Kwa hili la Ommy Dimpoz na Babake wee uliye biological mother/father ukimkataa/kumtelekeza mtoto wako ujue umemuumiza sana kisaikolojia na makuzi yake

Kuna baba mmoja jirani yangu hapa alimfanyia unyama mkewe wa ndoa akauza nyumba wakati mke akiwa ameenda kuzika kwao anarudi anakuta nyumba Ipo chini ya mtu mwingine akaenda pangisha na watoto wake kwenye nyumba ya udongo huku jamaa anakula bata na mahawara akaoa kabisa huyo hawara, yule mama na watoto wake presha na mawazo vikamuua hata miaka 6 haijaisha tangu mkewe afariki jamaa laana inamtafuna tu hana hata mia na. Kulima vibarua vya mashambani, anahama hama kwenye vyumba vya kupangisha tu.
 
Najaribu kuliangalia hili kuna mambo naona kama yananifikirisha sana:
Ukimsikiliza baba yake na ommy ni kama alishakubaliana na maisha yake na maisha ya mwanae hana habari nayo maana yake ikiwa alikataa tangu zamani hata sasa hajamuhitaji na wala hajamuomba msaada wowote isipokuwa habari hii imeibuliwa upya na waandishi wa habari ili kutengeneza attention tu
Anasema ni hana ubaya na ommy na wala hana haja na mali za ommy pamoja na kuwa yeye ni baba yake mzazi anaishi maisha yake binafsi na Bajaj zake and nothing more.
Ukimsikiliza ommy ni kama anajaribu kujibu(hamjibu baba yake Lah hasha) anajibu media, watanzania na baba levo, kwa nini hamjibu baba yake ni kwa kuwa yeye na baba yake walishamaliza zamani hawana wanachoweza kuongea tena kila mtu alishaamua kwenda na njia yake
Anachokifanya ommy ni kujibu tuhuma za kumtelekeza baba yake ili kuogopa jamii itakavyomchukulia, ko anajaribu kwa nguvu zake kuonyesha ubaya wa baba yake mbele ya baba levo na media ili kujustify maamuzi yake na kupata kinga kwenye jamii tofauti kabisa na mzee wake ambaye hasemi baya la ommy wala la mke wake mama yake na ommy (hapa najifunza busara na hekima alizonazo mzee)
My note: Ommy huyo ni baba yako, achilia mbali kuwa ni baba mzazi lakini hata angekuwa baba mlezi muheshimu na ufunge mdomo wako jifunze busara kutoka kwake.
Hujui lolote kuhusu kuzaliwa kwako na huko unakokuita kukataliwa kwa kuwa hukuwa unaelewa lolote zaidi ya kusimuliwa na kusikia pengine kwa evidence ndogondogo sana zikakuaminisha kuwa baba yako ni mbaya...(nikukumbushe hapa ni kawaida kwa wanawake kupandikiza chuki kwa watoto wanaowalea wenyewe dhidi ya baba zao, zipo sababu nyingi na za kawaida kabisa za mke na mme kutengana sasa hasira na chuki hupandikizwa kwa watoto na hasa chuki zinazosababishwa na wivu wa mapenzi)
Kwa baba ommy: najua unayajua mengi na hutaki kuyasema kwenye media kuhusu mahusiano yako na mama ommy na ommy hii ni busara ya hali ya juu kwangu naona bado umemlindia heshima marehemu mke wako na hutaki kumdhalilisha mtoto wako. Kwangu wewe bado ni mzazi.
Hebu tusishabikie kwa kulaumu upande mmoja tukasahau kusikia upande uliokimya unasemaje.
Asante
 
Alijisema kuwa yeye ni......BASTARD BOY! Ana courage kweli!
 

Tusishabikie utelekezaji wa watoto

Mama ommy alifariki ommy akiwa primary school. Fikiria wewe ni baba wa aina gani hata pamoja na mzazi mwenzio kufariki hushughuliki wala hujali kumtafuta na kumtunza mwanao katika umri huo mdogo!?

Haya mwanae kasema japo hawajawahi kuwa na ukaribu heshma yake kama baba inabaki palepale. Kuna nini cha ziada ya heshma?

Heshma yashinda mali na ommy anampa heshma; unaweza kuonewa kila kitu kwa kudharauliwa
 
Vijana tupo tayari kumsamehe mpenzi bila tatizo lolote lakini mzazi wako eti!! Haumsamehi ilo ni tatizo
Kama hujawahi kataliwa na mzazi/wazazi usishangae watu wanaoshindwa samehe wazazi waliokula kona. Inaumiza sana.
 

Ukisikia mwanakulaaniwa ndio huyo

KUMBUKUMBU LA TORATI 28:15-30

15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda
 
Asamehe aoe maisha yaende, hawezi badilisha historia asingetelekezwa asingekuwa star.
Cause and effect principal
 
Kwa nini Wanaume wengi mnapenda kujitetea kwa kipengele hiki cha chuki kupandikizwa,mkuu umesikiliza Ommy alivyoelezea alipokuwa anamuuliza marehem Mama yake alimueleza kwamba baba yako amesafiri iko siku atarejea (hapa na mpongeza huyo mama alionesha ujasiri mkubwa) kitendo hiki kilisababisha Ommy ajiulize why baba yake hakutokea hata siku ya msiba.

Hakuna chuki hapo sio kila Mwanamke ni mjinga
 
Hilo kenge acha liumie. Linapata haki yake!
 

Mama yake alifariki akiwa la pili alimezeshwa lini hizo sumu acheni kutteea upuuzi
Omy hajakosea popote
 
Vijana tupo tayari kumsamehe mpenzi bila tatizo lolote lakini mzazi wako eti!! Haumsamehi ilo ni tatizo
Kuna kipindi kinaitwa Long lost Family
Yaani kuna watoto walipelekwa kwenye nyumba za kulelewa ila baada ya miaka kibao hata 50 wameamua kuwatafuta wazazi
Haijalishi Tajiri au masikini mradi tu aondoe yale maswali

Ila sisi ni tatizo kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…