Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nina laki mbili,nataka kufanya biashara ya mtaji mdogo usiozidi ela hiyo kwa kuanzia,isiwe ya usimamizi wa moja kwa moja.Naombeni mawazo yenu.


!
!
Pasipo Kuuliza Zaidi. Chukua Hiyo Hela Nenda Nayo Kwenye Kijiwe Ah Chama Cha Bodaboda Wanakuwaga Na Shida Na Mrejesho Na imejensi Mbalimbali. Tengeneza Mfumo Mzuri Uwe Unakopesha Kati Ya 5 000 Mpaka 15 000 Kwa Muda Wa Wiki Moja. Weka Riba Rafiki
 
!
!
Pasipo Kuuliza Zaidi. Chukua Hiyo Hela Nenda Nayo Kwenye Kijiwe Ah Chama Cha Bodaboda Wanakuwaga Na Shida Na Mrejesho Na imejensi Mbalimbali. Tengeneza Mfumo Mzuri Uwe Unakopesha Kati Ya 5 000 Mpaka 15 000 Kwa Muda Wa Wiki Moja. Weka Riba Rafiki
Nashukuru,ni idea mpya kabisa hii,ngoja niifanyie kazi
 
Tafuta wamama wanaotembeza mboga na matunda,waongezee huo mtaji mgawane faida.
 
Mpaka hapo umeshafeli biashara tayari, hiyo pesa tafuta kitu kingine cha kufanya ila sio biashara. Pole sana mkuu.
 
Biashara ya kuchoma mahindi inapesa sana maeneo ya Kiborloni au Majengo utapiga pesa
 
mimi ninapesa takriban shilingi 700,000 nimepewa na baba nifanyie biashara likini bado sina idea ya biashara yoyote kwahiyo ninaombeni mnisaidie ideas zenu
 
Hakuna biashara isiyo na changamoto,nina uzoefu wa kutosha kwenye hii biashara na si risk kama zingine.....haikupi mawazo kwani haiozi isipokuwa inahitaji juhudi na ushawishi tu.
Mkuu mi nafkiria kufanya hii biashara, hivi balo la nguo za watoto ni kiasi gani?nilienda pale nikakutana na madalali nikaondoka,pili je hawabambiki na malonya hata ukichukua namba 1?
 
Habari Ndugu zangu,
Mimi nimekuwa nafanya biashara tofauti tofauti saana na Nashukuru Mungu nipo katika lavel ya kati ya maisha sikosi ninachihitaji hata kwa kuchelewa kidogo, nimekuwa nikitoa fursa kwa watu tofauti ili mradi tuongeze kipato cha maisha......

Naomba mtu anayejiamini kuwa ni mwaminifu (nitamfanyia uchunguzi wa kina) mwenye idea ya biasha za mtaji wa 500K - 1M aje hapa tupeane na tufanye biashara! unaweza pia kuni PM kama hutapenda kuweka jambo hili adharan
 
Namjua mtu ambae anafit kwenye hiyo offer yako 105% sema tatizo hayupo humu.
 
Hahaha uzi wako umeunganishwa
 
good sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…