Hivi kwanini makao makuu ya dini yetu ya kikristo yasiwe Israel halafu hawa Wayahudi hivi ni dhehebu gani..?
wayahud sio wakristo Dini yao ni Judaism ni mchanganyiko wa mafundisho ya Agano la kale na taratibu za kiasili za wayahudi...
kama ilivyo kwa Islamic religion ina mchanganyiko wa Taratibu za kidini na tamaduni za kiarabu
judaism ni moja kati ya dini kubwa tatu. ulimwengunk wayahud sio wakristo... hawaamini kuwa Yesu ndie mwokozi na alietabiriwa na yohana mbatizaji.. wao wanasubir mwokoz wao..
tofauti ya Mkristo na Myahud ni kuwa Myahud hana Agano jipya kwenye Biblia yake (Hebrew bible) anatumia Agano la kale tu kwa maana hiyo yeye anafata mafundisho ya agano la kale .. kumbuka Agano jipya ni kumhusu yesu na maisha yake na wao wanaomuona yesu ni mwanaharakati tu na inspirational leader sio Holy figure (Masihi)
ila Ukristo umetoka kwenye judaism ( sexond temple of judaism) ndo maana kuna wayahud wakristo kwa maana ya wanaomwamini Yesu Kristo
Biblia ya Wayahud na ya wakristo ziko sawa tofauti ni ya wakristo imeongezeka Agano jipya ambalo wayahud hawalitambui .. Mkristo maana yake ni anatemfata kristi ambaye ndio Yesu
So kwa ufupi ukiwa ww mkristo ukaingia kwenye kanisa (sinagogi) la wayahud kama unaelewa kiebrania hautapata shida kusali... shida yako itakuwa ni zile taratibu zao za kusali za kiasili (hawakai kwenye viti hawaingii na viatu na wanasujudu) kama unavyoona waislam...
chimbuko la kusujudu au kutokuingia na viatu kwenye masinagogi yao.. wayahud wamepata kutoka kwenye agano la kale pale Musa alipoongea na Mungu kupitia kichaka kilichokuwa kinawaka.. akaambiwa via viatu hapa ni mahali patakatifu.
tukihitimisha ni kuwa Wakristo wanafata mafundisho ya Yesu ambaye kwake yeye life style na material things (kama mavaz na aina ya vyakula ) sio issue kwake , issue ni kuwa msafi wa kiroho na imani. wakat wayahud wanaamin mafundisho ya Musa (agano la kale) ambalo linatoa muongozo wa jinsi ya kuishi na aina ya vyakula.