Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kama unania kweli ya biashara kanunue u- fresh ni maji yaliyowekwa ladha na rangi box(ice cream za wanafunzi) ni 4000tsh na zinakaa 100 na zinauzwa kila moja 100tsh.
100*100=10000
Hapo faida ni 6000

Haya kwa hy 50000
Nunua box 8 kwa 32000
Itabaki 18000
Kama unaweza kukomaa nauli kutoka tegeta kiwandani popote kwa dar haizidi 10000
Hiyo 8000 ongeza umeme nyumbani ili uzigandishe tayari kwa biashara

Box 8 * idadi ya pc 100=800
800*100=80000
80000-50000=30000
Faida ni 25000-30000

Aya kijana kazi kwako!
daa uko vzr
 
Kuna watu wanamshauri huyu kijana upumbavu mpaka unashangaa kama huu ushauri umetoka kwa mtu mzima mwenye akili timamuu au wale wenye mihemko?
Eti "nunua bando la halichachi, weka ufanye nauli ya kambini,ka beti n.k" wale wote waliomshauri hivi huyu kijana kwa mtaji wake wa elfu 50 nadiriki kusema ni WAPUMBAVU wa akili na kufikiri"
Kwenye Biashara hakuna ela ndogo ni wewe tu na juhudi yako ya kuitafutia soko tu.
Mdogo wangu, hongera kwanza na nakusihi usikatishwe tamaa na wapuuzi wachache wa JF, wewe umeonyesha nia na akili zaidi inayowashinda hata Graduate wabeba bahasha,zipo vingi vya kufanya ila nitaviorodhesha baadhi
* kama upo Dar amka asubuhi sana nenda katika masoko makubwa ya mitumba kama Soko la Ilala boma n.k muda huo ndio mitumba hufunguliwa na kuuzwa kwa bei nafuu sana, tafuta hata Nguo za watoto kwa buku buku na ukaziuze mtaani kwa kuzitembeza nyumba kwa nyumba hata kwa elfu 2 mbili tayari utakua unakuza mtaji wako taratibu Sana lakini wenye matumaini na kuendelea kujitanua.
*kwa kua sasa hivi ni msimu wa mihogo nenda sokoni asubuhi sana kanunue roba lako la mihogo (hapa yakupasa uwe makini ya kutambua aina ya mihogo kama ni mitamu + inaiva kwa haraka) nunua hata mihogo ya elfu 10 tu kwa kuanzia,
Karai lako La elfu 5 na kuni bila kusahau mafuta , anza kukaanga mihogo taratiibu utapata chochote kitu
*Nenda k/koo kwenye maduka ya vyombo ya jumla AU Maduka ya urembo na viatu (simple shoes za akina mama na watoto wa kike) kanunue vitu vichache tu na anza kuvitembeza na kuvikopesha kwa akina mama wa mitaani (hawa hupenda kukopa sana) alafu waambie utapitia kila siku buku buku, utajikuta unasogea
*tafuta karai size ya kawaida tu, nunua mafuta na uamke asubuhi kwenda machinjio ya kuku, nenda kanunue kuku huko hata kwa kuanzia na wa 3 sio mbaya mfano niliwahi nunua kuku wa kizungu kwa elfu 6, anza biashara mdogo wangu hapo hapo mtaani kwenu

Siku zote muheshimu sana Mtu anayeanzia chini kwenye biashara maana kiu yake ni kubwa mno kufikia mafanikio, naamini na wewe kiu hiyo unayo, Allah akuongoze vyema InshaAllah
Ubarikiwe san mkuu, ushauri wako nimeupokea na nitaufanyia kazi.
 
Kama upo maeneo yamjini hiyo Elfu hamsini yako atakusaidia vizuri sana kupata hela yamahitaj muhimu au hata kukuza mtaji wako fanya hivi ingia sokoni wanapofungua nguo zamitumba hasa zawatoto langua nabei yao mara nyingi nielfu mbili nanguo inakuwa inalizisha kutokana nahiyo bei kisha nawewe unaanza kuzitembeza humohumo sokoni kwabei zajuu zaidi kuanzia Elfu tatu nahata kuingia majumbani ilimradi uwe namoyo tu
 
