Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kukodi ?
Kulima = 40,000
kupanda = 15,000
kupalilia = 80,000 ( kama pana rutuba palizi huwa 2 kila moja nimekadiria 40,000
kulinda = 50,000 (makisio)
kuvuna = 100,000 (kuvuna, kukusanya na kupiga)
usafiri = 80,000 (hapa itategemeaa ukiyatoa shamba unapeleka home kusubiri soko au unapeleka sokoni, gharama zinaweza kuzidi.
magunia tupu = 40,000
unaona, inakaribia 500,000 ingawa haya si mahesabu rasmi. Ningekushauri umtafute mkulima mkweli wa eneo lile akupe picha kamili ili uone kama inawezekana. 300,000 haitoshi.

Mkuu umenipa angalizo zuri,ingawa kwenye kupalilia,kulinda na kuvuna umeweka makadirio ya juu mno!huku kwa kupalilia ni 15,000 mpaka 20,000 kwa heka,kulinda ni kama 20,000.

Na ni makubaliano unaweza lipia baada ya mavuno,kuvuna kwenyewe ni 25,000 mpaka 35,000 kwa heka,na kuifadhi nitaifadhi kama umbali wa km 6 kutoka shambani,asante kwa angalizo ndugu yangu
 
hela hii ungewekeza kwenye bustani ya lisilo zidi robo hekari ingekulipa zaidi kuliko hicho kilimo unachotaka kwenda. sikukatishi tamaa ila kilishaniliza kwa kiasi fulani.
vinginevyo kwa kuwa huna kazi kabisa basi fanya kwanza biashara ya kuku na huku ukiendelea kulima kwa kuwafata kijijini na kuwaleta mjini inaweza ikakutoa saaaana

Unaposema bustani labda kwa vitu gani mkuu?ushauri ni muhimu mkuu ili kuweza kujikwamua!
 
Vipo vingi mtu wangu chochot kinawezekana unachohitaji ni bidii yako mchicha ndani ya siku 45 unauza vitunguu ndani ya miezi mitatu carrot.

Sasa ukishindwa kabisa panda hata pilipli mbuzi hazina changamoto kubwa ndani ya robo hekari unaweza kuvuna debe za kutosha ukachanganyikiwa.

Hicho kilimo unachotaka kina hitaji mambo mengi kuzidi unavyoweza kufikiria na akili zako bora wanawake kidogo huwa wanahusisha mioyo yao wanaweza kufanikiwa.

Vinginevyo ni pm ili niweze kukupa alternative zingine za haraka
 
Mkuu umenipa angalizo zuri,ingawa kwenye kupalilia,kulinda na kuvuna umeweka makadirio ya juu mno!huku kwa kupalilia ni 15,000 mpaka 20,000 kwa heka,kulinda ni kama 20,000
na ni makubaliano unaweza lipia baada ya mavuno,kuvuna kwenyewe ni 25,000 mpaka 35,000 kwa heka,na kuifadhi nitaifadhi kama umbali wa km 6 kutoka shambani,asante kwa angalizo ndugu yangu

ngoja nikupe busu jingine la mwisho ; ni hivi

Kila unapojipanga kufanya shughuli fulani, hakikisha bajeti yako unaipanga juu ili ubaki kwenye lengo endapo mabadiliko yoyote yatatokea.

Kwenye hizi shughuli za bei makubaliano kuna mambo ya ajabu sana, mtu anaona unahitaji kupaliliwa anaamua kutaja bei yoyote bila kuangalia umejipangaje akijua huna ujanja ukiacha mazao yataoza shambani. NAKUTAKIA KILA LA KHERI
 
vipo vingi mtu wangu chochot kinawezekana unachohitaji ni bidii yako
mchicha ndani ya siku 45 unauza
vitunguu ndani ya miezi mitatu
carrot
sasa ukishindwa kabisa panda hata pilipli mbuzi hazina changamoto kubwa ndani ya robo hekari unaweza kuvuna debe za kutosha ukachanganyikiwa.
hicho kilimo unachotaka kina hitaji mambo mengi kuzidi unavyoweza kufikiria na akili zako bora wanawake kidogo huwa wanahusisha mioyo yao wanaweza kufanikiwa.
vinginevyo ni pm ili niweze kukupa alternative zingine za haraka

Asante mkuu, na kupm
 
ngoja nikupe busu jingine la mwisho ; ni hivi

Kila unapojipanga kufanya shughuli fulani, hakikisha bajeti yako unaipanga juu ili ubaki kwenye lengo endapo mabadiliko yoyote yatatokea.

