Kwa mshahara gani viongozi wa sasa wananunua nyumba za bilioni 25 uko Dubai?

Kwa mshahara gani viongozi wa sasa wananunua nyumba za bilioni 25 uko Dubai?

Kwa hiyo tuwe tunahukumu watu bila ushahidi?Yaani mjinga mmoja akikurupuka tu tukukamate na uwekwe ndani.Hata China wafujaji wa mali ya umma na wala rushwa wanapigwa risasi lakini ni baada ya kufikishwa mahakamani.
Tatizo tz ni nani wa kufuatilia huo ushaidi. Okay, Kigwa keshasema, sasa unadhani ni jukumu la nani kuthibitisha lisemwalo. Labda km wewe siyo raia wa tz. Wa tz wanafahamiana vyema kwa tabia zao, mienendo na akili zao.

Okay, let's assume ni kweli mhusika unadhani atafanywa nini, na nani. Wewe endelea kulilia ushaidi siku ukishtuka ................
 
Unauliza mshahara hakuna mwanasias maskini... Mkiandamana mkivunjwa miguu ,wanasiasa wanaenda kutibiwa Dubai wewe pale Muhimbili.
 
Mbona hiyo nguvu ya umma haifanikiwi Tanzania ? kwa kuna ni Tanzania ambacho ni kikwazo.
Swali zuri mno. Kikwazo ni raia. Hatujitambui. Kuna mzee mmoja, ni marehemu sasa hivi, siku moja aliniumbua sana. Nilisema hivi ilikuwaje waarabu wanakuja kuchukuwa watumwa, wanawafungasha bogi la mstari mrefu wakati wenyewe wako watatu tu na raia wanakaa kimya? Akanijibu mbona siku hizi polisi anafanya unyama mtaani, anaua raia bila kosa na sisi tunakaa kimya?
 
Bila kuleta ushahidi wa kutosha kwenye hii kauli yake hiyo ni hearsay.
Kama waziri wa zamani angekusanya hizo facts zake na kuleta habari kamili yenye ushahidi.Asipofanya hivyo hizo ni kutupa jiwe baharini na kutegemea italeta mabadiliko.Hamisi ashaauriwe aache tabia ya kuropoka bila hard facts.Inashusha hadhi yake na kuonyesha uwezo wake wa kufikiri ulivyo mdogo.
Kimsingi huyu Hamisi hana hadhi yoyote ya kumfanya kuwa mbunge achilia mbali waziri. Ni mfumo songombingo wa nchi ndiyo umemfanya akafika hapo. Halafu hawa ni wale watu wa ''nitokeje leo''? Ila hilo la viongozi kuwa na nyumba za gharama ni ukweli sema tu hawezi kusema kwani wote ni mafisi na hupiga kelele yanapokuwa hayako kwenye ulaji.
 
Tatizo tz ni nani wa kufuatilia huo ushaidi. Okay, Kigwa keshasema, sasa unadhani ni jukumu la nani kuthibitisha lisemwalo. Labda km wewe siyo raia wa tz. Wa tz wanafahamiana vyema kwa tabia zao, mienendo na akili zao.

Okay, let's assume ni kweli mhusika unadhani atafanywa nini, na nani. Wewe endelea kulilia ushaidi siku ukishtuka ................
Wacha kuleta sweeping statements za watanzania tunafahamiana.Ukileta acussations zozote basi burden of proof ipo juu yako.Hivyo ndio inavyotakiwa iwe.Tusiwe jamii ya watu inayoaamini katika kupakaziana na kuamini majungu.
Tuache assumptions kwamba itatokea nini?Leta ushahidi madhubuti halafu tutavuka hilo daraja baada ya ushahidi kuonekana.
 
Ila Kigwa huwa na nongwa sana ni yeye ndiye alimtoa kwenye ramani na Dr Mwaka.

Yeye si ndiye alituambia CCM kwa sasa imerudi kwa wenyewe!!

Hao ndiyo wenyewe halafu anaongea kwa kujiumauma kama yule aliyetuambia kuna pesa "pre bargaining" zimefichwa China bila kututajia mfichaji.

Hizi ni porojo tu za kuibua mjadala isiyo mbele wala nyuma.
 
