Pesa inasadia kuleta furaha, LAKINI sio wakati wote na sio kila kitu.
1.Umepata vihela vyako unamwambia bebi wako anakuambia hataki kuolewa Kwa Sasa kumbe yupo na bodaboda, hapo unemnunulia vizawadi vya gharama.
2 una Pesa za kutosha LAKINI umepigwa marufuku kutumia vyakula vya sukari sijui chumvi, yaani afya mgogoro.
3.Hii Pesa iliwahi kunitesa sana mwaka fulani maeneo ya shinyanga vijijini kwenye project fulani Pesa tunazo LAKINI hakuna hoteli wala mgahawa au gesti. Shida kubwa ikawa maji yakunywa hayapo kwa maduka yao. Mifukoni tuna hela lakini huduma hakuna mpaka tunamaliza ile project tulijifunza kuishi kama wanavyoishi wao. Kushea maji na wanyama
4. Pesa inafaa sana ikutembelee wakati ukiwa timamu kimwili na kiakili yaani huna stres una furaha vitu vinapatikana nk. Ni maoni TU.