Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Usijali sana nani kaandika, jibu hoja tu.

Ukianza kuangalia sana nani kaandika ndiyo mwanzo wa kufanya logical fallacy ya ad hominem.

Yani ndiyo mwanzo wa kuacha kujadili hoja iliyoletwa na kumjadili mtoa hoja kwa personal attacks.

Hoja ni kwamba umeambiwa Kikwete anazungumzwa pande zote, mabaya na mazuri yake.

Ubaya wa Watanzania wengi ni watu wa falsafa ya "all or nothing at all". No nuance.

Yani, wakimpenda mtu, wanampa mahaba yoote, hakuna kibaya watakachokiona kwake, wanamtetea kama ushabiki wa Simba na Yanga.

Na wakimchukia, wanamchukia moja kwa moja. Bila breki.

Ukiwapa watu mtihani wa kuorodhedha mazuri na mabaya ya Paul Makonda hapa, wengi wataweka mazuri tu au mabaya tu, kuweka mizani ni kiti kigumu sana kwa wengi.

Sasa tunapokuja wengine ambao tunaweza kuongea kwa nizani, siku moja Kikwete tukimtetea, siku nyingine tukimponda, kulingana na hoja, wasiompenda wengine wakiona tumemtetea wanaona huu ni ushabiki wao wa Simba na Yanga wa kila siku.

Come on man.

Some of us are more evolved than that.
🙏🤝🔊🆒
 
- Kinachojadiliwa hapa kumhusu Kikwete ni issue yake na Lowassa, hayo ya zamani wachana nayo. Nikitazama majibu yako kwa hii issue, ndio nimekwambia nakuona umejigeuza msemaji wake kwasababu majibu yako ni kama unatuaminisha kwamba Kikwete hakuwa mtu wa visasi, yeye anaujua na kuupenda utani wa vijiweni.

Wakati kiuhalisia nimekuwekea yaliyotokea enzi za utawala wake, ukabadilika, ukahamishia lawama kwa wasaidizi wake, nikakuuliza tena, kama hakuwa mtu mbaya kwanini hakujitokeza kuwakemea hao wasaidizi wake wakati wa awamu yake, sikuona jibu lako.

- Nashangaa hapa unaniuliza swali dogo namna hiyo!, kwamba hukujua uliposema Kikwete alikuwa mtu wa "Saigon" na "kuacha upepo upite" hukuwa unamtetea?, hukujua kama kwa kusema kwako hivyo, ulituonesha tabia za Kikwete kwamba ni mtu asiyejali maneno ya watu? mpaka pale nilipokuonesha vile maneno ya wengine yalivyomkera akawaumiza wakati wa utawala wake?!

Hata kama ulitoa mfano mmoja wa case ya Melo, lakini nami nikakujibu kwa kukupa mifano yangu inayoonesha Kikwete alikuwa tofauti, hakuwa mtu wa kupuuza maneno kama unavyotuaminisha hapa, wakati mwingine alikuwa akijibu kwa vitendo.

-Hili la wewe mara zote ulipoitwa kwa balozi ukaonane na Kikwete ulikataa, ukweli unaujua mwenyewe, lakini haufiti wala kufubaza yote niliyokuandikia hapo juu. I rest my case.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
1. Zamani ni lini? Unawezaje kuongelea mambo ya Kikwete na Lowassa bila kuzungumzia mambo ya zamani wakati hawa watu wana historia kutoka Chuo Kikuu?

Kwani mtu akiwa anaujua utani wa vijiweni ndiyo maana yake hana visasi? Unaelewa kuwa mtu mwenye kifua cha kuweka maneno anaweza pia kuwa mtu wa visasi sana tu? Akawa mtu wa kufuata maneno ya Shakespeare "revenge is a dish best served cold". Yani mtu anayatunza maneno miaka na miaka, anakuchekea tu, halafu siku hujategemea kabisa anakupiga daflao. Unaujua huo msemo wa "revenge is a dish best served cold"?

Mbona unasoma kitu ambacho mimi sikuandika?

Mimi nimeandika "Kikwete ana kifua cha kuweka maneno" wewe unasoma "Kikwete hana visasi". Where do you get this?

Unasoma ninayoandika au unayotaka niandike ambayo sijaandika?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Huzo habari za wasaidizi wake nimekwambia siwezi kumtetea Kikwete pote, kwa sababu pengine aliona anapata political advantage na political expediency akapafumbia macho.

