Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani


Hoja zangu ni kwaajili ya watu wenye akili timamu, upeo mpana na wakweli wa nafsi. Wewe haikuhusu.
 
Ingekuwa ni dhulma wala asingeiacha Chadema na kurudi tena kule CCM kirahisi.
 
kwahiyo tunakubaliana kuwa marehemu alikuwa miongoni mwa mafisadi na kaonewa na mafisadi wenzie katika harakati zao za kutaka kupeana vyeo ili wapate kuongeza mianya ya kufanya ufisadi zaidi...so marehemu hapaswi kuonewa huruma,wakuonewa huruma mwananchi ambaye alitegemea baada ya marehemu kujiuzulu labda angechukuliwa hatua au kutaifishwa baadhi ya mali zake kulingana na ufisadi alioufanya...unakumbuka yale malipo ya milioni 150+ kwa siku?
 
Hilo bwege we hujalizoea? Amejiconfuse mwenyewe. Eti CHADEMA ndiyo inamtegemea km mshauri wao?

Nni lini nilikuwa mshauri wa CHADEMA?

Unachotakiwa kufahamu ni kuwa, hakuna hata kiongpzi mmoja wa CHADEMA wa ngazi ya Taifa anayenifahamu au ambaye amewahi kukutana nami ana kwa ana.

Sijawahi kuwa mshauri wala kiongozi wa chama chochote cha siasa. Nimewahi kutana ana kwa ana na Lowasa RIP, niliwahi kuongea kwa simu na Magufuli RIP kabla hajawa Rais, niliwahi kukutana na Mwalimu Nyerere na kushikwa mkono nikiwa chipukizi. Zaidi ya hawa, nao ilikuwa ni matukio ya mara moja, na siyo uhusiano wa karibu, sijawahi kuwa karibu kiasi cha kuweza kuwa mshauri wa kiongozi wa chama chochote cha siasa. Naendelea kuwa mtaalam mshauri wa taasisi mbalimbali za nje kwenye fani yangu, lakini siyo siasa wala siyo uongozi. Hivyo kudai kuwa eti CHADEMA inanitegemea kama mshauri wa chama, ni uwongo mkubwa, labda kama ni ushauri wa kupitia haya maandiko ya JF.
 
A good analysis.
 
Ingekuwa ni dhulma wala asingeiacha Chadema na kurudi tena kule CCM kirahisi.

Naamini kuwa Lowasa maisha yake yote alikuwa ni mwanaTANU na baadaye mwanaCCM. Alienda CHADEMA ili agombee Urais akijua ana watu wengi waliokuwa wakimwunga mkono, hasa ndani ya CCM.

Alijua wazi kuwa jina lake halikukatwa na CCM bali maadui zake wenye nguvu ndani ya CCM, ambao walikuwa wanajulikana na wanahesabika.
 
Hata JK kwenda Dodoma na majina matano na Lowassa kutokuwepo ni mpango wa Mungu pia, labda hujui namna Mungu anavyofanya kazi kupitia sisi katika maisha yetu ya kila siku.

Hujawahi kusikia hadithi mbalimbali za namna Mungu anavyowaokoa watu wanaotaka kusafiri na ndege wanakutana na vikwazo mbalimbali kutoka kwa familia zao wenyewe halafu baada ya ndege kuanguka ndio wanaanza kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa na kifo?.

Baadhi ya watu walikwepa kifo siku ile ya September 11 kule New York wakiwa wamekwenda kwanza kuwaacha shuleni watoto wao saa mbili asubuhi na wakati ndege ya kwanza inalipuka saa mbli na dakika 48 asubuhi walikuwa bado wapo njiani wakienda ofisini, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.

Apumzike kwa amani Lowassa, amefanya mengi lakini hakuna sababu ya kuhuzunika kuukosa Urais, hii ni nchi yenye watu milion 63 haupo uwezekano kila mwenye ndoto za kuingia ikulu aje siku moja aitimize ndoto yake hiyo.
 
Alita
CCM gani wewe unayoizungumzia? Hiyo ambayo wajumbe wengi wakiwemo kina Nchimbi, Sophia Simba, Kimbisa, Bashe, Musukuma n.k walifura hadi kuanza kuimba wana imani na Lowassa baada ya kutoliona jina lake??

Haijalishi ishu ilikuwa kweli au laah ,hata watu hawana uhakika kama Lowasa alihusika ila alishakuwa na shutuma watu wengi walikuwa wanajua ameiba.


Kumuweke Magufuli ni trick mpya kwa vile hakuwa na kashfa kwa sana , Magufuli sio mkamilifu ila angalau alikuwa anajulikana kwa utendaji kazi wake .

CCM ni kubwa kuliko Lowasa na hakuna ugomvi wa Lowasa na CCM mpaka anakufa .
 
Kila mahala mitandaoni watu wanajadili usaliti wa Kikwete, na kama vile wanamsuta na kumsonkora kwa kimsaliti rafiki yake mkubwa, Edward Lowassa.

Usaliti si mzuri
 
Katika watu walio yumbisha taifa ni huyu Mzee Kikwete, ni Jambazi sugu limejificha kwenye kichaka cha Urais mstaafu, mauji mengi ya wanasiasa ana kwa njia moja au nyingine, mnafiki ni balaa, lakini wananchi wamesha mshitukia
 
Kwenye siasa mambo ya kusalitiana ni kawaida na wanasiasa wanalijua hilo, Kinachofanya watu wamkosoe JK sio usaliti ni unafiki anaouonyesha na sio JK tu viongozi wengi wanaonyesha unafiki ila JK amekuwa # 1 on trending kwa sababu ya tukio la 2015.
All in all ....WANASIASA PUNGUZENI UNAFIKI HAYA MNAYOFANYA KWA EL NA NYIE MTAFANYIWA SIKU MUNGU AKIWAPENDA ZAIDI.
 
Kumuweke Magufuli ni trick mpya kwa vile hakuwa na kashfa kwa sana , Magufuli sio mkamilifu ila angalau alikuwa anajulikana kwa utendaji kazi wake .
Hakuna trick yoyote, hiyo ni bahati ya mtende tu ilimdondokea jiwe, njia zote zilikuwa zimechorwa kuelekea kwa jasusi wa Rondo. Wajumbe waliomuweka ENL moyoni ndio walioamua kama wenzao jikoni wamemwaga mboga basi wao bora wamwage ugali tu wote wakose walale njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…