Kwa CCM kuingiza siasa kwenye taifa stars, dua langu ni kesho tuaibishwe na Morocco

Kwa CCM kuingiza siasa kwenye taifa stars, dua langu ni kesho tuaibishwe na Morocco

Inabidi viongozi wa CCM wajue kuwa Tanzania ni nchi yenye vyama vingi vya siasa, iache kuvamia kila tukio la kitaifa kuwa la CCM.

Kitendo cha kuingiza kampeni za uchaguzi 2025 kwenye kutafuta nafasi ya Kombe la Dunia 2026, sisi tusioiunga mkono CCM tutaanza kufunga na kuomba dua ili tufungwe katika michezo iliyobaki kuanzia kesho, amina.
Hii ni taifa stars ya Mama
 
Kuifunga na kuishinda Morocco, nyumbani au ugenini, ni muujiza tu. Si mchawi wa CCM (kama kina mchawi) au wa Taifa Stars (kama ina mchawi) anayeweza kuifanya Taifa stars ishinde dhidi ya Morocco. Hakuna ha haja ya kuiombea Taifa Stars sababu hakuna wakati katika historia ya dunia ambapo maombi yaliwahi kuwa mbadala wa wajibu.

Mama anunue tu tiket 30k zaidi watu wakaishangile Taifa Stars lakini kama hiyo itakuwa na maslahi ya kisiasa atakuwa anawakosea sana watanzania wapenda soccer wenye itikadi mbali mbali za kisiasa.
 
Kwaninunatakiwa kuwa mwanachama au mpenzi/shabiki wa chama gani, ili kuiunga mkono Taifa Stars? CCM na mwenyekiti wao wanaharibu sana kuingiza siasa kwenye mpira.
😀 😀 acheni kucheza mpira myoyoni na saikologikali bana,

kwahiyo ukimwona samia tu mara moja bendera ya ccm inapepea😀
 
Mpumbavu wewe, namuunga mkono SSH na sera zake lakini huwezi kuniita chawa, kwangu mimi hilo neno ni tusi.

Kesho nitaishangilia Stars kwa sababu nafsi yangu ipo hivyo sitangulizi siasa kwenye mapenzi ya timu yangu ya taifa.

Chawa at work
 
Hesabu za nini wakati kila kitu kipo wazi.

Ufisadi

Wizi

Huduma mbaya kwa jamii

Ndugu kupeana madaraka nk

CCM ya Nyerere haikufanya huo upuuzi, ila hii ccm ya sasa sio ya kushobokea kabisa hasa hii awamu ya 6.

Siwezii hama nchi ila sitashangilia staz ya ccm.
Tanzania ni hii hii moja kama unaumia sana Tafuta nauli uhamie ncho jirani, hapo maisha yataendelea kama kawaida.
 
Inabidi viongozi wa CCM wajue kuwa Tanzania ni nchi yenye vyama vingi vya siasa, iache kuvamia kila tukio la kitaifa kuwa la CCM.

Kitendo cha kuingiza kampeni za uchaguzi 2025 kwenye kutafuta nafasi ya Kombe la Dunia 2026, sisi tusioiunga mkono CCM tutaanza kufunga na kuomba dua ili tufungwe katika michezo iliyobaki kuanzia kesho, amina.
Acha kuleta visingizio Tanzania hatuna uwezo wa kuifunga moroco labda , miujiza itokee tu
 
Back
Top Bottom