Kwa Mara ya kwanza Napongeza Ubunifu alioufanya Makonda Arusha

Imagine kwa hii thinking wewe ndo unanafuu... imagine wewe mwenye nafuu unaowazidi ndo hao wengine ma DC, RCs, Mawaziri nkt. Imagine hii thinking inatawala na kubuni mbinu za mwafrika kutoka hapa kuelekea pale...

Naungana na waliowahi sema "Mwafrika bado sana hajaweza kujitawala"
 
Dada angu wewe huwezi kuelewa hizi mambo
 
Mkuu unachosema ni kweli, ila mleta mada kasema pamoja na mapungufu yote aliyo nayo Makonda kwa hili ni ubunifu wenye tija kwa Taifa.

Na ni kweli!!

Mkuu ukumbuke kuwa hata saa mbovu kuna muda husema majira sahihi.
Mi sikatai lakini mwendelezo wake ni upi?
 
Oooh sawa. Ila hata kwa kulichukua na kulifanya liwe namna lilivyofanywa anastahili pongezi zetu.

Nategemea kuwaona Mawaziri wa Utalii na Habari wakishiriki kulipa publicity kubwa hili tukio ili liwe na manufaa tuliyoyasema humu.
Kwanini sasa litafanyika Mjini kuleta usumbufu wa foleni badala ya kufanya huko mbugani ili kutangaza huo utalii vizuri?
 
Kwanini sasa litafanyika Mjini kuleta usumbufu wa foleni badala ya kufanya huko mbugani ili kutangaza huo utalii vizuri?
Nimesikia kesho wana ratiba ya kwenda mbugani.

Ni jambo zuri usumbugu mdogo lazima utokee. Tutizame faida yake zaidi
 
Pongezi nyingi kwake,
Nimesikia akisema kuwa;
1. Nov kuna Balloons Festival, kwamba ballons Parachuti zote za Africa Mashariki zitahusika.
2. Dec kuna Festival nyingine inayohusu mataifa zaidi ya 12 na hayo mataifa yataonesha culture zao kuanzia vyakula hadi mapambo katika mtaa watakao gaiwa hapo mjini kati Mwezi huo.

Nasikitika Ma RC kama Chalamila anashindwa hata kukusanya watu kusema Beach festival watu wakakusanye uchafu kule kusafisha fukwe zetu, mahala kama Dar ndipo angeweza kufanya wonders lkn bahati mbaya ubunifu umeishia kwenye kucheza Singeli!
 
Kwa kweli kwenye haya anastahili pongezi zetu. Sekta ya utalii Tanzania inahitaji vitu vingi kufikia it's potential na kimoja wapo ni publicity na matukio ya namna hii
 
of course amefanya kitu kizuri. naamini waingereza watakuwa wameona namna landrover ilivyopiga promo na wanaweza kusapoti mwakani.
 
Kama wana business analyst mzuri anaweza washauri wawe na kiwanda kabisa hapa Tanzania as inawapa picha kuwa gari zao zinapendwa na kukubaliwa pia
of course amefanya kitu kizuri. naamini waingereza watakuwa wameona namna landrover ilivyopiga promo na wanaweza kusapoti mwakani.
 
Wajinga ndio waliwao

Tuna safari ndefu sana ya kujitambua

Umejiuliza nani amefadhili hili?
Kwa pesa ya nani? Kwa faida ya nani? Why now?
Endeleeni kusifu na kuabudu.

Huyu na matukio yooooote bado mnamsifu ?
Kuna watu wanalia usiku na mchana kwa kudhulumiwa mengi ninyi mpo humu kumshangilia kafanya jambo. Lipi jambo?

Tuombe Neema ya Mungu kwa Taifa lipate kukombolewa.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika mwenyewe.
 
Kama wana business analyst mzuri anaweza washauri wawe na kiwanda kabisa hapa Tanzania as inawapa picha kuwa gari zao zinapendwa na kukubaliwa pia
hizo defender zilishastop kuzalishwa, hazizalishwi tena na hawategemei kuzalisha kama hizo. siku hizi zipo zile soft ambazo moja inauzwa milioni kama 400 za kitanzania, ambapo hata wakiweka kiwanda hapa bongo hakuna atakayenunua. kuweka kiwanda hua wanaangalia na wateja wao. wanachotakiwa kufanya hapo, ni kulenga kutangaza utalii na kuwavuta landrover wawasponse kwenye festive zingine na kwenye mashindano mengine. manake hapo tumewapiga bao hata wakenya hawajawahi kuwa na icho kitu.
 
Reactions: Cyb
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…