kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Kwa mara ya kwanza Tanzania inaandika historia chini ya Rais Samia Suluhu kwa kutekeleza ujenzi wa Kilometa nyingi za barabara kwa wakati mmoja. Serikali inaenda kutekeleza miradi mikubwa yenye Jumla ya kilometa 2035 ambayo itaanza kutekelezwa Kwa wakati Mmoja na itagharimu shilingi trillioni 3.7.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2023/24.
Sambamba na ujenzi wa miundombimu ya barabara, serikali imeendelea na ujenzi wa madaraja makubwa pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR. Uboreshaji wa miundombinu unaunganisha nchi na kufungua fursa za kiuchumi kwa kurahisisha usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa na malighafi.
Hakika awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu hakuna kilichosimama, utekelezaji unaendela na kazi inaendelea.