Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge. Nilivyosoma tu hii sehemu niliangalia ID, hivi we lini utakuja kuwa na akili? We ni bure kabisa, umeshajichanganya mwenyewe na kuanza uzushi km ulivyo siku zote. Kweli mwongo n i mwongo tu na tabia haina dawa. Acha uzushi na uwongo havina posho

Hoja zangu ni kwaajili ya watu wenye akili timamu, upeo mpana na wakweli wa nafsi. Wewe haikuhusu.
 
Lowassa hata hakuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu kashfa ya Richmond, hii peke yake ilionesha kutohusika kwake.. sasa Kikwete kukata jina la Lowassa lisiende kupigiwa kura ndio inayoitwa dhulma kwa wajumbe kukataliwa kumchagua mtu wanaemtaka na dhulma kwa Lowassa kwa kukataliwa nafasi ya kuweza kuchaguliwa!
Ingekuwa ni dhulma wala asingeiacha Chadema na kurudi tena kule CCM kirahisi.
 
Kaka, mafisadi ni wengi mnoo ndani ya CCM, wengi mnooo. Ila ilibidi EL achafuliwe kwa makusudi ili mambo 'yao' yaende. TIS ni ufisadi, madini kuna ufisadi, madawa, MSD, kuna ufisadi, Sukari ufisadi, Mafuta ya kula na ya mitambo ufisadi, ufisadi umeota mizizi ndani ya CCM, ila EL amefanywa alama ya taifa ya ufisadi! TANAPA na TANESCO kuna ufisadi wa kuda mtu
kwahiyo tunakubaliana kuwa marehemu alikuwa miongoni mwa mafisadi na kaonewa na mafisadi wenzie katika harakati zao za kutaka kupeana vyeo ili wapate kuongeza mianya ya kufanya ufisadi zaidi...so marehemu hapaswi kuonewa huruma,wakuonewa huruma mwananchi ambaye alitegemea baada ya marehemu kujiuzulu labda angechukuliwa hatua au kutaifishwa baadhi ya mali zake kulingana na ufisadi alioufanya...unakumbuka yale malipo ya milioni 150+ kwa siku?
 
Hilo bwege we hujalizoea? Amejiconfuse mwenyewe. Eti CHADEMA ndiyo inamtegemea km mshauri wao?

Nni lini nilikuwa mshauri wa CHADEMA?

Unachotakiwa kufahamu ni kuwa, hakuna hata kiongpzi mmoja wa CHADEMA wa ngazi ya Taifa anayenifahamu au ambaye amewahi kukutana nami ana kwa ana.

Sijawahi kuwa mshauri wala kiongozi wa chama chochote cha siasa. Nimewahi kutana ana kwa ana na Lowasa RIP, niliwahi kuongea kwa simu na Magufuli RIP kabla hajawa Rais, niliwahi kukutana na Mwalimu Nyerere na kushikwa mkono nikiwa chipukizi. Zaidi ya hawa, nao ilikuwa ni matukio ya mara moja, na siyo uhusiano wa karibu, sijawahi kuwa karibu kiasi cha kuweza kuwa mshauri wa kiongozi wa chama chochote cha siasa. Naendelea kuwa mtaalam mshauri wa taasisi mbalimbali za nje kwenye fani yangu, lakini siyo siasa wala siyo uongozi. Hivyo kudai kuwa eti CHADEMA inanitegemea kama mshauri wa chama, ni uwongo mkubwa, labda kama ni ushauri wa kupitia haya maandiko ya JF.
 
Sasa, kama Lowassa alimwambia Kikwete anataka kujiuzulu, Kikwete akakataa, lakini Lowassa akalazimisha kujiuzulu, huoni Lowassa kajitakia mwenyewe kupigwa chini kwa kulazimisha kujiuzulu?

Ulitegemea vipi Kikwete aendelee ku support mbio za Urais za Lowassa baada ya Lowassa mwenyewe kulazimisha kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond?

Yani ulitaka Kikwete ampigie kampeni ya urais Lowassa aliyeshindwa Uwaziri Mkuu kwa kashfa?

Huoni kwamba Lowassa ndiye aliyemsaliti Kikwete hapo kwa kulazimisha kujiuzulu na kumuachia manyanga Kikwete, wakati labda alihitajika kupambana akiwa upande wa serikali?

Mtu aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na msukosuko wa kashfa, unajuaje akipata urais na kupata msukosuko wa kashfa hatajiuzulu tena?

Lowassa alipewa mtihani wa uongozi, akashindwa. Kikwete akaona huyu kashindwa, twende na wengine.

Hata mimi ningemshangaa sana Kikwete kama angempigia kampeni Lowassa kwa sababu ni rafiki yake tu.
A good analysis.
 
Ingekuwa ni dhulma wala asingeiacha Chadema na kurudi tena kule CCM kirahisi.

Naamini kuwa Lowasa maisha yake yote alikuwa ni mwanaTANU na baadaye mwanaCCM. Alienda CHADEMA ili agombee Urais akijua ana watu wengi waliokuwa wakimwunga mkono, hasa ndani ya CCM.