Kwa nini unazing'ang'ania bado? Unataka niwe ninesema namtetea Kikwete kwenye kila kitu wakati sijasema hivyo?

Mkuu, unajua kusoma? Unasoma ninayokujibu?

Nishakwambia Kikwete siwezi kumtetea huko, kwa nini unataka kufanya kama bado nataks kumtetea?

Una matatizo ya kisaikolojia kwenye kichwa chako yanayokufanya ushindwe kusoma vizuri ninayoandika?

Nimeshakwambia "Hapa kwa kweli siwezi kumtetea Kikwete. Kqa sababu mengine hakuyakemea, inaonekana yalimoa faida ya kisiasa ndiyo maana hakuyakemea". Halafu bado unaniandama kwa kumtetea Kikwete?

Una matatizo gani wewe?

Mimi nikisema "Huyu Kikwete ni kiongozi asiyejali maneno ya watu" ni kumsifia? How? Kiongozi kutojali maneno ya watu ni kukwepa wajibu wake, ni dharau, ni kuwa kichwa ngunu, ni kukosa unyenyekevu, ni kutowapa wananchi haki yao ya kusikilizwa. Wewe unaonaje mimi kusema kiongizi hasikikizi maneno ya watu kuwa namsifia?

Again, unajua kusoma? Una matatizo gani?

You rest your case? Which case? You don't have one.
 
Na pia kuna kujiuzulu ili kumnusuru Bosi na maswahiba!

Rais H.A. Mwinyi wa Zanzibar ameeleza, alimwandikia Rais Kikwete barua ya kujiuzulu uwaziri wa Ulinzi kutokana na milipuko ya Mabomu, na ilitokea mara mbili. Rais Kikwete alimkatalia kujiuzulu.

Kuhusu ENLowassa
Rais Kikwete alikuwa na uwezo wa kuita 'caucus' ya Chama chake kulijadili suala
Kikwete alikuwa na option ya kutishia kulivunja au kulivunja Bunge kama litamwandama Waziri mkuu wake
Rais Kikwete akiwa sehemu ya Bunge angeomba kwenda kulihutubia Bunge kwa kadhia hiyo.

Rais Kikwete hakufanya jitihada zozote na kumwacha ENL akikaangwa na Bunge.

Hapa simaanishi kwamba kulikuwa na makosa kumkaanga, la hasha lakini ni ukweli kwamba 'rafiki yake ' hakumsaidia. Pengine Kikwete alijua huo ndio utakuwa mwisho wa ushawishi wa ENL katika siasa za Tanzania

Lowassa alibaki na machaguo mawili, kwanza, akomae kutojiuzulu, Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani.
Kuondolewa kwa 'vote of no confidence' kungehitimisha ndoto na safari yake kisiasa once and for all

Pili, ajiuzulu kama sehemu ya kuwajibika na kuinusuru serikali ili apate nafasi mbele ya safari.
Hii ilikuwa '' viable option'' na tumeona ilimsaidia kurudia katika ulingo kwa mara nyingine akiwa na nguvu kubwa.

Kwanini Kikwete analaumiwa? Si kwasababu hakumpa mshirika wake Urais.

JK analaumiwa kwa mambo mawili, kwanza kumtosha ENL wakati alijua mafisadi walivyosaidia mtandao uliomweka madarakani. Kama Rais wa nchi , JK alijua mauza uza ya Richmond na walioko nyuma yake! alijua!

Pili, ENL alijijenga tena baada ya anguko la Uwaziri mkuu. Utaratibu wa chama ni majina kupitiwa na lenye kura nyingi linasonga mbele kwa mchujo zaidi. JK alijua ushawishi wa Lowassa.

Kwa kujua Lowassa hana Kikwakzo na ameshinda kwa uhalali na kwa kujua mbinu za kumzuia kwa kumuanguasha u-P,M zimeshindwa, JK akakata jina la Lowassa si kwa kushindwa bali kwa hiyana tena kinyuma na taratibu za upatikanaji wa mgombea.

Kikwete hakumdhulum Urais , alimdhulumu Lowassa kwa kuvunja taratibu zilizokuwa zinapeleka jina na Lowassa mbele. Alikata jina, Lowassa hakushindwa! hiyo ni dhuluma inayoongelewa
Kulikuwa na ulazima gani Lowasa awe Rais?

