Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
JK kama mtu ana mapungufu yake, hawezi kukosa. Huwezi kuongoza mamilioni ya watu ukakosa matatizo.Unanishangaza unavyoamini kupitiliza maneno ya JK, mpaka unajigeuza kabisa kuwa kama msemaji wake!.
Angekuwa haogopi maneno yule;
- Asingehangaika kumtuma Makonda akampige ngumi Mzee Warioba wakati wa utawala wake.
- Asingehangaika kuyavuruga maandamano ya Chadema kule Arusha, kwa kutumia polisi na kuwaumiza waandamanaji.
- Wala asingehangaika kumteka Dr. Ulimboka, aliyekuwa akipigania haki za madaktari, akaokotwa ameumizwa kwenye msitu wa Mabwepande, wakati ule wa utawala wake.
Hapo hakuna cha Saigon wala upepo.... tafakari. Anawadanganya na wenzio kwa maneno matupu, mnadanganyika, huku chini chini anachukua hatua kwa vitendo, ndicho alichomfanya Lowassa.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Lakini, haya mambo mengi hatuna hata uhakika kama yametokea hivyo yanavyosemwa yalitokea, na kama yametokea kweli, ni JK aliyeamuru ama watu wa chini yake tu wamejipendekeza kufanya mambo bila amri.
Sitaki kuongea mengi, lakini nataka kusema kwamba ukiongea katika network za kifamilia, halafu ukisikiliza stories za kwenye magazeti na vijiweni, stories nyingi ni tofauti sana. Tatizo viongozi wa Bongo hawana uwazi. Mimi saa nyingine naongea na hao watoto wa kina Warioba na Lowassa, naona dah, kazi yetu kupata story straight ni kubwa sana.
Kuna mambo nashindwa hata kukubishia kwa sababu sitaki kutengeneza mzozo ambao hauwezi kuwa settled one way or another hapa.
Ukweli utabaki kuwa, kipindi cha JK ni kipindi ambacho watu walikuwa huru sana kusema. Kipindi pekee cha kukilinganisha na kipindi cha JK ni kipindi cha Mzee Mwinyi cha Ruksa.
Mambo mengine mtamlaumu JK wakati JK hahusiki moja kwa moja na wala hajaagiza mtu.
Nitakupa mfano mmoja ninaoujua binafsi unaoonesha mambo mengine mnaweza kumpa lawama JK kuwa kaamuru, wakati hata hakuamuru na in fact yupo against nayo.
Kipindi cha JK Jamiiforums ilikuwa moto sana. Kipindi hicho FMES (RIP) na wenzake waliokuwa serikalini walikuwa wanapata sana nondo za ndani ya serikali na kuzimwaga hapa, watu wakawa wanachambua mambo na kuinanga serikali kwa style ya "Kumkoma Nyani Giladi". Wakongwe wa JF watakumbuka.
Sasa, ikatokea Polisi fulani wakubwa wakawa wanataka sifa, wakamkamata mkuu Maxence Melo. Wakamfunga.
Kusikia hivyo, tukalianzisha bonge la timbwili kimataifa. Tukawatafuta "The Committe to Protect Jouranalists" www.cpj.org , tukawatafura Human Rights Watch, wakalianzisha timbwili kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Shout out to Mimi Mwanakijiji kwa kazi kubwa aliyoifanya.
Tanzania ikawa ina trend vibaya kwamba inaminya uhuru wa habari.
JK kusikia hivyo, akasema kwa nini mnawasumbua hawa vijana wa dotcom ambao hawana hata impact kwenye utawala wangu? Waachieni tu, msiwabugudhi. Msinichafulie jina la nchi yangu bila sababu.
Mara moja Max akaachiwa.
Sasa, kwa mtu ambaye hakuwa karibu na ile story, angeweza kujua kuwa JK aliamuru Max ashikwe, halafu ikaonekana issue imeleta negative press kimataifa, akaamuru Max aachiwe.
Kumbe, Max alivyoshikwa hata JK hakujua.
Mambo mengine tunaweza kumlaumu JK kwa sababu watu wa chini wamejipendekeza tu. JK mwenyewe hata hakuyapenda.