Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Cha kushangaza hata kamati ya Bunge haikumpa shinikizo la kujiuzulu.
Kamati haikumuhoji, maana hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia hatiani.
Lowassa alijitakia mwenyewe kujiuzulu.

Hana wa kumlaumu.

Yani hata kama alilazimishwa kujiuzulu, kama aliona hajafanya kosa, alitakiwa kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe kazi tujue kafukuzwa.

Ukijiuzulu tu, umekubali makosa, usitarajie kurudi.

Kurudi hapo ni kufanyiwa hisani tu.

Sasa watu wanataka kulazimisha hisani?
 
Lowassa hata hakuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu kashfa ya Richmond, hii peke yake ilionesha kutohusika kwake.. sasa Kikwete kukata jina la Lowassa lisiende kupigiwa kura ndio inayoitwa dhulma kwa wajumbe kukataliwa kumchagua mtu wanaemtaka na dhulma kwa Lowassa kwa kukataliwa nafasi ya kuweza kuchaguliwa!
 
Kama hivyo ndio ilivyokuwa Kikwete alikuwa na sababu gani kukata jina na Lowassa lisiende kupigiwa kura ? Roho ya korosho, halafu anakuja msibani bila haya anatamka kuwa marehemu bado alikuwa rafiki yake!! Jamaa ana roho ya kichawi kabisa.
Urafiki hauna uhusiano wa kupata madaraka ya uma.
Kila siku jamii inalalamika kuhusiana na jambo hilo bado kuna watu mnalilia kubebwa na marafiki.
Pambana mwenyewe kama una uwezo, acha kulilia watu.
 
Kama hakuyapenda angeyalaani, sio kukaa kimya kama alivyofanya.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Dhuluma ya kwanza kumtosa Richmond wakati ishu ilikua ya kwake.
Kutumia madaraka yake kuhakikisha lowasa hawi rais
 
Hutaki mabaya ya Kikwete yasemwe sijui kwa nini, na kila napozidi kukusoma nakuona unavyojigeuza kuwa msemaji wake, kumtetea mpaka kwa maneno yanayoonesha dhahiri umejitungia mwenyewe.

Unaposema Kikwete alikuwa na mazuri na mabaya yake, kisha hapo hapo ukaanza kumtetea kwa kumuita alikuwa "mzee wa Saigon kwenye vijiwe vya kahawa" na "mtu wa kuacha upepo upite" unajichanganya mwenyewe.

Kwasababu nilipokuonesha hayo mabaya ya wakati wa utawala wake, naona unahamishia lawama kwa wasaidizi wake, sio tena mzee wa kuacha upepo upite, unadai yeye hakutoa ruhusa, jambo ambalo ninaamini kabisa huna uhakika nalo, ni mawazo yako binafsi, na huku ndiko kujigeuza msemaji wake nakokwambia.

Na mara nyingi kufahamiana na mtu kwa karibu, automatically kunakufanya kisaikolojia uwe upande wake kumtetea bila kujua, ndicho unachofanya hapa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
πŸ€”πŸ’­πŸ”­πŸ“
 
πŸ€”πŸ€πŸ“
 
πŸ—ΌπŸ™πŸ†’
 
With RESPECT kwako, inaonekana wewe unaishi kule LALA LAND, kama hujui why Lowassa (MHSRIP)alirudi ccm, nikuache tu,kweli mkuu hujui kuwa alilazimishwa kwa kunyimwa haki yake kwa serikali ya ccm kutumia vyombo vya dola,basi wewe ni kenges
Ndugu sio lazima umtukane mwenzio, ukiwekwa hoja yako kuonyesha na kuthibitisha hoja yako inatosha kama alivyofanya wenzako! hajatukana popote!

Mahaba yasitupofushe!

Msiba utaisha, maisha yataendelea, kujukwaanika utaendelea Mkuu!
 
Mwinyi alijiuzulu kwa kashfa ya polisi kuua raia.
 
Mkuu,

Uliwahi kujua tafsiri ya push up za Magufuli jukwaani????

Umesahau kesi ya mwanaye Lowasa?

Je, stahiki zake kama waziri mkuu zilishitishwa na nani?

Aliyesema hawezi kumpa mkono mpinzani ni nani?

Aliyewafukuza kina Sofia simba uanachama ni nani?

Usitete unafiki Mkuu, tulia, acha watu waomboleze kwa amani!
 
πŸ€πŸ“πŸ†’
 
πŸ€πŸ“πŸ†’
 
Mkuu Denoo rudia kupitia andiko la Kiranga upya utaona anachosema. Hasemi Kikwete alikuwa malaika wala shetwani.

Anamaanisha Kikwete alikuwa na mazuri yake na mabaya yake! Naye Kiranga anasema kwenye zuri atasema na kwenye baya atasema, na ndivyo alivyo!

Sio kwa Kikwete tu hata kwa watu wengine, kwa kweli yupo objective kwenye hoja zake, na mara nyingi hana biasness!

Tujadili bila mahaba, tutajifunza mengi!
 
Hii nchi ina viazi wengi Sana , walitaka uraisi wa kupeana kishikaji , ?? Hii ni nchi siyo Mali ya mtu , alaf unajiuzuru Kwa makosa ya wengine , Kwa nn usiache kila mtu akapambana na Hali yake na ukweli ukajulikana , unalinda uovu wa mtu ili aje akulipe wema , duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…