Kwa CV hii ya Dkt. Mashinji simuoni wa kumfikia pale Lumumba, jamaa kapiga shule namtabiria uteuzi wa mapema


Kwahiyo unataka Kutuaminisha tena kilazima kabisa kuwa ndani ya CHADEMA na hata huku CCM alipohamia hakuna Watu ambao ama wana Elimu hiyo Kubwa na CV nzuri kuliko Yeye? Je, baada ya Kuipitia hii CV yake umeshafanya Juhudi zozote zile pia za ama Kuomba au Kutafuta CV's za wengine hasa hawa Wanasiasa? Na aliyekudanganya kuwa Kipimo sahihi cha Utendaji wa Mtu ni Elimu na CV yake pekee? Hivi waliopewa Nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania tokea Uhuru hadi hii leo hawakuwa na hizo Elimu na CV's kubwa na nzuri? Je, hizo Elimu na CV's zao zimeikomboa Tanzania na Umasikini wake na kuifanya isiwe Tegemezi kwa Maraifa makubwa ya nje? Je, hizo Elimu na CV's kubwa kama zingekuwa na Tija Rasilimali mbalimbali za Watanzania zingepotelea mikononi mwa Wajanja hasa Mataifa makubwa hasa Kiuchumi? Nitaheshimu Elimu na CV's za Waafrika ( hasa za Watanzania ) pale tu zitakapotumika kuleta Mabadiliko hasa ya Kiuchumi na Kimfumo kwa Watanzania wote kinyume na hapo bado nitaendelea tu Kuzipuuza japo Wewe unaonyesha ukisikia fulani ana Elimu kubwa na CV ya Kutisha huwa unababaika na kuwa tayari hata Kuwalamba Nyayo zao kama ukiwaona hata kabla hawajakuambia uwafanyie hivyo.
 
Akienda jela familia yake utailisha wewe bwashee?!
Kwa hiyo sababu kubwa iliyompeleka huko ni dili ya kufutiwa mashitaka katika kesi inayomkabili pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chadema, na kama ni hivyo huu ni ushahidi kuwa Mahakama inafanya kazi zake kwa maagizo toka Lumumba. Waswahili wanasema kuchamba kwingi kuondoka na mavi. Johnthepaptist unafikiri unaitetea CCM kumbe unaipaka mavi. Asante kuijuza dunia kuwa Mahakama zetu haziko huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyu ndiyo hasa ana akisi picha halisi ya utawala wa CCM mpya,yaani wanathamini makaratasi na titles za watu bila kujali uwezo wao wa kudeliver.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…