Kwenye hizi shughuli za bei makubaliano kuna mambo ya ajabu sana, mtu anaona unahitaji kupaliliwa anaamua kutaja bei yoyote bila kuangalia umejipangaje akijua huna ujanja ukiacha mazao yataoza shambani. NAKUTAKIA KILA LA KHERI

Nashukuru sana ndugu yangu,nitayafanyia kazi maangalizo yako,kwa kweli ni ya maana sana tu
 
Wadau habari!jamani mimi ni kijana niliyemaliza elimu yangu miaka kadhaha (zaidi ya mitano) iliyopita!ila tokea wakati huo sijabahatika kuajiriwa,nimeshakata tamaha,na nimeonelea bora nijiajiri!nina mtaji wa Tsh laki tatu (300,000/=) na wazo kuu ni kuanzisha kilimo hasa cha mahindi na baadae mpunga hasa mkoani Morogoro,naomba maoni yenu wadau je kwa mtaji huo naweza kuanzisha kilimo kweli?asanteni

Dogo Kapuku83 pesa yako inatosha kulima eka moja ya nyanya chungu (Yebo yebo). Usihesabu gharama za kazi ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe. Kuna thread humu inahusu kilimo cha Nyanya chungu ifuatilie humu itakusaidia. Limia kwenye maeneo yenye umwagiliaji. Ukianza kuchuma utavuna mzigo wa kujaza canter mara mbili kila wiki. Utapata pesa hadi utashangaa!

Dogo Kapuku83 pesa yako inatosha kulima nusu eka ya Mpunga. Nenda maeneo ya Mvomero, Msowero, Mvumi, Ludewa ukakodi nusu eka. Kwa kuwa nusu eka ni eneo dogo ni wazi shughuri nyingi utazifanya mwenyewe kwa nguvu yako. Pesa yako laki tatu itatosha hadi unaingiza mzigo sokoni naitabaki kwa sababu eka moja ya mpunga kwa kulipia kazi zote hugharimu laki sita hadi saba. Nusu eka ukiitunza kitaalaumu utavuna gunia 15 hadi 18! Gunia la mpunga hutoa kilo 70 ukiuza kwa bei ya sh 1500 utapata sh 105,000/= kwa gunia! Ukiwa na gunia 15 ukiuza mchele utapata 1,575,000/=!

Hicho kipato cha mpunga kinawezekana na hiyo bei ya mchele ni wastani tu! Usithubutu kulima mahindi kwakuwa ni rahisi sana kupoteza pesa yako uliyoihangaikia kuipata. Kilimo cha mahindi kinategemea mvua ni cha kubahatisha sana. Nakutakia safari njema kuelekea kwenye utajiri wako! Ukitaka utaalamu wa mpunga au Nyanya chungu ni PM!
 
Mkuu wangu kubota hapa natumia simu,ila nita ku pm muda si mrefu!unipe mawazo mkuu wangu
 
Mawazo yako ya kuanzisha kilimo ni mazuri ila nina maswali mawili kwako.
1. Je, unaishi huko huko Morogoro?
2. Je, kama nikisema niongeze mtaji ili tushirikiane tuweze kulima hata ekari 10 utakuwa tayari? Maana mimi niko Dar na ninafanya kazi za kuajiriwa na kwa mantiki hiyo kama tutakubaliana katika hilo wewe ndiyo utakuwa msimamizi mkuu, japokuwa lazima nijitahidi kuja huko angalau mara moja au 2 kila mwezi.

Kama uko tayari tafadhali ni PM au nipigie 0767 591610 ili tuweze kupanga namna ya kuonana na kuweka mkakati wa jinsi ya kuanza.
 
Habar wakuu mim ni mwanachuo hapo mbeya must kama mnavojua maisha ya bumu yana mwsho wake sasa nlikuwa nmefikria nianzshe japo biashara il ncje juta hapo mbelen ..sasa wakuu n bishara ipi inalipa nfanye ila nlikuwa napendlea zaid ya kuchukua mzgo na kuuza papo hapo kwa sababu mda mwng nnakuwa bize na chuo ntashkuru kwa kuncklza wakubw naomb msaada wenu sana japo ata wa mawazo
 
Chonga kitanda na uoe tunawajua nyie huwa mnatusumbua sana na hzo bm zenu au tuma TIGO PESA nkuhfadhie mkuu
 
Back
Top Bottom