Kwa 'body language' tu ya Mama azungumzapo huhitaji Akili Kubwa kujua ya kwamba...

Yeye mwenyewe the Late alikuwa mwizi na mjomba wake plus Bashite by then
 
Wakati ukiwa jangwani una kiu na umekata tamaa, Mungu anateremsha maji kwa njia ya ajabu kabisa.

Mungu ana maguvu sana
 
Kilicho muhimu siyo vyama vya siasa, siyo CCM, CHADEMA au ACT au chama kingine chochote BALI ni
kwa Taifa letu kuwa na viongozi wazuri na mifumo mizuri ya kiutawala.

Sina shaka kabisa Rais Samia ni kiongozi mstaarabu anayejua thamani ya utu wa mwanadamu. Anayetakbua kuwa kazi ya kiongozi ni kuwajengea mazingira watu wa makundi yote, ya kuweza kuijenga nchi yao, kuyajenga maisha yao na ya familia zao. Wananchi wana haki ya kuyafurahia maisha yao hapa Duniani kwa muda ambao Muumva wetu alitupangia alimradi hatuvunji sheria tulizozitengeneza.

Mh. Rais Samia ana uwezo wa kuliunganisha Taifa. Umoja katika Taifa letu ndiyo utakaoushinda umaskini.

Rais asisahau kujenga mifumo imara ya kiutawala ambayo italilinda Taifa dhidi ya watawala wabaya ambao wanaweza kuja kutokea hapo baadaye.

Tuachane na siasa za chuki, tumkosoe Rais wetu, tumshauri inapobidi, lakini kumpa ushirikiano ni jambo jema zaidi. Na hili livuke mipaka ya imani na ushabiki wa vyama. Taifa letu ni muhimu kuliko CCM, CHADEMA au ACT.

Mungu wetu, umjaze hekima Rais huyu mwanamke wa kwanza katika Africa Mashariki. Aongozwe na upendo wa kweli kwa Taifa lake. Ajue kuwa wanaomshangilia, wanaomsifia, wanaomkosoa, hata wanaomkejeli, wote ni watu wake.
 
Yeye mwenyewe the Late alikuwa mwizi na mjomba wake plus Bashite by then

Mjomba wake ni Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara kwa uhamisho. Bosi wake kapanda cheo ni namba bee. Khalafu unakuja na hizi hadithi. Unataka kuipa jamii taswira gani kuhusu Mh Rais wa JMT?
 
Hii kitu inafikirisha mkuu 🤔🤔🤔
 
Kujaribu kuchukua rasilimali za Tanganyika " Tanzania" kuzipeleka Zanzibar ni udwanzi
 
Hapo kanigusa sana na pia vitakuwa huru sasa, uhuru wa Habar ulipotea sana

Acha tu nilikuwa najua tangia awali ,wazanzibar wana hofu ya Mungu,hawapendi uonevu,ukiona mzanzibar chakaramu basi ujue huyo amekulia bara ila wazawa wenyewe wanapenda haki.

Mh SSH atatuongoza vizuri ila namuomba asicheke na hawa "CHAWA aka WAPIGA MAPAMBIO" watampoteza, asimamie misimamo yake aliyoonyesha kwamba macho malegevu lakini yanaona ,ukimzingua na yeye anakuzingua ,bango moja DED/RC anakwenda na maji.
 
Waliokua wanawadanganya watanzania kuwa wapinzani kazi yao ilikuwa nikupinga tu, wajiulize kwanini wanampongeza kiongozi wasasa nawakati nimwana ccm?
 
Naomba nikwambie tuu mie n muhanga wa maisha na niliathirika na transformation ya "The Magufuli effects" Ila Jambo jema nikuwa from day one kipindi anahutubia bungen siku ya kwanza Kama Rais nilimuelewa na nikajipanga katika line za maneno yake aliyokuwa anasema nilienda shambani japo kiubishi nikaumia nikarud mtaan ikawa ngumu nikatafuta kazi nikaajiriwa ikala kwangu nikarud mtaan Tena nikapata majanga maisha yakawa ngumu kama jiwe.

Ila nikaamua kubadilisha shida kuwa fursa karibu na watu wanaonizunguka TAFADHALI NAOMBA NIELEWE Tanzania Ni nchi nzuri Sana ukiwa mwaminifu na ukajituma jua wewe Ni mtaji mkubwa sana hapa Tanzania.

Sitaki kukwambia mwangalie mkuu wa mkoa wa simiyu ndugu Anthony mtaka na jiulize kwann yeye na simiyu nasio wengine na mikoa yao au hata wilaya utajifunza kitu na ANZA KUBADILIKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…