Lowasa alishakuwa na kashfa za uwizi ,CCM walikuwa wanalinda brand ...It was a technical trick..

lowasa analazimisha mpaka akaenda upinzani yeye ndio mweny tamaa acheni unafiki...Shule za kata mlimsifu kwa vile alikuwa waziri mkuu wala idea ilikuwa sio yake ila Escrow mnadai kasingiziwa wakati alikuwa waziri mkuu 😅😅😅.

Lowasa ndio msaliti kwa tamaa za uongozi mtu anaapa lazima awe Rais kabla ya kufa mbona kafa bila ya kuwa Rais😁😁

Lowasa ndio msaliti mkuwa mpaka kumpa pesa Mbowe ili agombee CDM...lowasa ,Membe na Mbowe ndio wasaliti wakubwa kutokea.
 
Na pia kuna kujiuzulu ili kumnusuru Bosi na maswahiba!

Rais H.A. Mwinyi wa Zanzibar ameeleza, alimwandikia Rais Kikwete barua ya kujiuzulu uwaziri wa Ulinzi kutokana na milipuko ya Mabomu, na ilitokea mara mbili. Rais Kikwete alimkatalia kujiuzulu.

Kuhusu ENLowassa
Rais Kikwete alikuwa na uwezo wa kuita 'caucus' ya Chama chake kulijadili suala
Kikwete alikuwa na option ya kutishia kulivunja au kulivunja Bunge kama litamwandama Waziri mkuu wake
Rais Kikwete akiwa sehemu ya Bunge angeomba kwenda kulihutubia Bunge kwa kadhia hiyo.

Rais Kikwete hakufanya jitihada zozote na kumwacha ENL akikaangwa na Bunge.

Hapa simaanishi kwamba kulikuwa na makosa kumkaanga, la hasha lakini ni ukweli kwamba 'rafiki yake ' hakumsaidia. Pengine Kikwete alijua huo ndio utakuwa mwisho wa ushawishi wa ENL katika siasa za Tanzania

Lowassa alibaki na machaguo mawili, kwanza, akomae kutojiuzulu, Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani.
Kuondolewa kwa 'vote of no confidence' kungehitimisha ndoto na safari yake kisiasa once and for all

Pili, ajiuzulu kama sehemu ya kuwajibika na kuinusuru serikali ili apate nafasi mbele ya safari.
Hii ilikuwa '' viable option'' na tumeona ilimsaidia kurudia katika ulingo kwa mara nyingine akiwa na nguvu kubwa.

Kwanini Kikwete analaumiwa? Si kwasababu hakumpa mshirika wake Urais.

JK analaumiwa kwa mambo mawili, kwanza kumtosha ENL wakati alijua mafisadi walivyosaidia mtandao uliomweka madarakani. Kama Rais wa nchi , JK alijua mauza uza ya Richmond na walioko nyuma yake! alijua!

Pili, ENL alijijenga tena baada ya anguko la Uwaziri mkuu. Utaratibu wa chama ni majina kupitiwa na lenye kura nyingi linasonga mbele kwa mchujo zaidi. JK alijua ushawishi wa Lowassa.

Kwa kujua Lowassa hana Kikwakzo na ameshinda kwa uhalali na kwa kujua mbinu za kumzuia kwa kumuanguasha u-P,M zimeshindwa, JK akakata jina la Lowassa si kwa kushindwa bali kwa hiyana tena kinyuma na taratibu za upatikanaji wa mgombea.

Kikwete hakumdhulum Urais , alimdhulumu Lowassa kwa kuvunja taratibu zilizokuwa zinapeleka jina na Lowassa mbele. Alikata jina, Lowassa hakushindwa! hiyo ni dhuluma inayoongelewa

Barua ya kujiuzulu kumnusuru bosi na maswahiba utaiandikaje?

Hata ukisema "mimi sina makosa, ila najiuzulu kwa kuinusuru serikali kutoka kwenye matatizo yanayohusiana na mimi kuwapo serikalini" tayari unanuka, tayari umejiweka katika matatizo ya kukufanya uwe untenable. Kuna calculations fulani umekosea hapo.

Bismarck said Politics is tge art of the possible.

Caesar's wife must be above suspicion.

Kuhusu Kikwete.

