Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Mkuu ni nadra sana au hakuna mahali popote duniani Rais au mtawala mkuu wa nchi anaweza kuthibitika kutenda mambo yoyote yaliyo mabaya zaidi sana kwenye nchi ambayo katiba imempa madaraka makubwa mno Rais na kumfanya kutowajibika au kuweza kuwajibishwa na chombo chochote.

Ni vigumu kuona popote Hitler akisema au akitoa amri ya Wayahudi kuuwawa, ni vigumu sana hata kwa madikteta wakatili sana kupata ushahidi popote wakiamuru mateso kwa wapinzani na wakosoaji wao, mara zote huwa ni watu "wanaojipendekeza". Ila kama mtawala hataki mambo fulani ni wajibu wake kuonyesha kwa kauli zisizo na kificho hataki hayo mambo na kuwaondoa kabisa wanaojipendekeza wanaoweza kufanya hayo mambo asiyokubaliana nayo.
 
Halafu inaendeshwa kwa karata tatu.

Cheusi umeliwa wewe, chekundu nimekula mimi 🤣🤣🤣.

😂 😂 😂 😂 😂 😂 Kama wana majuto wajijutie wenyewe...kama wana machozi wajililie wenyewe. Huwezi kufikiria nchi yenye watu Mil 60 ni mali ya watu wachache. Waigawane wanavyotaka.

Ni ujinga uliojificha kwenye usomi.
 
Lazima umtetee huyo bwege wenu anaewalisha nyie maboya!

Hapana...Marehemu aliigizwa cha kike..ila alidhani yeye ni mtoto wa mujini haikumuhusu. Mnagawanaje nchi kama vile ni mali yenu binafsi? Ni utopolo uliopitiliza
 
Sawa,

Na JK alikuwa anaangalia "political expediency". Alikuwa mtu wa mahesabu.

Alikemea pale alipoona kuwa watu wanaonewa wakati hata wasipoonewa hakuna impact kwenye serikali yake.

Lakini pia, kuna mengi hakuamuru, ila yalifanyika na hakukemea, kwa sababu yalimpa political advantage.

Ndiyo maana hata polisi walikuwa wanabahatisha bahatisha wanakamata kamata hawajui wapi mzee atafurahia na kuwaacha tu, na wapi ataona hapafai na kuwakaripia.

Kwa hayo siwezi kumtetea.

Lakini, kwenye la Lowassa, Lowassa kukubali kujiuzulu tu alijiangusha mwenyewe.

Kuna jamaa mmoja anaitwa Preet Bharara. Mmarekani mwenye asili ya India. Alikuwa US District Attorney for The Southern District of New York. Hapo ndipo kwenye ma deal yote machafu ya Wall St. Majambazi ya dunia ya wizi wa kalamu kwenye New York Stock Exchange , NASDAQ etc yalikuwa chini ya jurisdiction yake, ma boss yote ya Mafia ya New York City yalikuwa kwake. Hicho kiti alikalia Rudolph Giuliani kabla hajawa meya wa New York City.

Sasa, Trump alivyoingia kuwa rais alimkuta huyu Preet Bharara. Trump alijua kuwa ana madudu mengi sana hapo New York City. Akawa anataka kukutana na Preet Bharara ampange. Trump huwa ana ujinga fulani wa kuleta u Mafia kwenye kazi za serikali. Yani anawaambia wale wateule wa rais waape kiapo cha kuwa watiifu kwake personally, si kwa rais wa US.

Sasa huyo jamaa Preet Baharara anajua kazi yake vizuri, yani kazi yake haimruhusu hata kukutana kutana na rais ovyo. Kwa sababu kazi yake inamtaka awe huru na ana mipaka mpaka ya kuweza kumchunguza rais. Sasa Trump akawa anataka kukutana na Preet Bharara. Preet anauliza sababu, anataka justification kisheria na kikazi. Trump akawa hawezi kutoa sababu. Preet Baharara akawa anampotezea.

