Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Unanishangaza unavyoamini kupitiliza maneno ya JK, mpaka unajigeuza kabisa kuwa kama msemaji wake!.

Angekuwa haogopi maneno yule;

- Asingehangaika kumtuma Makonda akampige ngumi Mzee Warioba wakati wa utawala wake.

- Asingehangaika kuyavuruga maandamano ya Chadema kule Arusha, kwa kutumia polisi na kuwaumiza waandamanaji.

- Wala asingehangaika kumteka Dr. Ulimboka, aliyekuwa akipigania haki za madaktari, akaokotwa ameumizwa kwenye msitu wa Mabwepande, wakati ule wa utawala wake.

Hapo hakuna cha Saigon wala upepo.... tafakari. Anawadanganya na wenzio kwa maneno matupu, mnadanganyika, huku chini chini anachukua hatua kwa vitendo, ndicho alichomfanya Lowassa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
JK kama mtu ana mapungufu yake, hawezi kukosa. Huwezi kuongoza mamilioni ya watu ukakosa matatizo.

Lakini, haya mambo mengi hatuna hata uhakika kama yametokea hivyo yanavyosemwa yalitokea, na kama yametokea kweli, ni JK aliyeamuru ama watu wa chini yake tu wamejipendekeza kufanya mambo bila amri.

Sitaki kuongea mengi, lakini nataka kusema kwamba ukiongea katika network za kifamilia, halafu ukisikiliza stories za kwenye magazeti na vijiweni, stories nyingi ni tofauti sana. Tatizo viongozi wa Bongo hawana uwazi. Mimi saa nyingine naongea na hao watoto wa kina Warioba na Lowassa, naona dah, kazi yetu kupata story straight ni kubwa sana.

Kuna mambo nashindwa hata kukubishia kwa sababu sitaki kutengeneza mzozo ambao hauwezi kuwa settled one way or another hapa.

Ukweli utabaki kuwa, kipindi cha JK ni kipindi ambacho watu walikuwa huru sana kusema. Kipindi pekee cha kukilinganisha na kipindi cha JK ni kipindi cha Mzee Mwinyi cha Ruksa.

Mambo mengine mtamlaumu JK wakati JK hahusiki moja kwa moja na wala hajaagiza mtu.

Nitakupa mfano mmoja ninaoujua binafsi unaoonesha mambo mengine mnaweza kumpa lawama JK kuwa kaamuru, wakati hata hakuamuru na in fact yupo against nayo.

Kipindi cha JK Jamiiforums ilikuwa moto sana. Kipindi hicho FMES (RIP) na wenzake waliokuwa serikalini walikuwa wanapata sana nondo za ndani ya serikali na kuzimwaga hapa, watu wakawa wanachambua mambo na kuinanga serikali kwa style ya "Kumkoma Nyani Giladi". Wakongwe wa JF watakumbuka.

Sasa, ikatokea Polisi fulani wakubwa wakawa wanataka sifa, wakamkamata mkuu Maxence Melo. Wakamfunga.

Kusikia hivyo, tukalianzisha bonge la timbwili kimataifa. Tukawatafuta "The Committe to Protect Jouranalists" www.cpj.org , tukawatafura Human Rights Watch, wakalianzisha timbwili kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Shout out to Mimi Mwanakijiji kwa kazi kubwa aliyoifanya.

Tanzania ikawa ina trend vibaya kwamba inaminya uhuru wa habari.

JK kusikia hivyo, akasema kwa nini mnawasumbua hawa vijana wa dotcom ambao hawana hata impact kwenye utawala wangu? Waachieni tu, msiwabugudhi. Msinichafulie jina la nchi yangu bila sababu.

Mara moja Max akaachiwa.

Sasa, kwa mtu ambaye hakuwa karibu na ile story, angeweza kujua kuwa JK aliamuru Max ashikwe, halafu ikaonekana issue imeleta negative press kimataifa, akaamuru Max aachiwe.

Kumbe, Max alivyoshikwa hata JK hakujua.

Mambo mengine tunaweza kumlaumu JK kwa sababu watu wa chini wamejipendekeza tu. JK mwenyewe hata hakuyapenda.
 
Hata hili nalo bado linahitaji uhakiki.

Kwa sababu michakato yetu haina uwazi.

Lakini, hata kama ikiwa kweli, Lowassa mwenyewe alijijengea mazingira ya kukatwa kwa kujiuzulu (against Kikwetes advice per Bams).

Sasa, ikiwa Kikwete alikuwa na choice, CCM iende na mgombea ambaye hana wingu la kashfa za ufisadi, ambaye itaweza kuanza naye kampeni moja kwa moja bila kumsafisha, au iende na mgombea mwenye wingu la kashfa za ufisadi, mpaka akajiuzulu, kiasi kwamba huyu mwenye kashfa, chama kabla ya kuanza kampeni, kitahitaji kutumia nishati na muda wa ziada kumsafisha kwanza, kabla ya kuongelea ajenda za chama kwenye kampeni.