Kwanza kabisa mna uhakika gani Kikwete alikata jina la Lowassa? Kwa uamuzi wake tu. Hizi habari zina uhakiki gani? Was Kijwete realky that powerful?

Pili,

Chama kinapeleka vipi mbele jina la mtu aliyejiuzulu kwa kashfa kubwa ya rushwa na kutoa angalau optics kwamba ama ameshiriki moja kwa moja katika hiyo rushwa, ama ameshindea kusimamaia wizara rushwa hiyo isitokee?

Yani chama badala ya kujikita kwenye ilani na kampeni, kianze kumsafisha mgombea na ku explain kwa nini mgombea alijiuzulu, huku wapinzani wakimpiga mawe kwamba huyu ni mla rushwa aliwahi mpaka kujiuzulu kwa rushwa?

Kwa nini chama kichague mgombea huyo wakati kina wagombea wengine ambao hawana wingu hilo la kashfa ya rushwa na wanaweza kuanza kampeni moja kwa moja bila kuhitaji kusafishwa?
 
..
20240213_044014.jpg
 
Kulikuwa na ulazima gani Lowasa awe Rais?

Lowasa alishakuwa na kashfa za uwizi ,CCM walikuwa wanalinda brand ...It was a technical trick..

lowasa analazimisha mpaka akaenda upinzani yeye ndio mweny tamaa acheni unafiki...
Lowasa ndio msaliti kwa tamaa za uongozi mtu anaapa lazima awe Rais kabla ya kufa mbona kafa bila ya kuwa Rais😁😁
Lowasa ndio msaliti mkuwa mpaka kumpa pesa Mbowe ili agombee CDM...lowasa ,Membe na Mbowe ndio wasaliti wakubwa kutokea.
Rudi ukasome bandiko kwa utulivu utapata majibu ya kila neno lako hapo juu.

FYI nimeandika wazi, ENL hakudhulimiwa Urais. Ngoyai alidhulumiwa taratibu ambazo alishinda
Wajumbe ndio walliopaswa kuamua hatma yake, kukatwa jina ni kukiuka taratibu

CCM walijua amechukua Form. Ikiwa walijua ni Fisadi wangetumia kanuni kumzuia hata asichukue Form.

Kumwacha achukue halafu kuondoa jina kwasababu alikuwa ana ushawishi ni kumdhulumu.
 
Hoja ni kwaajili ya wenye akili timamu, siyo wewe.

Hakuna mahali iliposemwa kuwa Urais ilikuwa ni haki yake Lowasa bali kama umechaguliwa na wananchi, ni haki ya wananchi kuongozwa na mtu waliyemchagua.

Juzi umemsikia Prof. Tibaijuka akisema kwamba alimwambia Lowasa kuwa akigombea kuoitia chama kingine tofauti na CCM kwa mifumo ya nchi ilivyo, hatatangazwa kuwa Rais. Na ndicho alichokifanya Kikwete.
Yule alishakuwa na kashfa CCM sio wajinga ila wanatawala wajina..

Tamaa gani kaonyesha Lowasa kisa cha pesa kwenda kuhonga ndugu yake wa kaskazini ili agombee kule ....Punguzeni ujinga lowasa hakupangwa kuwa Rais wa Tanzania hamuwezi kupingana wala Mbowe hawezi kuwa Rais ,hivyo ndio mambo yalivyo.

Mnaangalia kikwete wakati alikatwa kulinda brand mtu ana kesi kibao japo sio uhakika...Unamsikiliza pro Tibaijuka ambaye ni wale wale wenye kesu za wizi .

Lowasa alikuwa na tamaa za madaraka ndio maana kafeli ,acheni unafiki semeni ukweli kulikuwa na haja gani kwenda upinzani na Mbowe kumsapot kisa kanda yao ili awe Rais ...Jamaa yenu alikuwa mzuri ila alitaka kutumia pesa awe Rais kwa lazima jambo ambalo haliwezekani ..

Baadae karudi CCM what a hypocrisy ?mnatetea tu ujinga huyo Tibaijuka ana kesi kibao kiburi cha kujiona hana lolote alikuwa CCM ila mda ushamtupa mkono.
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Umeandika kwa uchungu usiomithilika,hakika Lowassa alishinda urais ni imani yangu pia na kwenye mtandao wa X Tibaijuka amesema jambo ambalo ni uhalisia "mfumo".
 
Rudi ukasome bandiko kwa utulivu utapata majibu ya kila neno lako hapo juu.

