Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

Elimu tatizo..tunafundishwa njia za kuajiliwa na sio njia za kujiajiri..Kwa ugumu wa maisha haya watu wata jitokeza
 
Sasa unamlipa mtu 130,000/= hiyo motisha ya kufanya kazi anaitoa wapi?

Anafanya tu bora liende ila ukimlipa vizuri na kuset rules zako kazi zinafanyika vizuri tu.
Mtanzania kadri unavyomlipa mshahara mkubwa ndio anazidi kuwa mvivu.......

Mshahara haumpi Mtanzania motisha ya kazi bali unampa nafasi ya kuwa mzembe na mwenye kiburi kazini....

Naongea kutokana na uzoefu
 
Umeona point mkuu.
 
Kampuni ya WCB wasafi, inawafanya kazi zaidi ya 50 lakini wanalipwa vyema hakuna malalamiko.

Platnumz hongera kwa hilo. [emoji4] [emoji377] [emoji377]
 
General Mangi,

Hakuna Bepari ambaye ana huruma na yupo kwaajili ya kuboresha maisha kwa wafanyakazi wake hata siku moja,alwazy a capitalist want to maximize super profit bila kujali maslahi ya wanao umia.Ukiona mtu tajiri lazima kuna watu wananyonywa
 
Mleta uzi alicho shauri ni hiki; serikali isiwe busy tu na Mange Kimambi, ikomae na wafanya baishara wasio fata sheria, kima cha chini cha mshahara Tanzania kinajulikana.
 
Hii ni outcome ya umaskini wa kutupwa unaolikabili Taifa hivi 130000 ni nini kwa maisha ya sasa ? Na si Bakhresa na Dewji tu makampuni kibao wanafanya. Huu unyonyaji mfano .Kagera sugar na Mtibwa sugar kuna.watu wanalipwa. 100000 kwa. Mwezi .Can you imagine how this guy survives ? .........Bado tuna safari ndefu sana aisee kama Taifa..........Taifa la watu wasio na future ya maisha mazuri..........Lost souls with no hopes .........
 
Hao ni wanyonyaji wakubwa ndomana wanatajirika

Ova
 
Mkuu ,wewe unawashangaa hao tu?
Yapo makampuni mengi sana yanayo wanyonya wafanyakazi ,jaribu kufanya utafiti machozi yatakutoka.
---
 
Mkuu mi naamini wewe ni member wa muda mrefu humu unajua kutofautisha baina ya kitu official na habari ambayo haijathibitishwa.

Unawezaje kutoa habari ya ZoomTanzania na kuifanya kama ushahidi wako? Kila mtu hata mimi na wewe tunaweza tukatengeneza Account ZoomTanzania na kujifanya kama Mo.

Sijawahi fanya kazi A one ila nimewahi fanya kazi moja ya Kampuni ya Mo. Jamaa mishahara yake ni midogo ndiyo lakini watu wanapata hela ya kuishi hapa mjini.

Kwa Mo kazi ya kufanya mtu mmoja wanafanya watu wa 3 au 4. Ofisi zake hazina tofauti na za serikali watu wanaenda saa 3 au 4 asubuhi, mtu anatoka muda anaotaka, unaweza hata usiende kazini na mtu asijue,

Akiamua mo anaweza lipa mishahara ya 1m+ na kupunguza nusu ya wafanyakazi wake na wala hatayumba sababu wapo watu kibao hawana kazi kwa mo wanakesha tu na kupiga stori.

Pia Hao madereva unaowasema wana mishahara yao ya mwezi ambayo ni midogo kama laki 2 hivi, wana allowance kubwa kutegemea na kazi ila dereva mmoja anapata hadi laki 1 na nusu kwa siku kutegemea na kazi. Ni kawaida dereva kutengeneza milioni moja kwenye allowance nje ya mshahara wake, sisi wenye vidigrii vyetu tunawaonea wivu.
 
Woga wa kujitegemea unatugharimu sana!! Hivi mwanamume mzima huwezi ukafanya shughuli yako binafsi na kupata hiyo laki na 30 kwa mwezi mzima?
Naamini utapata zaidi ya Mara mbili ya hizo!!! Hao matajiri kupe watoseni tuone watafanya nini! Wakiajiri mh*ndi mwenzao wanamlipa vizuri! Wakiajiri mbong* wanampunja!
 
hicho wanachokifanya ni ukwepaji wa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…