Trump akamwambia Preet Bharara, Preet, usiringe kukutana na mimi, ninaweza kukutoa kwenye hiyo kazi. Preet Bharara akaendelea kukataa kukutana na Trump.

Trump akamwambia Preet Bharara, naona hatutaendana, nakutaka ujiuzulu nichague mtu mwingine akalie hicho kiti.

Preet Bharara akamwambia Trump, over my dead body, sijiuzulu ng'o. Kama unataka, nifukuze kazi dunia nzima ijue umenifukuza kazi. Nijiuzulu kwa sababu gani wakati sijakosea kitu?

Trump akaona hakuna jinsi. Akamfukuza kazi Preet Bharara.

Politico waliandika hii habari hapa.


Sasa, huyu Muhindi Mmarekani mimi namuheshimu sana.

Kwa sababu, ni mtu ambaye alijiona hana kosa, akaombwa kujiuzulu kisiasa, akakataa, ikabidi afukuzwe kazi dunia nzima ijue katoka kazini kwa kufukuzwa, si kwa kujiuzulu.

Sasa, mtu kama huyu Preet Bharara akiniambia kuwa yeye hakufanya lolote baya, ndiyo maana hakujiuzulu, amefukuzwa kazi kwa sababu za kisiasa, naweza kumsikiliza.

Si Lowassa, mtu aliyekubali kuandika barua ya kujiuzulu mwenyewe.

Ukishaandika barua ya kujiuzulu umekubali makosa.

Watu wakikuchinjia baharini kisiasa baada ya hapo ni sawasawa tu.
 
Wajinga wenzako wame like,eti wewe una akili [emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Wote hawakuwa wema kwa watanzania, walilinda maslahi yao binafsi na watu wao, mwananchi akaachwa ajipambanie katika mazingira magumu.

Huu utamaduni mpaka sasa unaendelea.

Labda kama ita make sense kuwa JK alikuwa na huruma kidogo kwa kuwaza huyu akiingia kwa ushauri ambao huwa ananipa, hata hayo mazingira magumu, yatakuwa magumu zaidi.

Ndio maana wakatuacha tena kwa mtu alieamua kutubatiza na jina kabisa "wananchi wanyonge", nae akaendelea na mambo yale yale, akayapaka rangi tu na maigizo mengi.

Rais wa kujali maendeleo ya Tanzania kiujumla hawezi kutoka CCM, labda kile chama kipasuke na kufuta tamaduni mbovu zilizopo katika masuala ya kiuongozi.

Lowasa(R.I.P) alidhulumiwa au hakudhulumiwa, alikuwa anacheza timu ambayo huo ni utamaduni wao.
 
Waswahili wa Pwani sio watu wakuwaamini.


Lowasa alifanya kosa kubwa kumuamini mswahili
Lowassa alikataliwa na Julius Nyerere 1995

Lowassa akakataliwa na Bunge 2007

Lowassa akakataliwa na Chadema akawekwa kwny orodha ya wahalifu wakubwa wa Taifa
Lowassa akakataliwa na Dr Wilbroad Slaa

Jakaya pamoja na tofauti zake na Lowassa hakuhujumu miundombinu ya kiuchumi ya Lowassa hata mmoja

lakini baada ya Jk kustaafu Lowassa kishapelekwa polisi na kuanza mbinyo wa kiuchumi hadi akarudi chamani
 
hata mimi naona kuna jitu linaenda kuishi maisha ya wasiwasi sana hadi pale Mungu atakalichukua..maana lilitenda dhurma na uongo mwingi kwa wengine. pole yake
 
JK inawezekana ana matatizo yake, mengi tu.

Lakini, kwenye hili la Lowassa.