Sasa wananchi wafanye nini?! [emoji3][emoji3][emoji3]

Wakiandaa mapinduzi na mbinu za kimyakimya mashushu waliowekwa kuilinda system ya wizi ya CCM wamejaa kila kona... mwisho wa siku yanabumburuka mnatekwa mnaenda kuteswa na kuuwawa kusikojulikana na hao usalama wa CCM.

mkitaka kuandamana WAPUMBAVU na wao wanamwaga wanajeshi wao siku husika wafanye usafi.

Mkilalamika mitandaoni mnafuatiliwa mnakamatwa mnapewa kesi au mnapotezwa.

Mkitaka kuiondoa CCM kwa njia ya uchaguzi wanageuza tu maana wao ndo wanaoamua. Hata kama wameshindwa uchaguzi, kulia inaenda kushoto..., kushoto inaenda kulia matokeo hadharani CCM inaendelea kupeta. Mfano:- (2015)

Mkitaka kukimbia nchi mnawekewa vikwazo... kupata passport ni kama kupata madini ya tanzanite au almasi

Ajira wanapeana wao kwa wao.

Wananchi wafanye nini?!


Kwa hoja hii ina maana Wananchi wa Tanzania ni wafungwa huru? Au ni wafungwa wanaoota wapo huru?
 
Mbona mnajitekenya
Lizone kanunua nyumba ya billion 10 Dubai
January 2023 kamunua masaki jengo la billion 8 na falme za kiarabu ya billion 40.
Mtoto sa Saammbili kanunua jengo la billion 20 Dubai.
Laurance mafuru kanunua jengo masaki la billion 8...
Wengine nitawataja baadaye
 
Mahojiano ya Daktari Kigwangala yametupa ufunuo na kutupa maswali inawezekana vipi Kiongozi wa Tanzania akanunua nyumba shilingi bilioni 25 uko Dubai,na wengine wamenunua nyumba za bilioni 6 Masaki,je wamelipwa kitu gani hadi wamepata pesa hizo,je wameuza nini hadi kupata fedha hizo!? Je ni bandari,Mlima,Mbuga au madini!?

Na ndiyo wasioelewa waelewe sasa ni kwanini watawala na viongozi hawa wezi wa mali ya umma wanatumia kila njia haramu kubaki madarakani...

Ndio wasioelewa waelewe sasa kuwa ni kwanini watawala hawa wezi wa mali za umma wa Watangnyika wameamua kuamuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kukabiliana na waandamanaji wa maandamano yatakayoongozwa na CHADEMA tarehe 24/01/2024 hapa DSM ili kudai UHURU na HAKI katika nchi yao.

Ni kwa sababu hawapendi wananchi waujue uovu wao. Wanataka kubaki kwenye madaraka hata Kwa kumwaga damu.!

Ila tunawatahadharisha kuwa, hakuna uovu utakaoachwa pasipo kufunuliwa na kuwekwa wazi ili dunia na mbigu zote zione na wahusika walipe gharama yake.

No evil acts will go unpunished. Kila tendo ovu lazima lipate hukumu yake!!
 
Mahojiano ya Daktari Kigwangala yametupa ufunuo na kutupa maswali inawezekana vipi Kiongozi wa Tanzania akanunua nyumba shilingi bilioni 25 uko Dubai,na wengine wamenunua nyumba za bilioni 6 Masaki,je wamelipwa kitu gani hadi wamepata pesa hizo,je wameuza nini hadi kupata fedha hizo!? Je ni bandari,Mlima,Mbuga au madini!?



CHUKUWA CHAKO MAPEMA C C M
 
IMG_8148.jpg
 
Yes mkuu, Tiss ipo kulinda status ago, tiss ya uhalika iliyokuwa na heshima ni ya awamu ya kwanza tu,zingine wapigaji tu

Hiyo ya awamu ya kwanza ilikufa over a night?

Hiyo ya awamu ya kwanza inajitoa vipi kwenye Haya yanayoendelea ilhali wao ndio waanzilishi?

Hao “wazee wa hiyo awamu history zao katika uwajibikaji zikoje? Na matokeo yake leo hii yakoje?

Yakichunguzwa vizuri Haya mashina ni wazi hao “wazee watakutwa wakiwa sehemu ya mizizi.
 
Ukifahamu hayo utafanya nini?au ndio ushujaa wa key boards

tukiwajua na familia zao zikijua kuna msaada pia hata kama hatuna cha kuwafanya, vizazi vitaandika na ni aibu kwa familia zao maana jamii inajua ustawi wao unatokana na wizi wa mali za umma.
 
Back
Top Bottom