Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Rais A.H Mwinyi alipoandika barua kutokana na mauaji ya Watu hakuwa na kosa. Mwinyi hakuagiza wala hakuwa na ufahamu wa kilichotokea. Katika kuonyesha kwamba serikali inajali alijiuzulu.Barua ya kujiuzuku kumnusuru bosi na maswahiba utaiandikaje?
Kujiuzulu kwa mwinyi kulimuondolea Rais mzigo kwasababu kinyume chake ingalikuwa tabu.
Barua inaandikwaje? Soma barua ya A.H. Ipo mtandaoni.
Hapana , ndiyo maana A.H. Mwinyi alirudi na kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania chini ya Uongozi ulioshuhudia anguko lake. Timu nzima ya kupitisha majina akiwemo RC wa Shinyanga Peter Kisumo ilikuwa ile ile.Hata ukisema "mimi sina makosa, ila najiuzulu kwa kuinusuru serikali kutoka kwenye matatizo yanayohusiana na mimi kuwapo serikalini" tayari unanuka, tayari umejiweka katika matatizo ya kukufanya uwe untenable. Kuna calculations fulani umekosea hapo.
Walijua hakutenda, aliwajibika.
I agreedCaesar's wife must be above suspicion.
Kuna habari kutoka kwa 'privy' na mtando mzima. Kumbuka mtandao ulikuwa na watu wengiKuhusu Kikwete.
Kwanza kabisa mna uhakika gani Kikwete alikata jina la Lowassa? Kwa uamuzi wake tu. Hizi habari zina uhakiki gani? Was Kijwete realky that powerful?
Habari zinatoka ''horse's mouth'
Kuna circumstancial evidence pia kuhusu nguvu ya Kikwete
Rais SSH anasema wakati wanachagua nani awe VP baada ya Magufuli kuteuliwa, kamati kuu iliitwa.
Rais Samia anasema, ''sisi tulikaa nje tukinywa chai na biskuti wakati vingunge wameingia na kujifungia' Vingunge si Kamati kuu ni JK na watu wachache sana. Maana yake ni kwamna hata CC haikuwa na nguvu
Pili, unakumbuka ' ...Tunaimani na Lowassa''. Ilikuwa dhahiri wajumbe wa NEC walikuwa na taarifa za nini kimetoke.
Magufuli akathibitisha kwa kusema ''.... walioimba ningewatimua siku hiyo' akionyesha nguvu ya Mwenyekiti.
Tatu, mwaka 1995 Mkapa alipomshinda JK, ilisemwa kura ''hazikutosha'. hii ilikuwa lugha laini tu, tunajua Mwenyekiti wakati huo akiwa na Nyerere walimtaka Mkapa. Unaweza kuona nguvu ya Mwenyekiti kama Kikwete
Nne, Mkapa anathibitisha alitumwa na Nyerere kwenda kwa mzee Kitwana Kondo. Nyerere ndiye alimshawishi achukue Form, tunajua the rest is history
Hapa ndipo pana hoja nzuri sana. Suala ninaloongelea si kukubalika au kutokubalika kwa Lowassa.Pili,
Chama kinapeleka vipi mbele jina la mtu aliyejiuzulu kwa kashfa kubwa ya rushwa na kutoa angalau optics kwamba ama ameshiriki moja kwa moja katika hiyo rushwa, ama ameshindea kusimamaia wizara rushwa hiyo isitokee?
Yani chama badala ya kujikita kwenye ilani na kampeni, kianze kumsafisha mgombea na ku explain kwa nini mgombea alijiuzulu, huku wapinzani wakimpiga mawe kwamba huyu ni mla rushwa aliwahi mpaka kujiuzulu kwa rushwa?
Kwa nini chama kichague mgombea huyo wakati kina wagombea wengine ambao hawana wingu hilo la kashfa ya rushwa na wanaweza kuanza kampeni moja kwa moja bila kuhitaji kusafishwa?
Wala siongelei na sikubali kuwa alidhulumiwa Urais.
Ninachosema hapa ni kwamba alidhulumiwa taratibu. Chama kina sifa za mgombea na zinajulikana.
Ikiwa ENL alikuwa hana sifa, Chama kilimpa vipi Form ya kugombea? Chama kiliridhika alikuwa na sifa!
Pili, taratibu zinasema mwenye kura nyingi atasonga mbele. Iwe Kikwete au kundi lote liliondoa jina lake si kwa kukosa kura bali kwa fikra zao, hiyo ni dhuluma. Kikwete au kundi hilo wangemzuia kwa kukosa sifa, na kwa kukosa kura. Kukata jina lake kwa utashi na si taratibu ni dhuluma
Nipo kwenye rekodi, sijawahi kumkubali ENL na hata juzi niliandika machache mazuri na mengi mabaya yake.
Hata hivyo hatuwezi kuacha kusema dhulma aliyofanyiwa! na katikati ya dhulma yupo Kikwete in so many ways.