda daladala na bodaboda mlijificha wapi?
Kwa mfano sisi ndugu yetu kuna vikao kabla ya ndoa yao tulifanya juu ya maandalizi ya siku hiyo lakina alikataa kufanya sherehe Wala kuwachangisha watu.
Tulialikwa kuhudhuria ndoa yao kanisani lakini pia walitukaribisha jioni tukabariki nyumbani kwao.

Ndugu yangu aliondoka kwa usafiri wa uba na mkewe. Na sisi tukatawanyika kila mtu kwake.
 
Uislam dini nzuri sana kwenye upande wa kuoa 😂😂😂,,, pisi 4 za kwenda ruksa kuzimiliki kwa gharama ya chupa za chai na mandazi tu.
Ndoa za kiislamu zimerahisishwa kulingana na zenyewe zilivyo.

Kwanza ukishatoa barua tu ( Probably Tsh 30,000 ) tayari unaruhusiwa kupiga mashine hata kuzalisha au kwenda kulala kabisa kwao. Wakizingua unarudishiwa chako.

Hata ukishaoa unaweza kutoa talaka 1, ukaendekeza ubabe, ya pili tena then ujamrudia ukikumbuka goma mpaka 3 ndio mwisho.

Unaweza kuoa wengine vile vile mpaka 4.

Note: Hatpa inategemeana na hadhi ya familia unakooa.


Sasa Sisi kwetu ( siyo kidini ) ukishatoa mahari ndio kwanza demu anamibdwa kama mboni ya jicho 🤣🤣.

Na hata kishika uchumba ukishatoa ( siyo pungufu ya Tsh 100,000 ) huwa hakirudishwi hicho ukighairi.
 
Hatari mpka nafikilia ning'oe pisi ya hijabu hizi za vitenge vya santini ni cost sana mara ununue vitu upeleke kwa mashangazi zake wote ndiyo ubebe mke kwa hili hawataniona ,😆😆🤸🤸
Chukua mtoto wa hijab tu mzee. Muhimu sana huko kwenye WAX mambo ni mengi.
 
Zamani walokole tulifikiri umasikini ni sifa njema na ni ishara ya uaminifu, wakati hata kwenye biblia Abraham baba wa imani alikuwa tajiri, kufunga ndoa na kumpakia mke kwenye daladala sio sifa njema wakuu tusake pesa.
 
Kukiri kuwa kuna tatizo hakugharimu kitu.Huo uondokaji wa bila kuwasindikiza maharusi hauko sawa .Hizi picha na maelezo ya mleta mada yanajitosheleza kabisa ba yanaonyesha hali halisi ya ndoa zote 21 kuwa hakuna hata moja iliyosindikizwa kuondoka iwe na waumini iwe na ndugu iwe na marafiki au majirani

Baada ya kufunga walijiondokea kama wakiwa au yatima kwenda nakwao kuanza maisha ya upweke ya ndoa
 
Yeah, binafsi napendaga ndugu, majirani, na hata wapita njia wale ubweche mpk wabebe kwa nguo. Ni vzr ndugu washiriki furaha ya wanandoa. Kupunguza gharama huku kwetu watu huja wamefungasha vijizawadi, vyakula nk na huwa inapendeza. Hao wa Kakobe sijui watakuwa wana shida gani kama hawakupata kampani
 
ISSUE HAPA NI KUTAKA KUUFANYA UMASIKINI FASHION ZA KUJISIFIA. HICHO NDICHO NINACHOKIKATAA! SEMA SINA PESA NAPANDA DALADALA! NITAKUSIFU
Mkuu swala sio umaskini, kubwa ni mtu akubaliane na Hali yake , shida kubwa watu wanafanya shughuli kubwa kutegemea michango ya majirani na ndugu inakuwa Vita sio furaha. Ifike mahali kila mmoja afanye Jambo kulingana na kipato chake. Tusiforce vitu Kama viko nje ya uwezo.
 
Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Huwa mnahangaika sana!

Wanaojitambua siku hizi wanafunga ndoa serikalini. The process is very CLEAN and simple.

Huna haja ya kubebelea mapipa ya pilau na kualika kijiji kizima.

Funga ndoa, rudi nyumbani. Haina makelele.
 
Hawajitambui.

Na ukiona hivyo, ujue hiyo ni dalili ya kwanza ya mwanamke mpuuzi.

Atakusumbua sana!
 
Mkija kuambiwa hao ni watu waliokodiwa toka sehemu mbali mbali msije mkashtuka tu 🤣🤣
 
Ilikuwa kabla ya ujio wa barakoa!?
 
Huwa mnahangaika sana!

Wanaojitambua siku hizi wanafunga ndoa serikalini. The process is very CLEAN and simple.

Huna haja ya kubebelea mapipa ya pilau na kualika kijiji kizima.

Funga ndoa, rudi nyumbani. Haina makelele.
Watu wa aina yako tunawajua shida zao unawanyima watu sherehe ya harusi yako hakafu huyo nkeo akifariki huko ndani kelele unapiga mtaa nzima kuwa umefiwa na mjeo waje msibani wakati kwrnye harusi hukuwaalika unajifanya mtu wa principle usiyetaka kuingiliwa personal affairs zako na mkeo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…