FYI nimeandika wazi, ENL hakudhulimiwa Urais. Ngoyai alidhulumiwa taratibu ambazo alishinda
Wajumbe ndio walliopaswa kuamua hatma yake, kukatwa jina ni kukiuka taratibu

CCM walijua amechukua Form. Ikiwa walijua ni Fisadi wangetumia kanuni kumzuia hata asichukue Form.

Kumwacha achukue halafu kuondoa jina kwasababu alikuwa ana ushawishi ni kumdhulumu.
Kukatwa kwa EL kulituletea majanga watz tukaongozwa na mshamba wa madaraka kwa kivuli cha uzalendo
 
Usijali sana nani kaandika, jibu hoja tu.

Ukianza kuangalia sana nani kaandika ndiyo mwanzo wa kufanya logical fallacy ya ad hominem.

Yani ndiyo mwanzo wa kuacha kujadili hoja iliyoletwa na kumjadili mtoa hoja kwa personal attacks.

Hoja ni kwamba umeambiwa Kikwete anazungumzwa pande zote, mabaya na mazuri yake.

Ubaya wa Watanzania wengi ni watu wa falsafa ya "all or nothing at all". No nuance.

Yani, wakimpenda mtu, wanampa mahaba yoote, hakuna kibaya watakachokiona kwake, wanamtetea kama ushabiki wa Simba na Yanga.

Na wakimchukia, wanamchukia moja kwa moja. Bila breki.

Ukiwapa watu mtihani wa kuorodhedha mazuri na mabaya ya Paul Makonda hapa, wengi wataweka mazuri tu au mabaya tu, kuweka mizani ni kitu kigumu sana kwa wengi.

Sasa tunapokuja wengine ambao tunaweza kuongea kwa nizani, siku moja Kikwete tukimtetea, siku nyingine tukimponda, kulingana na hoja, wasiompenda wengine wakiona tumemtetea wanaona huu ni ushabiki wao wa Simba na Yanga wa kila siku.

Come on man.

Some of us are more evolved than that.
Wala sina tatizo nae huyo, kama ana hoja yake aje nayo nipo nitamjibu, lakini kutumia hoja zako kunijibu mimi bila kujua wapi tumeanzia na kipi kilinifanya nikakujibu vile, namuona kama aliyedandia treni kwa mbele.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Bora Lowasa lakini alichomfanyia SALIM A SALIM ni Zaid Alimuita muislam mwenye misimamo mikali hafai kupewa nchi akamalizia kuwa SALIM ni Hizbu
Binafsi naona dhulma aliyomfanyia EL haimithiliki,kimsingi kufanya deal na mswahili wapaswa kua makini,waswahili wana hulka ya unafiki
 
1. Zamani ni lini? Unawezaje kuongelea mambo ya Kikwete na Lowassa bila kuzungumzia mambo ya zamani wakati hawa watu wana historia kutoka Chuo Kikuu?

Kwani mtu akiwa anaujua utani wa vijiweni ndiyo maana yake hana visasi? Unaelewa kuwa mtu mwenye kifua cha kuweka maneno anaweza pia kuwa mtu wa visasi sana tu? Akawa mtu wa kufuata maneno ya Shakespeare "revenge is a dish best served cold". Yani mtu anayatunza maneno miaka na miaka, anakuchekea tu, halafu siku hujategemea kabisa anakupiga daflao. Unaujua huo msemo wa "revenge is a dish best served cold"?

Mbona unasoma kitu ambacho mimi sikuandika?

Mimi nimeandika "Kikwete ana kifua cha kuweka maneno" wewe unasoma "Kikwete hana visasi". Where do you get this?

Unasoma ninayoandika au unayotaka niandike ambayo sijaandika?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Huzo habari za wasaidizi wake nimekwambia siwezi kumtetea Kikwete pote, kwa sababu pengine aliona anapata political advantage na political expediency akapafumbia macho.

Kwa nini unazing'ang'ania bado? Unataka niwe ninesema namtetea Kikwete kwenye kila kitu wakati sijasema hivyo?

Mkuu, unajua kusoma? Unasoma ninayokujibu?

Nishakwambia Kikwete siwezi kumtetea huko, kwa nini unataka kufanya kama bado nataks kumtetea?

Una matatizo ya kisaikolojia kwenye kichwa chako yanayokufanya ushindwe kusoma vizuri ninayoandika?