Hapo kweli mnaona Kikwete alipaswa kukubali mgombea mwenye wingu la ufisadi aende ku distract message ya ajenda za CCM na kuwabebesha mzigo wana CCM kumsafisha kwanza kabla ya yote?

Kikwete aliona twende na mtu asiye na mzigo wa ziada wa kashfa. Tujikite kwenye kuelezea ilani ya chama zaidi kuliko kumsafisha mtu.

Hoja ya kuwa Kikwete alikataa Lowassa asijiuzulu sio kweli. Lowassa alijiuzulu baada ya kuona hana support ya Rais!!
Hata kama asingejiuzuru na kuendelea na uwaziri mkuu lile doa la ile kashfa lisingeondoka !
Hata hivyo uzito wa kashfa ile na jinsi ingeathiri chama ungeamuliwa kwa kura za wanachama na sio kiongozi mmoja kwa kutumia mamlaka ya uenyekiti! Kikwete angeacha kura za wajumbe ziamue kama Lowassa angefaa kupeperusha bendera au la!’ Mkwere kwa fitina zake akaingia na majina aliyetaka yeye wakiwemo Chawa wake watatu ; January Makamba, Asha Rose Mtengeti na Membe!!
Hao wengine Magufuli na Amina kwake walikuwa wasindikizaji!
Amina should have been the de facto vice presidential pick but in her campaign speech she alluded to be pro Lowassa hence again Kikwete used his influence to pick Samia instead of Amina as is always the case! Amina missed the Vice presidential slot simply by mentioning Lowassa’s name.
 
Kwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?

Cha ajabu wanaolia Lia na hili ni Chadema...kama Lowassa aliona Ccm wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema inawauma sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?

Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Inashangaza sana mkuu
 
Nimesoma kidogo lakini kubwa nimeona umbea umetamalaki,mara ndege alikodi Lowasa,mara Membe mdogo wake Kikwete! Membe mmwera kwa baba na mama wakati Kikwete ni mkwere kwa baba na mama! Huu ujinga unaopeana kwenye vijiwe vya kahawa muuache hukohuko jamani.
Nimeongelea hili tatizo la speculation na kusema tatizo linakuzwa zaidi na ukweli kwamba viongozi hawaandiki vitabu kuelezea maisha yao, na wachache wanaoandika vitabu kuna mengi hawayaandiki.

Ukisikiliza haya maneno ya umbeaumbea mitaani, na pengine hata magazetini, halafu ukalinganisha na habari unazopata kutoka family networks, kwa watu tunaojuana na hizi familia za viongozi na kuongea kirafiki, kuna mambo mengi ya uongo yanasemwa.

Halafu kuna mengi ya ukweli ambayo ni mabaya kuliko hayo ya uongo hata hayajulikani.
 
Hoja ya kuwa Kikwete alikataa Lowassa asijiuzulu sio kweli. Lowassa alijiuzulu baada ya kuona hana support ya Rais!!
Hata kama asingejiuzuru na kuendelea na uwaziri mkuu lile doa la ile kashfa lisingeondoka !
Hata hivyo uzito wa kashfa ile na jinsi ingeathiri chama ungeamuliwa kwa kura za wanachama na sio kiongozi mmoja kwa kutumia mamlaka ya uenyekiti! Kikwete angeacha kura za wajumbe ziamue kama Lowassa angefaa kupeperusha bendera au la!’ Mkwere kwa fitina zake akaingia na majina aliyetaka yeye wakiwemo Chawa wake watatu ; January Makamba, Asha Rose Mtengeti na Membe!!
Hao wengine Magufuli na Amina kwake walikuwa wasindikizaji!
Amina should have been the de facto vice presidential pick but in her campaign speech she alluded to be pro Lowassa hence again Kikwete used his influence to pick Samia instead of Amina as is always the case! Amina missed the Vice presidential slot simply by mentioning Lowassa’s name.
Mkuu,

Kama unabishia hoja ya Kikwete kukataa Lowassa kujiuzulu, bishana na Bams kuhusu hilo.

Yeye ndiye kaileta hoja hiyo hapa. Mimi nimenukuu kwake tu na najitahidi kila ninaponukuu kumpa credit ya "per Bams".

Hoja ya kwamba Kikwete ndiye alikata jina kama Mwenyekiti kwa maamuzi yake pekee nayo bado inahitaji uhakiki. Suala hili limekubalika tu bila uhakiki wala ushahidi.

Mfumo mzima wa uteuzi wa CCM una mazingaombwe mengi, hata JK naye kuna malalamiko kuwa alibadilishiwa gia angani 1995 na Nyerere. Sheria za mchezo zikabadilishwa katikati ya mchezo kumpa ushindi Mkapa.

So, we have a systemic problem there, not a JK problem.
 
Mada hii inaweza kuonekana ni nzuri muda huu wakati wa kuuhani msiba wa Lowassa, lakini ghafla pumzi ikimrudia hayati naamini huu uzi utakosa kabisa mashiko.

JK anazeeka na amani sio kwa sababu aliishi vizuri alipokuwa rais na kabla ya hapo, ni kwa sababu hana vinyongo vingi na hujitahidi kucheka na kusamehe kabla hajaenda kulala usiku.

