Wa kutegua ndio wahusika wenyewe.
Mfumo wa utekaji ulitengenezwa, na haujafutwa. Kadiri dalili za kutokubalika zinavyozidi, imebidi watawala kuzidi kuutegemea mfumo huu.
Mfumo huu wa utekaji haukutengenezwa na JPM, labda yeye aliukomaza tu. Kikwete aliutumia, JPM aliutumia sana na kuupa nguvu zaidi, na mama naye inaonekana kadiri siku zinavyoenda anazidi kuupa nguvu, ndiyo maana hata wake vinara wa uharamia wa utekaji amewarudisha kwenye Serikali yake.
Uharamia huo hakuuanzisha JPM, yeye aliukuta, akauimarisha na kuupa nguvu zaidi. Akina Ulimboka, Mawazo, n.k. walitendwa na Kikwete, siyo JPM.
Akina Lisu, Mo, Roma, Mdude, Azory, Ben, Kanguye na wengine wengi, ni wakati wa JPM. Wakati wa JPM, waliouawa walifungwa kwenye viroba na kutupwa baharini.
Akina Sativa na hawa wengine wa sasa, ni wakati wa Samia, na orodha inaendelea. Sijui atafikia wapi!! Wakati wa Samia, wanaouawa inaonrkana miili yao wanapelekewa fisi, ref. case ya Sativa.