Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Nani katoa hela? Chanjo ya bure kwenye mfuko wa covax unasema tena wametoa hela? Hivi kwa nini mnakuaga wajinga hivyo? Hivi ni Tzn pekee wako kwenye covax? Unajua gharama za kununua chanjo wewe au unaropoka tuu? Mbona Gwajiboy alivyoambiwa athibitishe alishindwa? Saizi kategewa kwenye vyomba akapayuke teka kule kijiweni kwake ataona moto.Huu ni mkusanyiko wa watu ktk Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam mbele ya rais 02/09/2021. Halafu bila soni akasisitiza chanjo.
Hivi rais Samia yuko serious na gonjwa hili ama anaongea kuwafurahisha na kuwapumbaza walotoa hela?
Mwisho infact serikali ndio inatafuta pesa za mkopo wa masharti nafuu kutoka mfuko wa dharura wa kusaidia nchi maskini kujikwamua na athari za kiuchumi zilizosababishwa na covid 19.
Hiyo pesa is like grand fund lakini ina madharti,Kati ya hayo masharti ni lazima uthibitishe ulivyoathirika,sasa utathibitisha vipi ni kwa kutoa Takwimu za waathirika, vifo, lockdown (mwanzoni kabla ya chanjo) na hatua ulizochukua kukabiliana na ugonjwa na hapa ni dozi za chanjo zilizoidhinishwa.
Kimsingi pale kuna pesa ya Tzn imetengwa karibu dola za Marekani mil.500 zaidi ya Til.1.2 ya madafu.Riba ni ndogo Sana,unalipa mda mrefu ndani ya miaka 30 huku grace period ya kuanza kulipa ni miaka 3-7 kulingana na assessment yao.Sasa wewe kwa akili yako pesa kama hii unaiachaje wakati ukikopa kawaida ni ghali kupata na maumivu kulipa?
Hivi haukumbuki kashfa za kuzika majeneza matupu ya watu kule Uganda Ili wapate pesa? Hii pesa hata Magu aliitaka ila kwa kipindi kile sharti la lockdown hakukubaliana nalo ndio baadae chanjo zikaja.Kama ni mfuatiliaji sio mropokaji Magu mara kadhaa alivyokutana na IMF/WB aliwaambia wapewe mda hata wa miaka 5 wasilipe riba za mikopo na zisiwe zinaongezeka kama mbadala wa mkopo Ili kutoa nafuu kwenye uchumi.
Hiyo pesa ni tamu ikipatikana haraka Sana SGR inatoboa Mwanza na stiglaz inaisha sasa mnavyosikiliza upuuzi wa kina Gwajima ulioanzishwaga na Magu matokeo yake tozo kama kawaida na Rais kasema tozo zitaendelea kama vyanzo rasmi vya mapato Ili miradi isisimame.