JPM alikufa na vinyongo vingi na vikautesa moyo wake, Lowassa nae alihamia kwenye ulevi wa pombe kali baada ya kuukosa urais.

Ukiwa mwanasiasa punguza kabisa uwezekano wa kulala na chuki moyoni, itautesa moyo wake na itakuua siku moja.

Hilo ni somo la maisha ya JK, hana wema huo na haonekani kupigania ile hulka ya kutaka watu wamuone mwema lakini kajaliwa sana ule moyo wa kiswahili wa kuchukulia kila kitu katika mtazamo wa masihara.
Mkuu Steve, naunga mkono hoja Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

P
 
Wewe bwege hujui kuwa maamuzi ya mtu na vitendo vyake vinaweza kufanya maradhi yakamdhoofisha mgonjwa haraka! To me Kikwete ndio alisababisha Lowassa akapata stroke!
Kwavile wewe chawa wa mkwere utatuma na matusi yako hayatabadiri ukweli kuwa Jakaya hana utu na ni JambaziI tu!
Hauna akili mbwa wewe
 
Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.
Jumla nakubaliana na wewe kuhusu jk kumdhulumu Edo. Lakini kwamba Edo alihiyari kujiuzuli, sidhani kama ni kweli. Kumbuka wakati ule umaarufu wa Edo ulikuwa juu sana, nadhani hata kiasi cha jk kupata hofu. Hivyo jk alimfiksi rafiki yake jiuzulu halafu baadae haya ya Richmond yakishapoa nitakunyanyua. Edo alipoingia huo mkenge ndio ikawa fursa kwa jk huhakikisha hafurukuti tena.
 
JK ana bullet proof ya kisaikolojia kwenye hivi vimaneno maneno vya mtaani.

Mtoto wa Saigon yule kazoea matani ya wazee wa Kiswahili yale ya kujambishana kwenye vikao vya kahawa chungu nyeusi na kashata.

Vikao vile kama huna kifua cha kuhimili maneno huviwezi, na JK ndiyo vikao vyake.

Sasa Mswahili kama yule unafikiri unaweza kumtisha kwa maneno tu?

Kashasema "Huo ni upepo tu, utapita" wakati yupo katikati ya heavy scandal.

Unafikiri ataogopa maneno ya waombolezaji msibani?

Mtu kashajipitia life expectancy ya wabongo, kashakula mazuri ya nchi yote, kashaandaa vizazi na vizazi kukaa vizuri hata akifa kesho, anahudumiwa na taifa mpaka kufa, anataka amani gani zaidi ya hiyo?
Amani ya vitu anayo kwani ni fisadi aliyekubuhu na ndio maana akaihujumu katiba waliopendekeza wananchi kwa kulinda ufisadi wake!
Kwa mambo ya dhuluma aliyofanya akiwa madarakani NAFSI yake ndio itakayomuhukumu.
 
Ni hivi, ingekuwa Kikwete kamtuma Lowassa ajiuzulu, kamwambia "Edward, haya maji ni marefu, inabidi tumtoe mtu hapa ili kuinusuru serikali, tena mtu mzito, nakuomba kama rafiki yangu ujiuzulu ili kuinusuru serikali, halafu hapo baadaye mambo yakipoa, tutakurudisha ugombee urais nikimaliza mimi".

Halafu Lowassa akasema "Kweli? Serikali inaweza kuanguka? Na mimi kujiuzulu kwangu ndiko kutainusuru? Mnanitaka nijiuzulu halafu nitakuwa rais baada yako? Hapo hakuna shida, najiuzulu"

Halafu Lowassa akajiuzulu.

Halafu baadaye, alipotaka kuwa rais, Kikwete akamruka. Akamkata.
Ndivyo ilivyokuwa- alimfix.
 
With RESPECT kwako, inaonekana wewe unaishi kule LALA LAND, kama hujui why Lowassa (MHSRIP)alirudi ccm, nikuache tu,kweli mkuu hujui kuwa alilazimishwa kwa kunyimwa haki yake kwa serikali ya ccm kutumia vyombo vya dola,basi wewe ni kenges
I second you. Lowasa na Sumaye hawakurudi ccm kwa hiyari., walilazimishwa (indirectly). Kumbuka manyanyaso waliyopitia kabla hawajarudi.
 
Amani ya vitu anayo kwani ni fisadi aliyekubuhu na ndio maana akaihujumu katiba waliopendekeza wananchi kwa kulinda ufisadi wake!
Kwa mambo ya dhuluma aliyofanya akiwa madarakani NAFSI yake ndio itakayomuhukumu.
Wewe unasema nafsi yake ndiyo itakayomhukumu wakati wengine hata hawaamini kwamba wana nafsi.

Hapa naona dua za kuku nyingi ambazo hazimpati mwewe.

Kama unaona JK ana makosa sana, mfungulie mashtaka, mvizie mtandike kofi, fanya kitu.

Ukisubiri nafsi yake imhukumu wakati mwenzako anajua kula bata tu kwenda mbele, tena kwa kutumia kodi yako, utasubiri sana.
 
Back
Top Bottom