Alijua wazi kuwa jina lake halikukatwa na CCM bali maadui zake wenye nguvu ndani ya CCM, ambao walikuwa wanajulikana na wanahesabika.
 
Hakuna maana pana hapo mkuu, mchakato wote unahusisha watu na watu ndio wanapitisha watu wachaguliwe kuwa marais. Rais Kikwete inaaminika alienda Dodoma na majina yake matano ya mfukoni, labda kama unataka kusema Mzee Kikwete ni Mungu.

Mungu amekupa Pumzi uyatafute maarifa, Mungu hajawahi kumfanyia mtu chaguo hapa duniani.
Hata JK kwenda Dodoma na majina matano na Lowassa kutokuwepo ni mpango wa Mungu pia, labda hujui namna Mungu anavyofanya kazi kupitia sisi katika maisha yetu ya kila siku.

Hujawahi kusikia hadithi mbalimbali za namna Mungu anavyowaokoa watu wanaotaka kusafiri na ndege wanakutana na vikwazo mbalimbali kutoka kwa familia zao wenyewe halafu baada ya ndege kuanguka ndio wanaanza kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa na kifo?.

Baadhi ya watu walikwepa kifo siku ile ya September 11 kule New York wakiwa wamekwenda kwanza kuwaacha shuleni watoto wao saa mbili asubuhi na wakati ndege ya kwanza inalipuka saa mbli na dakika 48 asubuhi walikuwa bado wapo njiani wakienda ofisini, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.

Apumzike kwa amani Lowassa, amefanya mengi lakini hakuna sababu ya kuhuzunika kuukosa Urais, hii ni nchi yenye watu milion 63 haupo uwezekano kila mwenye ndoto za kuingia ikulu aje siku moja aitimize ndoto yake hiyo.
 
Alita
CCM gani wewe unayoizungumzia? Hiyo ambayo wajumbe wengi wakiwemo kina Nchimbi, Sophia Simba, Kimbisa, Bashe, Musukuma n.k walifura hadi kuanza kuimba wana imani na Lowassa baada ya kutoliona jina lake??

Haijalishi ishu ilikuwa kweli au laah ,hata watu hawana uhakika kama Lowasa alihusika ila alishakuwa na shutuma watu wengi walikuwa wanajua ameiba.


Kumuweke Magufuli ni trick mpya kwa vile hakuwa na kashfa kwa sana , Magufuli sio mkamilifu ila angalau alikuwa anajulikana kwa utendaji kazi wake .

CCM ni kubwa kuliko Lowasa na hakuna ugomvi wa Lowasa na CCM mpaka anakufa .
 
Kila mahala mitandaoni watu wanajadili usaliti wa Kikwete, na kama vile wanamsuta na kumsonkora kwa kimsaliti rafiki yake mkubwa, Edward Lowassa.

Usaliti si mzuri
 
Hakuna mnafiki aliyejaa ghiliba kama Jakaya! amemuambukiza na mchepuko wake saa100!
Kikwete alifanya maasi mengi sana kimya kimya huku akitoa meno nje kama anatabasamu la mbwa aliyeona mfupa!
Jakaya alijipendekeza akaanzisha mchakato wa katiba mpya baadaye akaja akaufuta. Huyu ndiye majinuni mkubwa kwenye taifa hili.
Jakata alishiriki wizi wote mkubwa kuanzia richmond (ambayo alimsukumia EL akafa nayo.
Escrow: Magunia ya Noti yalipelekwa ikulu kwa maelekezo ya Jakaya. Huyu ni wa kukamata kabla hajatutoka! kupoteza ushahidi!!!
Uchunguzi huru ukifanyika utawakamata Jakaya na saa100 kwa mauti ya Magu! trust me>
Kurogana vile vile vilikuwa wazi mno!
Katika watu walio yumbisha taifa ni huyu Mzee Kikwete, ni Jambazi sugu limejificha kwenye kichaka cha Urais mstaafu, mauji mengi ya wanasiasa ana kwa njia moja au nyingine, mnafiki ni balaa, lakini wananchi wamesha mshitukia
 
Kwenye siasa mambo ya kusalitiana ni kawaida na wanasiasa wanalijua hilo, Kinachofanya watu wamkosoe JK sio usaliti ni unafiki anaouonyesha na sio JK tu viongozi wengi wanaonyesha unafiki ila JK amekuwa # 1 on trending kwa sababu ya tukio la 2015.
All in all ....WANASIASA PUNGUZENI UNAFIKI HAYA MNAYOFANYA KWA EL NA NYIE MTAFANYIWA SIKU MUNGU AKIWAPENDA ZAIDI.
 
Kumuweke Magufuli ni trick mpya kwa vile hakuwa na kashfa kwa sana , Magufuli sio mkamilifu ila angalau alikuwa anajulikana kwa utendaji kazi wake .
Hakuna trick yoyote, hiyo ni bahati ya mtende tu ilimdondokea jiwe, njia zote zilikuwa zimechorwa kuelekea kwa jasusi wa Rondo. Wajumbe waliomuweka ENL moyoni ndio walioamua kama wenzao jikoni wamemwaga mboga basi wao bora wamwage ugali tu wote wakose walale njaa.
 
Back
Top Bottom