Nimeshakwambia "Hapa kwa kweli siwezi kumtetea Kikwete. Kqa sababu mengine hakuyakemea, inaonekana yalimoa faida ya kisiasa ndiyo maana hakuyakemea". Halafu bado unaniandama kwa kumtetea Kikwete?

Una matatizo gani wewe?

Mimi nikisema "Huyu Kikwete ni kiongozi asiyejali maneno ya watu" ni kumsifia? How? Kiongozi kutojali maneno ya watu ni kukwepa wajibu wake, ni dharau, ni kuwa kichwa ngunu, ni kukosa unyenyekevu, ni kutowapa wananchi haki yao ya kusikilizwa. Wewe unaonaje mimi kusema kiongizi hasikikizi maneno ya watu kuwa namsifia?

Again, unajua kusoma? Una matatizo gani?

You rest your case? Which case? You don't have one.
Ume panic. I repeat; I rest my case.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
W
Yule alishakuwa na kashfa CCM sio wajinga ila wanatawala wajina..

Tamaa gani kaonyesha Lowasa kisa cha pesa kwenda kuhonga ndugu yake wa kaskazini ili agombee kule ....Punguzeni ujinga lowasa hakupangwa kuwa Rais wa Tanzania hamuwezi kupingana wala Mbowe hawezi kuwa Rais ,hivyo ndio mambo yalivyo.

Mnaangalia kikwete wakati alikatwa kulinda brand mtu ana kesi kibao japo sio uhakika...Unamsikiliza pro Tibaijuka ambaye ni wale wale wenye kesu za wizi .

Lowasa alikuwa na tamaa za madaraka ndio maana kafeli ,acheni unafiki semeni ukweli kulikuwa na haja gani kwenda upinzani na Mbowe kumsapot kisa kanda yao ili awe Rais ...Jamaa yenu alikuwa mzuri ila alitaka kutumia pesa awe Rais kwa lazima jambo ambalo haliwezekani ..

Baadae karudi CCM what a hypocrisy ?mnatetea tu ujinga huyo Tibaijuka ana kesi kibao kiburi cha kujiona hana lolote alikuwa CCM ila mda ushamtupa mkono.
Watu mliofilisika kifikra ndio mnaowaza masuala ya ukanda na ukabila,nchi hii watu wa kaskazini mnatuchukuliaje eti!?.
 
Ume panic. I repeat; I rest my case.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Kupanic ni nini? Unahakikishaje hapa mtu ka panic na hapa anaandika kwa passion tu hajapanic?

Unajuaje wewe unapoona mtu ka panic, mwenzako hajapiga chafya tu kwa reflex action ila wewe nyoronyoro unaona amepanic?

Nimepanic vipi, wapi, kwa sababu gani, unajuaje nimepanic na si wewe uliye panic kusema nime panic?

How do you know you meet the requisite wattage to make me panic and that you are not just flattering yourself by thinking that you could make me panic?

Tutajuaje kuwa hutumii gia ya kuniambia "umepanic" kukimbia mazungumzo haya na kukimbia kujibu hoja na maswali nilliyoyaleta?

Mtu yeyote anayetaka kukimbia maswali anaweza kusema "Umepanic". Kwa nini tusikuchukulie kama mtu anayekimbia maswali kwa gia ya kusema "umepanic"?

You rest your case? Do you even know what a case is?
 
W

Watu mliofilisika kifikra ndio mnaowaza masuala ya ukanda na ukabila,nchi hii watu wa kaskazini mnatuchukuliaje eti!?.
Kama ulivyokuwa bogus angali huko juu umeandika nn?

Eti kaskazini mnamsapot Lowasa kuhusu kutoa Rais sio leo mkajipange🤣🤣🤣🤣...Yaani mtu atoke CCM siku mbili halafu mumpe nafasi ya kugombea kisa ndugu yenu baada ya Mbowe kuhongwa.

Hatuwezi kuongozwa na watu wa hovyo ,matapeli hawana utu ,wezi, wana tamaa za mali

Mpaka kafa hajawa Rais tambua CCM ndio ilimpa nguvu ila sio yeye na usaliti wake...Kama CCM wangetaka angekuwa Rais hilo kalitambua kabla hajafa ndio maana alirudi..

Eti pesa 🤣
 
Back
Top Bottom