Tayukwa
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 2,178
- 4,410
Tuungane ili kuondoa yale maswali ya NINA MTAJI WA SH........... Naomba mnishauri nifanye biashara gani.Wazo zuri sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuungane ili kuondoa yale maswali ya NINA MTAJI WA SH........... Naomba mnishauri nifanye biashara gani.Wazo zuri sana
Kweli kabisa......Tuungane ili kuondoa yale maswali ya NINA MTAJI WA SH........... Naomba mnishauri nifanye biashara gani.
Mkuu siamini hilo ulisemalo, kwani namba zote zipo hewani 24 hrs labda suala ni network tu na siyo km simu imezimwa.Nimepiga number zote izo hamna inayopatikana, hii issue ni serious kweli
Hahaha hahaha ha au km wale kina.....Nimepiga number zote izo hamna inayopatikana, hii issue ni serious kweli
Aikina Nani, malizia hapo mkuu plzHahaha hahaha ha au km wale kina.....
Hat m nmejrbu haziptkn cdhn kma useriouc upo hapNimepiga number zote izo hamna inayopatikana, hii issue ni serious kweli
Ahsante sana mkuuTengeneza kipato cha Ziada Kwa kupata kitabu maalumu kitakacho kufanya ujue kutengeneza bidhaa mbali mbali muhimu za viwamdani nyumbani kwako na uweze kujiajiri. Kitabu hicho utakipata Kwa bei ya TSh.5,000 tu! Katika email au whatsup yako. Nipigie au whatsup 0762208190 AU 0718978295. Utachagua unacho taka kujiajiri kitaalam kupitia kitabu hicho.
Tena akiwepo tabora akaeka kijiwe cha ukwel cha chips atapata hela vizur tuKua muwazi ni jambo Jema dogo, ila sasa yakupasa kueka wazi details like uko wapi,mjini au kijijini? Unapoishi ni kwako au umepanga? Hii itatusaidia kukushaur ww.
Kwa mfano uko kijijini na unaishi kwenu na Kuna eneo ambalo unaeza fuga kuku wa kienyeji huku unafanya shughuli nyingine kupata pesa ya kuwalishia kuku.
Kama uko mjini let's say Dar, unaeza tafuta kakijiwe ukaanza kukaanga chips kwa Huo mtaji Mdogo ulionao, unaeka chips na unadamka asbh unaanza kukaanga mihogo kwa ajili ya breakfast, saa nne tunaanza menya viazi kiasi kwamba saa tano chips tayar.
Kua msafi na wajali Wateja, naamini hadi umejiunga Jf Basi hata kama hujasoma sana lkn una uelewa mkubwa. Tumia akili yako kua mbunifu.
Katika kufanya yote usimwangalie mtu au kuwaza fulani atakuonaje, cha msingi zingatia unataka Kufika wapi.
Kukutia moyo tu, mm nlishauza chips nkiwa na degree moja lengo likiwa kupata mtaji wa kufungua kampuni ya ujenzi, nliuza for only one year huku nikilima na kufuga broilers ambao pia Nlikua nkiwakaanga hadi Miguu na vichwa vyao (vigondi) na kukamua utumbo wa kuku bila aibu, nliwauza masista duh na braza men kibao bila kujali tena kwa kuwaheshimu.
Boda Boda na dereva bajaji walikua wakiniagiza na kuntumikisha Lakini nliwaheshimu kwasababu ni Wateja, ktk kufanya hiyo kazi sikuwahi kuiwazia degree yangu hata chembe zaid ya kuwazia nataka Kufika wapi.
Baada ya mwaka mmoja nlianza usajili wa kampuni na baadae Mungu akanjalia nkavuna alizeti gunia 156 nkauza kila gunia elfu 54.
Nlitamani niendlee na chips Lakini nkaona hapana ngoja nkaitendee Haki ile degree. Ila kulima sijaacha had wa leo. Namshukuru Mungu ya Jana Si ya Leo.
Nimekupa kidogo tu ili usife moyo na uamini kila kitu kinaezekana