Kukodi ?
Kulima = 40,000
kupanda = 15,000
kupalilia = 80,000 ( kama pana rutuba palizi huwa 2 kila moja nimekadiria 40,000
kulinda = 50,000 (makisio)
kuvuna = 100,000 (kuvuna, kukusanya na kupiga)
usafiri = 80,000 (hapa itategemeaa ukiyatoa shamba unapeleka home kusubiri soko au unapeleka sokoni, gharama zinaweza kuzidi.
magunia tupu = 40,000
unaona, inakaribia 500,000 ingawa haya si mahesabu rasmi. Ningekushauri umtafute mkulima mkweli wa eneo lile akupe picha kamili ili uone kama inawezekana. 300,000 haitoshi.
Mkuu umenipa angalizo zuri,ingawa kwenye kupalilia,kulinda na kuvuna umeweka makadirio ya juu mno!huku kwa kupalilia ni 15,000 mpaka 20,000 kwa heka,kulinda ni kama 20,000.
Na ni makubaliano unaweza lipia baada ya mavuno,kuvuna kwenyewe ni 25,000 mpaka 35,000 kwa heka,na kuifadhi nitaifadhi kama umbali wa km 6 kutoka shambani,asante kwa angalizo ndugu yangu