Kwa maswali haya sensa imefeli kabla haijafanyika!

Kwa maswali haya sensa imefeli kabla haijafanyika!

Kwanza maswali ni mengi bila sababu ya msingi halafu mengi ni ya kijinga na kipuuzi. Ingewezekana kabisa kuwa na dodoso lenye maswali machache na ya msingi. Baadhi ya maswali wangeachiwa watendaji wa mitaa/vijiji wakisaidiwa na wenyeviti wao kwani ni ya kifamilia zaidi na yanahitaji utulivu.

Kwa ufupi hii itakuwa sensa ya hovyo kabisa kufanyika nchini na itachukuwa muda mrefu bila sababu yo yote. Wananchi wengi watayakwepa au kuyapuuza baadhi ya maswali kwa kusema uongo!

PIA, SOMA:
- Maswali 100 ya sensa ya watu na makazi ya mwaka
Ni ya kipuuzi kwako usiyejua maana na manufaa ya sensa.
 
Unafahamu kitu inaitwa skip katika utafiti? Si kila mtu au kila kaya inaulizwa maswali yote.
Kwa hali hiyo yalitakiwa yawepo madodoso tofauti!
 
Afadhali wewe unafikra chanya si Ileje mwenye mawazo mgando. Kukujibu, ni kuwa maswali ya muhimu ni mengi na ukitaka yote yaulizwe ni gharama kubwa sana. Usisahau kuwa swali moja ni sawa na billion moja. Mfano Uhusiano na mkuu wa kaya gharama yake ni billion moja
kolola ni mburula!
 
Kwa hali hiyo yalitakiwa yawepo madodoso tofauti!
Usisahau wanatumia tablet si kutumia makaratasi. Miaka ile tuliteseka sana na makaratasi. Hayo maswali ni traditional Censuses questions na yamejikita katika Population, Fertility, Mortality and Migration kama kawaida ya kila sensa duniani.
 
Dah inasikitisha jinsi comments zilivyo, watu bado hawajayaelewa maswali wala umuhimu wa sensa....sijui ni kwa makusudi au ni kiwango kidogo cha uelewa wa kupambanua mambo. Sad
 
Kwa vile wewe hujui haya masuala. Kila mtu na profession yake, hii ni yangu bwashee
Kama wewe ndiye professional basi tuna safari ndefu katika kuboresha mfumo wa elimu yetu!
 
Hivi katika hali ya kawaida kabisa unaweza kukaa kumuuliza mtu maswali 100 mfululizo ukitegemea matokeo chanya ya unachokifanya......wote muuliza maswali na mjibu maswali hadi mnakamilisha maswali 100 wote mpo hoi na fatigue na kizunguzungu juu...
 
Ndiyo tatizo la ku-copy na ku-paste kutoka madodoso ya watu wa nchi zilizoendelea.
 
Hivi katika hali ya kawaida kabisa unaweza kukaa kumuuliza mtu maswali 100 mfululizo ukitegemea matokeo chanya ya unachokifanya......wote muuliza maswali na mjibu maswali hadi mnakamilisha maswali 100 wote mpo hoi na fatigue na kizunguzungu juu...
Si rahisi mtu mujibu maswali yote mkuu. Yaani mtu ajibu maswali ya uvuvi, kilimo, uchimbaji madini n.k. Pia kuna maswali karani mjanja atapata majibu kwa urahisi akifika kwenye Kaya husika
 
Nashangaa kwanini watu wanataka kukwamisha zoezi kwa kusema uongo. Hizi takwimu zitatumiwa na serikali yoyote itakayokuja hata kama yule unayempenda awe rais atatumia takwimu hizi kuleta huduma. Ni muhimu sana sema watu mnajichanganya tu na mambo mengi.
Wao takwimu za tozo mbona wanatuongopea. Zile takwimu ni muhimu kuliko kutuhesabu na kwa minajili hio tutawaongopea tu
 
Back
Top Bottom