Mimi sielewi kwa nini JK analaumiwa kwenye hili.
Tena mainly wanaomlaumu ni Chadema followers...hapo ndo inazidi kushangaza
 
Tena mainly wanaomlaumu ni Chadema followers...hapo ndo inazidi kushangaza
Sio kweli kuwa wengi wanaomlaumu Kikwete ni wa Chadema; Lowassa alikuwa na following kubwa ccm kuliko alipoingia Chadema !!
It was his overwhelming following in ccm which catapulted Magufuli to be the ccm presidential flag bearer and ultimately the Tanzania President!
 
Tena mainly wanaomlaumu ni Chadema followers...hapo ndo inazidi kushangaza
Sasa hivi kuna kulaumu fulani kwa chuki na ushabiki tu. Sio kwamba hakuna kulaumu objectively, lakini kuna watu wanalaumu kwa fashion.

Yani mimi kuna mengi sana namlaumu Kikwete, lakini ukitaka kujua mtu anayelaumu objectively, angalia kama hata siku moja kamtetea Kikwete.

Ukikuta mtu kila kitu, kila siku anamponda tu Kikwete, kila siku, kila kitu, anaponda tu, ujue hapo hakuna objectivity, ni kulaumu kwa mkumbo, kwa ushabiki.

Kikwete hawezi kuwa amepatia kila kitu, lakini pia, hawezi kuwa amekosea kila kitu, sasa inakuwa vipi ukose kizuri chochote cha kusema hata siku moja moja?

Mimi naweza kumlaumu Kikwete leo kwenye jambo moja, kesho likaja jambo lingine nikamtetea.

Kwa sababu, najikita kwenye jambo zaidi, hoja, si kumuangalia mtu.

Kikwete mini sina shobo naye, nilikuwa naitwa kwenda kujutana naye nyumbani kwa balozi New York City, natoa udhuru tu kwa heshima ya balozi kusema ningependa kwenda, lakini nitakuwa kazini.

Kwa sababu nilikuwa naogopa naweza kwenda halafu nikamkaba rais, halafu balozi akaonekana hana maana kakaribisha wahuni waende kula na rais.

Lakini, hilo halina maana hakuna nilipoona Kikwete yuko sawa.

Kuna mtu kanukuu post yangu ya kitambo leo kuhusu kumtetea Kikwete.

From February 26 2011.

Post in thread 'Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko' Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko
 
Sipo upande wowote, lakini sioni dhulma yoyote hapa iliyofanywa na kikwete. Kikwete alikuwa na haki ya kuchagua kuwa anapendelea nani awe Raisi anayefuata, lakini haki hiyo haikuwa imefungwa kwa vigezo vya urafiki na Lowasa au kuwa kama mtu aliyeko kwenye Kifungo huru. Hakuwa na deni kwa Lowasa, hivyo ilikuwa ni haki yake kuchagua.

Mbali na hilo, kujiuzulu kwa Lowasa ulikuwa ni mpango uliolenga kuwapa masilahi wote wawili, na kama hujui Lowasa hakujiuzulu by surprise. Mchezo wote huu ulikuwa kwenye mpango na walijadiliana pamoja, wala haikuwa na tafsiri ya kuzungukana.

Sasa Basi, haijalishi ni mangapi Kikwete alifanya na Lowasa huko nyuma lakini yote hayo hayakuwa na kusudi la kumfanya yeye kufungwa katika kufanya machaguzi yake aliyoyapenda kwa moyo wake. Hakuna dhulma aliyoifanya kwa Lowasa.
 
Cha kushangaza hata kamati ya Bunge haikumpa shinikizo la kujiuzulu.
Kamati haikumuhoji, maana hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia hatiani.
Kama hivyo ndio ilivyokuwa Kikwete alikuwa na sababu gani kukata jina na Lowassa lisiende kupigiwa kura ? Roho ya korosho, halafu anakuja msibani bila haya anatamka kuwa marehemu bado alikuwa rafiki yake!! Jamaa ana roho ya kichawi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…