Kwa hakika jana ni siku ambayo mpira wa Afrika umepoteza mvuto Duniani kote.

Kama tu hamjiamini kwenye NBC premier league je, mtaweza presha za Klabu bingwa Afrika?
Tuna safari ndefu sana mkuu.
Makosa yanayofanywa na CAF giants wanapokutana na underdogs ndio yanafanya tufungue threads hizi.


Ila bado tuko nyuma sana sema tunakujakuja
 
Hapa mkuu tunajadili madhaifu ya CAF na sio simba wala yanga.

Soon nitafungua thread ya madhaifu ya wachezaji wa yanga.
Hamna kitu, madhaifu gani ya Caf??
Wacheni kujificha ficha, boresheni kikosi ala
 
Kwahiyo unamaanisha Engineer nae amebariki mipango ya kuiumiza Yanga?
 
Yote haya kwa sababu ya Yanga tu? Mbona mnapenda kujipa ukubwa msiokuwa nao?
 
Nyie wa mara nyingi ni lini mliwahi fanyiwa hujuma za waziwazi namna hiyo.
Yani Leo umesahau Simba alifungwa goli ambalo clear offside na Orlando nchi iyo iyo na hatua iyo iyo na VAR ipo u wnjani na refa akwenda ata kureview kabisa umesahau dadeki na mwisho Simba akatoka Kwa penati
The same imejirudia kwenu nchi Ile Ile hatua Ile Ile na mna ondoka Kwa penati umesahau hii mkuu
dhuluma ambayo yanga fans walishangilia na Leo ime waumiza Amin Kwamba malipo ni hapa kinachukopa furaha Leo kesho Kita kuumiza ndio hiki kimechoma.
 
Mimi naona jumatatu mashabiki wa yanga waandamane kwenda kwa mama kama kawaida yao ili apate kulitazama na hili haiwezekani wananchi wanyonge wananyang'anywa haki yao kwa nguvu.
 
Kunya anye kuku tu bata kaharisha. Yanga mliambulia pointing moja Kaitaba baada ya Kagera Sugar kudhulumiwa goli halali kabisa. Tena fungeni midomo yenu kabisa mgange yajayo vinginevyo hata NBC League mtaanza kupoteana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…