Kwa hili Arusha mnatuaibisha Watanzania

Kwa hili Arusha mnatuaibisha Watanzania

Undava King

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,659
Yero subahi wanangu wa ngaramtoni, mbauda, ngalimi na sanawari, mtu akisikia unasafiri unaelekea arusha kichwani anakuhusudu kama mtu anayeelekea.

Geneva ya kibongobongo mawazo yake ni sahihi isipokuwa atokuwa sawa akidhania ya kuwa pia unafaidi raha ya kusafiri kwa usafiri wenye comfort na luxury zote za mabasi kama waendao kwenye majiji mengine nchini.

Kiufupi ukisikia kuna Kenya ndogo inayoexist ndani ya Tanzania na hata watu wake hawakijui vizuri kiswahili karibia hapa penye stendi ugly ilojaa malori(fuso,scania na Isuzu).

Malori haya yalobadilishwa matumizi na kubambikiwa show ya mabasi a.k.a chinjachinja, saga kunguni au mabasi ya vijijini au kwenye minada ya ng'ombe yapo katikati ya jiji yakipakia abiria wasokuwa na hatia tayari kwa kuwatia tetenasi na nauli zao zisizo za kutabirika kuelekea DSM, Mwanza, Musoma, Tanga n.k.

Sasa usiguse hayo mangorika,sijuhi mtei, AM coach, coast n.k utaghahirisha safari yako bure ya kutoka nje ya jiji letu pendwa la utalii bado kwenye vi-hiace ndo balaa usisemee hilo vumbi na vuruge lake hapo ngarenaro stendi mbaya kama zizi la mbuzi haina hata vibao angalau kuindicate uelekeo au mitaa.

Kiufupi Arusha katika upande wa usafiri wa abiria kwa njia ya barabara mnaiaibisha Tanzania be modern bwana mbona mji mdogo kama Tarime umeweza na unamabasi mazuri ya wazawa na mengi pengine kuliko makao makuu ya mikoa mingi nchini na usafiri kule ni uhakika muda wote.

Achilia mbali mabasi yao hayana sura mbaya za kuchongwa na kubadilishiwa matumizi ya mizigo kuwa ya wanadamu ebu tafadhali tuwe japo kidogo na utu na huruma maana tunawaonea sana ndugu zetu wamasaai wanaoenda monduli, kiteto kibaya, simanjiro mirerani,tarakea rombo n.k.

Inawabidi walale guest za city center huku wakigeuka walinzi wakiofia kuachwa na mafuso haya yanayodamka usiku usiku huku yamepakia watu kama kuku usawa huu kweli katika karne ya 21 bado watu.

Wanapakia mizigo na mifugo juu ya carrier/bodi nimewapa mfano mdogo wa Tarime wala msijiangaishe kwenda miji mikubwa au kuomba msaada kwingine kawaulizeni kaka zenu wadogo wamewezaje maana.

Mnatuaibisha wenzenu tunawavumilia mpaka tumewashiba tafadhali wamiliki wakale na wakazi wa jiji pendwa la arusha haya mabasi myatenge na msiwe mnayapanda hili wamiliki na serikali wabadilike miundombinu iboreshwe.

Pamoja na magari yenyewe, haiwezekani wengine daily wanapanda vya kuimport luxury and modern japo tulitamani vingeundwa hapa hapa nchini lakini sisi tunakomaa na mamoshi.

Uchafuzi wa mazingira na uchafuzi wa mandhari ya jiji mwishowe watalii waogope kuzuru nchini kwa kutishwa na mabasi yenye sura nzito ka ya mpoto pili yanaifanya nchi yetu iwe na taswira ya mabasi pendwa ya nchi jirani.
 
Sijui hata ameandika manini?

Jirani hili wingu napata mafua [emoji23]
Jirani kumbe ni wewe! Naona umeamua kujibatiza[emoji1787]

Wingu hili jirani inabidi tutafute mbadala aise[emoji28]
 
Mkuu embu pangilia mada kwa mtindo unaoeleweka. Unaongelea vitu vingi mpaka point ya msingi haieleweki
 
Jirani kumbe ni wewe! Naona umeamua kujibatiza[emoji1787]

Wingu hili jirani inabidi tutafute mbadala aise[emoji28]
Nilisikia walitupa access ya kujibatiza wenyewe si ndio jana nikafanya jaribio 😂

Uhakika mbadala maana chai imegoma leo 🤣🤣
 
Bado wahuni wa hapo stendi wanaojiita wapiga debe, Arusha na Moshi nishida
 
Juzi nikamsikia mtangazaji flani anarudia kauli ya Clinton kuhudu Arusha as if Geneva ya afrika, eti mazingira na miundombinu ya arusha inalingana na hilo jiji 😳!.

Naendelea kumshangaa sana huyo mtangazaji, yaani kuna watu huwa wanashindwa kufungua akili zao kweli, kufananisha mtoto wa jirani na wake!.
 
Tunakuaibisha wewe kama nani sisi tunapenda mabus yenye engine ya scania 113 alafu chuma iwe ya masaa barabarani ni mwendo wa kukaa kulia Hadi inafika kwao.

Chuga ni republic kamili unavyosema hatujui kiswahili kwanza ujue chuga haiongei kiswahili chuga ina lugha yake ya pekee tunaongea kwa code ili mawaki wasituletee dashi za ki lafa kwani hamuoni tu tuko tofauti na nyie?

Hata mavazi yetu mwendo wetu na kiatu ni kubwa ya kucheba
 
Arusha kwa upande wa usafiri wa abiria (mabasi) na miundombinu kama vile stand ni changamoto sana.
 
Arusha kwa upande wa usafiri wa abiria (mabasi) na miundombinu kama vile stand ni changamoto sana.
Mabasi yapi unazungumzia? Buses, coaster or hiace?

Stand wenyewe wanawezana nazo.
 
Arusha bado sana kwenye suala la usafiri yani mpaka leo happy town tu wanatumia vipanya
 
Wana mambo yao fulani wapo vema. Binafsi nikiwa Arusha ninapenda mavituvitu kama sehemu za kula, bidhaa kama mavazi, clubs, hotels, n.k. Arusha ndipo hata nikitaka kufanya usafi wa suti na jackets zangu naufanya kwa kuridhika. Yani unalipa pesa ndefu na huduma swaaafi.Kwa kulinganisha na miji mingine naona wapo juu katika huduma ka hizo. Shida ni miundombinu na mandhari ya mji kwa ujumla. duh! Jiji hili ni kama laana. Mandhari mbovu, hekaheka za hapo down town ndo balaa. Hamna mtazamo wa kimji. Utasema pamepigwa bomu kama Baghdad, kha! Ukijumlisha na huu mtindo wa wafanyabiashara wadogo kujiachia popote, jiji limepinda. Barabara mbovu. Ulaaa!
 
Back
Top Bottom