Kuna watu wanamshauri huyu kijana upumbavu mpaka unashangaa kama huu ushauri umetoka kwa mtu mzima mwenye akili timamuu au wale wenye mihemko?
Eti "nunua bando la halichachi, weka ufanye nauli ya kambini,ka beti n.k" wale wote waliomshauri hivi huyu kijana kwa mtaji wake wa elfu 50 nadiriki kusema ni WAPUMBAVU wa akili na kufikiri"
Kwenye Biashara hakuna ela ndogo ni wewe tu na juhudi yako ya kuitafutia soko tu.
Mdogo wangu, hongera kwanza na nakusihi usikatishwe tamaa na wapuuzi wachache wa JF, wewe umeonyesha nia na akili zaidi inayowashinda hata Graduate wabeba bahasha,zipo vingi vya kufanya ila nitaviorodhesha baadhi
* kama upo Dar amka asubuhi sana nenda katika masoko makubwa ya mitumba kama Soko la Ilala boma n.k muda huo ndio mitumba hufunguliwa na kuuzwa kwa bei nafuu sana, tafuta hata Nguo za watoto kwa buku buku na ukaziuze mtaani kwa kuzitembeza nyumba kwa nyumba hata kwa elfu 2 mbili tayari utakua unakuza mtaji wako taratibu Sana lakini wenye matumaini na kuendelea kujitanua.
*kwa kua sasa hivi ni msimu wa mihogo nenda sokoni asubuhi sana kanunue roba lako la mihogo (hapa yakupasa uwe makini ya kutambua aina ya mihogo kama ni mitamu + inaiva kwa haraka) nunua hata mihogo ya elfu 10 tu kwa kuanzia,
Karai lako La elfu 5 na kuni bila kusahau mafuta , anza kukaanga mihogo taratiibu utapata chochote kitu
*Nenda k/koo kwenye maduka ya vyombo ya jumla AU Maduka ya urembo na viatu (simple shoes za akina mama na watoto wa kike) kanunue vitu vichache tu na anza kuvitembeza na kuvikopesha kwa akina mama wa mitaani (hawa hupenda kukopa sana) alafu waambie utapitia kila siku buku buku, utajikuta unasogea
*tafuta karai size ya kawaida tu, nunua mafuta na uamke asubuhi kwenda machinjio ya kuku, nenda kanunue kuku huko hata kwa kuanzia na wa 3 sio mbaya mfano niliwahi nunua kuku wa kizungu kwa elfu 6, anza biashara mdogo wangu hapo hapo mtaani kwenu

Siku zote muheshimu sana Mtu anayeanzia chini kwenye biashara maana kiu yake ni kubwa mno kufikia mafanikio, naamini na wewe kiu hiyo unayo, Allah akuongoze vyema InshaAllah
hakika hii forum ingekuwa na watu kama wewe hata 100 tu ingekuwa murua sana.
ZINGATIA HAYA KIJANA.
 
Jaman eh? Mlioweka namb zenu ni nani anayeadd watu ilo group? Km vp mnichek mm DM
 
Vipo ving ata taa za solar,VIATU vya wanawake, SAA za wanaume kwa mfano zinaweza kua na profit adi 50,000tshs
Vipi ushuru wake, najua solar products ni exempted lakini kwa viatu na saa sijui ni % ngapi ushuru wake.
 
Wakuu habar zaenu' poleni na majukumu ya kila Siku
Baada ya kukaa kwa muda mref nikitafakar ni Biashara ipi kwa hapa mjini Dar itanipatia kipato kizur kwa kuanza na mtaji Wa lak2 hv kugonga mwamba nimeamua kuleta Uzi huu kwenu mnisaidie katika kufanikisha jambo hili'' je kwa mtaji Wa laki 2 ninaweza kufanya Biashara IP kwa hapa dar
 
Haya magroup nayo somtimes wala siyo....yan huu uzi umehujumiwa na whatssap bila sababu yoyote yan....wakuu mliounda group la whatsap huko hebu rudini huku bana tujadilie huku,Mkuu mtengeneza uzi Mungu akupe kila lililo zuri na akuepushe na balaa zote za dunia ila mzee naona last seen january 2017..upo salama mkuu?
 
Wakuu mada kama hz n nzur sana, kuna watu wanaingia kusoma na kupata ideas hvyo n vema yakatolewa majibu yenye kujenga na kusaidia. Sisi wote n watanzanzania inabd tusaidiane vile tuwezavyo. Naona kama kuna watu wengine hawako serious vile. Ninaamn humu wako weng wenye mawazo mazur sana ya kujenga.
 
Back
Top Bottom